Matapeli Wamezagaa kupitia Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kuweni Makini

Matapeli Wamezagaa kupitia Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kuweni Makini

cemalema

Member
Joined
Feb 22, 2013
Posts
49
Reaction score
18
Ni taarifa kwa wanfanya biashara za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kuwa kuna vijana wanaotengeza mifumo ya wizi kwa mfano wanakuja kutoa pesa katika simu ya wakala inaingia sms yakuonyesaha kama amefanya muamala na kumtumia ujumbe wakala na kwake yeye kama amepokea sms ya kuonyesha floti imeongezeka ila akitizama kwa njia ya kawaida ktk sim ya wakala hakuna floti ilioongezeka wala kupungua na hizo sms zinakuja kama kweli ila ukitizama sms senta namba ni tofauti kabisaa na wanapendelea kutoa pesa kuanzia lakisaba au laki tano au hata milioni Mkoa wa Rukwa wametapeliwa sanaa na Mpanda
 
mobile money ni tatizo sana nafkiri wahusika wafikiri njia mbadala ya kuzuia money frauding
 
je akikutumia sms ongezeko la float ya wakala linaendana na salio lilokwepo kabla
 
Hivi unaweza kufanya money laundering kutumia mobile money?
 
je akikutumia sms ongezeko la float ya wakala linaendana na salio lilokwepo kabla

ndio.mkuu jamaa hua wanashirikiana na watu WA makao makuu,juzi Kati wamenipiga laki mbili na ishirini
 
Mkuu nashukuru kwa kuwajuza wadau. Ni kweli kabisa huu wizi upo. Mi mwishoni mwa mwaka juzi(2012) nilipigwa laki sita. Baada ya kufuatilia sana makao makuu ya tigo bila mafanikio ilibidi niwe mpole. Kitu cha kushangaza mesage iliingia kama meseji nyingine za tigopesa, na mbaya zaidi mesage inaonesha salio limebadilika sambamba kabisa kulingana na float iliyokuwepo. Watu wa kampuni ya tigo waliendelea kusisitiza kuwa mesej haikuwa generated na system yao bali matapeli. Nilielimishwa kuhusu reference namba iliyotumika, mwisho nikaishia tu kuwa mpole. Japo naamini kabisa hawa matapeli huwa wanashirikiana na watu wa makampuni husika ya simu. Nilifikiri kwenda TCRA kwa mawazo kwamba Tigopesa wanao wajibu wa kuhakikisha kuwa biashara wanayoendesha iko salama lakini nikaona nitazidi kupoteza muda. So wandugu tujitahidi kuongeza umakini linapokuja suala la pesa kwenye mitandao ya simu. Wajanja ni wengi sana na kina siku wanakuja na mbinu mpya
 
Back
Top Bottom