Duuh!.
Ukiachana na yote, tamaa pia huchangia sana. Mtu katumiwa sms ya Tsh 750,000. Tapeli atakachofanya atamuambia nenda ukatume Tsh 700,000, then hiyo 50k utatumia kama usumbufu..
Na anamtahadharisha sana asimuambie mtu yeyote. Wanamkamata mhusika kisaikolojia. Watatumia zaidi ya dakika tano kumfundisha how to handle..
Nakuhakikishia, hata ungemkuta binti kwa wakati huo, ukamuambia unatapeliwa hawezi kukuelewa abadani.
Ukiona hivyo mnyang'anye simu. Maana usipomnyang'anya atampigia tena baadae na kumjaza maneno kibao na hela atatuma tu.
Nina kisa kama hicho kwa Sister wa Kikatoliki. Nafika kwa Wakala (jirani yangu) kupata huduma namuona naye kaja kutuma fedha na vazi lake la kitawa. Lakini, naona anapokea maelekezo kutoka kwingineko.
Wakala akamuomba hela, hakuwa nayo. Akasogea pembeni akamuambia hana. Tukasemezana na wakala kuwa anatapeliwa. Nikamsogelea na kumuambia, sister unatapeliwa huyo achana naye. Wala hata hakunisikiliza. Akawa anaondoka kwa upesi, sikukata tamaa. Namfata kutaka kumuelewesha, anapiga hatua kama za mtu anayenunua plot. Anatanua mpaka misuli inauma. Nikakumbia nikamkamata mkono, sister nakuomba nisikilize, akanitoa mkono kwa nguvu na kuondoka.
Akawahi hostel kuchukua kadi, akaja kutoa fedha akatuma Tsh 1,600,000. Nikamuambia Wakala tuma 160,000 tu.
Baada ya kutumiwa akaondoka.
Baadae anarudi analia. Hata kile kilemba hakimtoshi, kichwa kimekuwa kidogo. Sister alivua, amechanganyikiwa. Nilitamani nimuwambe makofi. Analia kaka yangu nisaidie. Mimi namsaidiaje na hela imetumwa? Imeshaliwa?
Wakala akamrudishia kiasi kilichobaki. Ameshika adabu.