Wasalamu,
Kipo kisa kilichotokea juzi cha kujifunza. Kinahusisha wahusika wanne. Ambao ni binti, wakala, tapeli na boss wa binti.
Binti wa Kazi kapokea message kwamba katumiwa shilingi 750,000 kupitia namba hii 0672312375 ya tapeli, kisha tapeli kampigia simu binti kwamba amekosea kutuma pesa anaomba arejeshewe pesa hizo, binti kaambiwa asimwambie mtu yeyeto (kuuteka ufahamu) na aende kwa wakala akazitoe pesa hizo KISHA amuwekeek wenye namba hio ya tapeli.
Binti hana uelewa na aina hii ya utapeli kaondoka nyumbani kimya kimya asiwaambie watu kafika kwa wakala. Kafika kwa wakala kamwambia pesa ipo kwenye simu naomba nitumie pesa kwenye simu namba hii akaonyesha namba ya tapeli alikuwa kaiandika kwenye karatasi kisha atatoa hela hio laki saba unusu, wakala akasema hana kiasi hicho yaani lakini saba na nusu bali ana laki moja na nusu, huku tapeli Akiendelea kuongea na binti (kauteka ufahamu wake) akamwambia mwambie anitumie hio laki na nusu.
Wakala akamuuliza binti mara mbili mbili unayo hio hela binti akasisitiza ninayo kwenye simu. Kosa la wakala ni kuamini na kutuma pesa kwa tapeli bila kupokea pesa toka kwa binti. Hili ni kosa kubwa Sana wafanyalo baadhi ya mawakala ajapokea pesa toka kwa mteja anaanza kuruhusu muamala.
Baada ya tapeli kupokea pesa akamwambia binti mpe simu wakala, wakala kupokea simu tapeli akasema "mwambie huyo binti ameshatapeliwa" na wewe wakala ni mpumbavu na mjinga nishawatapeli unatumaje pesa kabla ujapokea pesa" kisha akakata simu.
Wakala akajaribu kuustopisha muamala tayari sekunde ulikuwa ushatolewa. Wakala kambana binti, binti kamuonyesha message aliyotumiwa hela, ni message ya kuforwadiwa yaani message feki. Means binti hana pesa hata mia mbovu.
Wakala kamuweka chini ya ulinzi binti akitaka ampeleke kwenye vyombo husika mabodaboda wakasema huyu binti boss wake tunajua ikashauriwa wamuone boss wake. Kufika kwa boss kuelezwa boss akamwambia wakala hivi inakuaje unatuma pesa KWA mtu na ujapokea pesa mkononi kwanza? Huo ni mzigo wako siwezi toa hata mia"
Wakala akajibu kwamba binti aliniambia pesa anazo kwenye simu atatoa na mimi nikaamini. Maamuzi ya busara yakafanyika kwamba wachangie hasara yaani binti alipe nusu na wakala alipe nusu kwa uzembe wake.
Mme wa boss alitaka alibebe jukumu hilo yaani ailipe hio hasara toka kwa binti wa wakazi sababu anajua ni ajali tu imetokea, mke akatia ngumu maneno yakataka kuzuka mke akatoa maneno mme ikabidi ajitoe na kusitisha mpango wa kuilipa hasara hio Ili dada wa kazi awe na amani, hofu ni mke asijesema anamtaka mdada wa kazi sababu mke ni fyatu achagui maneno.
Muafaka binti atalipa elf 80 badala ya mia 50. Binti kakubali atalipa kwa awamu. Mchana anapigiwa tapeli akapokea akaelezwa akataja ni wakala gani akatajiwa jina la wakala wa tigo aliyemtumia pesa kwenye simu yake 0672312375 (uzoefu anawatapeli wengi alipouliza jina la wakala), tapeli akakumbuka akauliza mpo wapi akaambiwa ni kituoni hapa tumemshikilia binti kwa loud speaker mazungumzo yakiendelea mbele ya wakala, binti na boss tapeli akasema "ni kweli nimechukua pesa huyo wakala ndie mjinga nishawatapeli na pesa sirudishi siwezi rudisha pesa nimepewa na Mungu tairudisha vipi?"
