Matapeli kwenye mitandao ya simu

Matapeli kwenye mitandao ya simu

Kitimoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2012
Posts
6,941
Reaction score
7,808
Hii thread ni maalum kwa ajili ya kuanika namba za simu za wanaotapeli kupitia huduma za fedha kwenye mitandao ya simu, naamini TCRA watakuwa wanapitia huu uzi, wangekuwa na Akaunti hapa JF kama Taasisi zingine ingekuwa vema.

0672388589 hii ni mojawapo ya namba inayotapeli, alinipigia simu akisema "napiga simu kutoka Vodacom, unatumia huduma ya MPesa", nikamwambia ndio. Akaniuliza mara ya mwisho kutumia huduma hiyo ilikuwa lini, nikamwambia leo, akaniuliza ulifanya muhamala wa kiasi gani, nikamwambia Dola Bilioni moja, akanitukana.
 
Hawa mbwa sijui wana ujasiri kiasi gani! Ukimpa ushirikiano, anakuoneshea upendo wa kipekee akijua mwisho wa siku atakupiga tu!

Ila ukimshtukia sasa mapema, na kujaribu kumpa ushauri wa kurudi kijijini kwenda kulima, ni lazima akutukane kwanza matusi mazito na ya nguoni, kabla ya kukata simu.

Halafu hata hawaishi, hawadhibitiki! Yaani wanaendelea tu kuwaibia watu kila siku. Hakuna cha polisi wala tcra wanao wamudu hawa matapeli!
 
TCRA: Line zote ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole zitafungiwa ili kuepuka matapeli.

TAPELI: ... Jina litatokea ....
 
Back
Top Bottom