Matangazo ya biashara ya vileo fb katikati ya posts za watumishi wa mungu kwenye akaunti zao: tunaionaje?

Matangazo ya biashara ya vileo fb katikati ya posts za watumishi wa mungu kwenye akaunti zao: tunaionaje?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
14,205
Reaction score
19,142
Kwangu huwa najisikia ukakasi wakati unasikiliza clip ya mafundisho ya Neno la Mungu aliyoposti mtumishi yeyote wa Mungu kwenye akaunti yake facebook au penginepo, halafu katikati ya mafundisho/mahubiri linaingilia tangazo la biashara lililo kinyume na imani ya mhubiri mwenyewe kama vile tangazo la pombe nk, kisha clip ya mafundisho inaendelea.

Ninachojiuliza:

1. Je mwenye akaunti hiyo ya Facebook ambaye ni mtumishi wa Mungu anakuwa ameridhia tangazo hilo la biashara na analipwa kwa tangazo hilo au hayo matangazo huingilia tu akaunti za watu bila ridhaa ya wahusika?

2. Kama anakuwa ameridhia haoni kuwa anashirikiana na shetani kuwezesha uovu ue ee kupitia marangazo hayo?

3. Kama anakuwa hajaridhia je hakuna namna ya ku-block matangazo hayo yasiingilie clip yake ya mahubiri/mafundisho?

3. Je pesa wanazopewa hao wenye views nyingi kwenye akaunti zao zina uhusiano wowote na matangazo hayo ya biashara?

4. Kama hakuna namna yoyote ya ku-block hayo matangazo yanayoingilia je kwa nini wahusika hawajawalalamikia facebook ikiwezekana kuwashitaki? Naomba kuelimishwa kwa anayejua mambo haya kwa usahihi.
 
Yaani gambe tu ndio unakuja kulalamika mkuu.... je zingekua zile za lile jukwaa lililo futwa sindio ungezimia kabisa....😜
 
Back
Top Bottom