Akaendelea kupiga mkwara "huyo binti hana makosa mwachie mara moja la sivyo nitawafanyieni kitu mbaya," akatishia mikwara ya uchawi (ignorance) kisha akaporomosha Sana matusi mazito ya 5G akasema "nimewaonea huruma hicho kipesa kidogo tu ndo mnapiga kelele je ningechukua nyingi je?' Akaendeleza matusi mazito Sana kwa aibu tukakata simu.
Jana tapeli akapigiwa simu akapokea (sauti ni ya kiume, lafudhi si ya mjini) akaambiwa arudishe hio pesa.Tapeli akaporomosha matusi mazito ya 10 G, eti hawezi rudisha pesa aliyopewa na MUNGU. Tapeli akatumiwa message " tulikuwa na shida na sauti yako tushaikamata tumeihifadhi kwenye chupa inafanyiwa kazi tegemea ugeni "tapeli akapiga simu anabembeleza anaomba msamaha kwamba" msifanye chochote haya ni maisha tu tusimfanye chochote, anarejesha hio pesa."
Akaomba Sana kwa sauti ya huruma na upole atumiwe namba arejeshe hio pesa Ili asidhurike, huku kwa nyuma ikisikika sauti nyingine ya kiume "Hakuna kurejesha pesa hapa."
Tapeli akatumiwa namba Ili arejeshe hela kwa madai yake.
Baada ya kupewa namba akatuma message yenye kuonyesha hela imeingia, hio message ikaja kama zile za kampuni ya simu na sio kama private number (changamoto kwa watu wa IT hawa wanaingiliaje mifumo ya kampuni za simu) message ya hela imekuja kupitia nembo ya kampuni ya airtel na sio kwa private number, ilipoangaliwa salio lina soma sifuri.
Means katuma message hewa. Kumpigia simu akapokea akaelezwa akasema "mbona nimekurudishieni hela yenu si mlituma laki na hamsini na nane? Ndio hio nimerejesha kupitia" KISHA akaendeleza matusi mazito akisema "nawatapeli waganga, wanajeshi, mapolisi, mahakimu, mawaziri sembuse nyie" akaendeleza matusi mazito Sana.
Huku akichimba mkwara "ungekuwa mjanja usingetapeliwa kata simu nipo kazini nawatapeli watu nitoe kiwingu unanipotezea mda kuna Kazi inaingia hapa" then akakata simu. Jioni akapigiwa "eeh unasemaje nipo home nakula ugali na familia" inasikika sauti ya kike kwa nyuma. Nimeweka sauti yake iliyorekodiwa akijigamba, muamala feki aliourejesha, majina ya usajili ya namba hizo mbili ya tigo na airtel.
Changamoto kwa mamlaka husika police, mamlaka ya mawasiliano, kampuni za simu na vyombo vingine ni watz wangapi wanatapeliwa kupitia njia hizi. Kumbuka pana watu awajui haya mfano wadada wa Kazi wapeni elimu. Mtu yeyeto akikuambia jambo KISHA akakuambia usiseme, au message yeyeto ya pesa sijui nimekosea sijui nini wawe na uelewa, matapeli wazee wa ile pesa bado wapo kazini.
Namba yake bado ipo hewani na anapokea tu simu swali anajiamini nini? Je, ni ignorance? Je, pana watu wa kampuni za simu anashirikiana nao? Je, anaingilia mifumo ya mawasiliano ya simu?
Kwa mliotaka kutapeliwa hii sauti si ngeni, hata mimi sio ngeni kwangu. Nimeleta kwenu tuelimishane. Naambatanisha sauti Kati ya tapeli na mtu mwingine.