Kuna matapeli ambao wanajifanya wahubiri wa Neno la Mungu wapo jijini Dar es Salaam. Jamaa hao wanne wanaoishi Mbagala Rangi 3, wanaongozwa na Anton Abel Magoya ambaye anafahamika kuwa ni muhubiri katika makanisa kadhaa ya Dsm, pia alisoma chuo cha IFM. Jamaa wakikutana na wewe wanajifanya kuzungumza kuhusu masuala ya Mungu, ukionyesha dalili za kuwasikiliza wanakufuata kokote unakoishi hata ikibidi kuja sehemu unayosali. Wakati wa usiku watakutumia message na mistari ya Biblia ya kusoma na jambo la kuombea siku hiyo. Taratibu utajikuta mikononi mwao.
Jamaa mmoja na mchungaji wake wameshatapeliwa mamilioni ya shilingi baada ya jamaa hao kuahidi kusaidia kununua vifaa mbalimbali vya kanisa vikiwemo vyombo vya muziki. baada ya kugundulika kuwa ni matapeli wametoweka ingawa simu zao zinaita lakini hazipokelewi.
Binti mmoja ambaye nae ametapeliwa na jamaa hao, anasema kwasababu alikuwa anamfahamu kiongozi wa kundi hilo kuwa ni mtumishi wa Mungu hakuwa na wasiwasi wowote juu yake. siku moja jamaa alimwomba amwazime laptop yake, lakini ilichukuliwa na haikurudishwa hadi leo. Dada huyo amenipa picha ya jamaa huyo na namba yake ya simu.
Wote waliotapeliwa wameshatoa taarifa polisi na upelelezi unaendelea.