Matangazo ya Mganga Radio Free Afrika

Matangazo ya Mganga Radio Free Afrika

gwego1

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2023
Posts
265
Reaction score
897
Wakuu habari.

Niko nasikilizia hapa radio Free!. Kuna kipindi Cha mganga anajinadi kuwa kama una tatizo lolote yeye atakusaidia kulitatua kwa kupiga namba ya sim Aliyoitoa.

Anasema kama unashida na Hela, cheo yeye anaweza kukusaidia.

Najiuliza hapa nikienda kwa huyo mganga na nisifanikiwe shida yangu Kuna namna naweza kuwadai fidia Radio Free? Maana watakuwa wamehusika kunielekeza mtu ambaye sio sahihi.

Nawasilisha.
 
Miaka 15 nyuma mtu angekuambia redio kubwa kama RFA itakuja fikia hatua ya kurusha matangazo ya waganga usingeamini kabisa.
Mkuu hiyo miaka 15 nilikaa mtaa mmoja na watangazaji wa RFA, Kiss na Star TV .Bwiru Place karibu na Stanley .Aisee walikuwa na majina makubwa ila walikuwa na njaa kali sana wangeweza kula hata magodoro.Walikuwa wamerundikwa kwenye nyumba ya Diallo pale kama wapo hostel.Sijui shida ni nini kwenye Media.
 
Safari bado ndefu mno!
Mpaka tuuache ujinga, uzuzu, undorobo, wenzetu watakuwa washatuvuna na kutajirika sana sana...
 
Nenda kwanza.acha lawama.
Kama ni tapeli utarudishiwa hela zako
 
Back
Top Bottom