Matapeli wa Simu wanazidi, licha ya simu kusajiliwa! Nani alaumiwe, Makampuni ya simu, TCRA, Polisi au Raia?

Matapeli wa Simu wanazidi, licha ya simu kusajiliwa! Nani alaumiwe, Makampuni ya simu, TCRA, Polisi au Raia?

MR.NOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
339
Reaction score
505
Wakuu hizi sms Mzee flani ni mganga maarufu, atakupa utajiri wa freemason, mara utajiri wa ndagu nk. sasa zimetawala sana, na hizi zingine za umeshinda milioni 700000000, piga Simu 0000 ili upate zawadi zako.

Au unapigiwa simu na litapeli likisema Kuna Hela imetumwa kwako kimakosa.

Simu zote zimesajiliwa sasa; nani alaumiwe kwa kushindwa kufuta hawa wezi?
 
Kusajili na kupata vitambulisho vya NIDA ni sawa tu kama ambavyo uwa tunakurupuka kufanya mambo. NIDA wenyewe sasa vitambulisho hawatoi tunaishia kupewa nnamba

TCRA bado wanashindwa daka watu hata baada ya kisajili namba kwa vitambulisho.
Nchi hii sijui ni kipi kiliwaho fanikiwa hata kwa 70%
 
Juzi nimetumiwa msg kutoka namba 0733 253 075
Ikisomeka

"Nitumie tu kwenye hii namba ya AirtelMoney (0784084548) Jina ni RICHARD MPATO"
 
Juzi nimetumiwa msg kutoka namba 0733 253 075
Ikisomeka

"Nitumie tu kwenye hii namba ya AirtelMoney (0784084548) Jina ni RICHARD MPATO"
Tatizo hata TCRA ukitoa taarifa za namba zinazo tapeli unakuta tena namba ile ile baada ya wiki inakutumia tena sms ya kukutapeli.
 
Sheria zilizopo ni kadamizi kwa wahanga wa utapeli na zinawafeva matapeli. Haya nilijionea kwa macho yangu wakati namsaidia mama mmoja msataafu aliyetapeliwa mil 14.9
 
Majuzi nilikuwa nimetoka kusajili laini ya hslotel (Mpya) baada tu ya kuiweka hewani sijakaa hata nusu SAA inaingia SMS ya kujiunga na Freemasons wametumia namba ya TTCL.

Hapo ndipo nilipoamini matapeli ni wafanyakazi wa kampuni za simu.

Mtu wa kawaida asiyejua A wala B hawezi kufanya hicho kitu.

Walijuaje kuwa hii namba iko hewani tayali?
 
Jamaa bado wanaendelea na huu upuuzi, sometime wanapiga simu wanajifanya wamekosea kutuma hela kwako, wakati mwingine wanatuma haya mameseji.
IMG_6705.jpg
 
Wanabuni namba na kujaribu. Ikitokea wamempata mtu hayupo makini ananasa kwenye mtego. Hatari sana. Tunazidishiana shida tu.
 
Jamaa bado wanaendelea na huu upuuzi, sometime wanapiga simu wanajifanya wamekosea kutuma hela kwako, wakati mwingine wanatuma haya mameseji.
View attachment 2065787
Ni mtu mjinga pekee anayeweza kushawishika na kutuma pesa baada ya kupokea meseji kama hii. Kwa ujinga huo, acha waendelee kupigwa tu mpaka akili zao zikae sawa
 
Nadhani ifikie tu wakati hiyo TCRA na polisi wajitokeze hadharani na kukiri waziwazi kushindwa kuwadhibiti hawa matapeli.

Ingawa kwa upande wangu naamini chanzo cha haya yote ni Makampuni ya simu. Kiufupi tu, yana mfumo mbovu sana wa kusajili line za simu, kiasi cha kuruhusu matapeli kuutumia mfumo wao huo dhaifu, kuwaumiza wananchi wasio na uelewa wa kutosha dhidi ya utapeli.
 
Jamaa wanatumia zaidi TTCL kutapeli watu.
 
Kama mwenye hii number 05674031816 ni mwizi, TCRA mfuatilieni huyu mtu
 
Back
Top Bottom