Matapeli waoneeni huruma Watanzania

polisi hawezi deal na kesi ya kipumbavu kama hizo zinazo zinazozalishwa na tamaa yako, utaulizwa tu, "kwanini umtumie pesa mtu ambaye humjui ?" hapo polisi kamaliza
Hizi za kipumbavu ndizo uwapa maisha, police wanapoingia gharama kumsaka mwizi wako,mwizi akishadakwa yeye ndie urejesha gharama zote na kuwatoa maisha police na aliyeibiwa.
Ukiibiwa dili na mwizi mkamate aliyenunua vitu.
Kuna mtu aliuziwa simu ya wizi kwa laki 2 akaja kutoa milioni 5 Ili kuimaliza kesi.Gharama iliyotumika kumpata ni laki saba SAsa nani hapa kapata faida nani kapata hasara.
KWA milioni 5 huyo mnunuzi angepata simu ngapi.
 
Ulitumia sana ustaarabu kwa huyo sister mkuu, God bless you!
 
Hivi wenzetu mnatapeliwa vipi?
Yaani mi mwenyewe najiuliza?
Au kuna uchawi wa kwenye Simu?
.Mimi hao wajinga wakinipigia wakianza swaga zao tu najua ni tapeli naanza kuwazingua hadi wanashtukia wanaishia kunitukana.
Kuna mmoja nilimchanganya zaidi ya DK 5 alikuwa ananielekeza jinsi ya kutumia hela kutoka kwenye Simu yangu, weka nyota,sijui weka namba yako ya siri, basi mi najifanya natoa ushirikiano kumbe na msanifu najifanya nimekosea alipokuja kushtuka namzingua alitukana karibia DK nzima .
Nilimsanifu sana Yule tapeli alikuwa anajua kashapata mshamba anaenda kumpiga
 
Ipo milioni 3 ya haraka mwenye kuweza kunikamatia huyo tapeli anichek private.
Nataka nionane nae live nimuonyeshe yeye ni boya tu ujanja wa kishamba. Nimetangaza dau popote alipo TANZANIA tutafika.
Ipo milioni 3 ya haraka mwenye kuweza kunikamatia huyo tapeli anichek private.
Nataka nionane nae live nimuonyeshe yeye ni boya tu ujanja wa kishamba. Nimetangaza dau popote alipo TANZANIA tutafika.
Mkuu, hebu tulia.

Laki moja na hamsini isikuingize hasara ya Million 3. Hasira zisikuongoze.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]ungemlamba makofi hata mawili ya kumtoa wenge
 
Changamoto kwa mamlaka husika police, mamlaka ya mawasiliano, kampuni za simu na vyombo vingine ni watz wangapi wanatapeliwa kupitia njia
Yaani tena huu mtandao wa airtel sijui wanashida gani? Sijui ni hao maIT baadhi hawako makini au wanashirikiana nao katika hili.
Kisa kama icho kimemkuta mamaangu mdogo pia ila yeye alikua anatuma pesa (walisha ongea nae kitapeli huko na kumwambia atume pesa)na ile message ya kutuma muamala (kwamba umefanikiwa kutuma kiasi fulani)ikaingia na inaonekana kabisa kuwa ametuma pesa.
Kumpigia huyo tapeli ili kumwambia kuwa ameshatuma pesa anaskia jamaa anacheka tuu saana, ndo kushtuka na kutuambia sisi😂😂
Mwisho wa siku sasa kuja kufatilia sijui kujaribu kurudisha muamala sijui kuwapigia cm huduma kwa wateja ili wafatilie,io kampun ikasema hakuna muamala wowote uliotumwa kutoka katika hii namba.Tulibaki tunashangaa..
ila tulivokuja kuangalia kwa umakini kwenye ile message ya muamala kulinganisha na message nyingine za kutuma pesa kulikua na utofauti kidogo sana yan kwenye zile herufi za chini huwa wanaweka MP sijui PP alafu namba , ila kwake ilikua ni DD😂😂basi tukajua ameshatapeliwa.
 
Kama wanaweza ingilia mawasiliano ya kampuni za simu si hatari
 
Shida mifumo yetu bado sana.

Tapeli wa Aina hii anaweza kujipanga kwa kua na laini nyingi. Anacho fanya ni kuzitenga lain za kutapeli na hizo za kitapel anafanyia mawasilino feki tu hata simu ikipugwa anajua ni mtu Aliye nje ya mfumo wake. Yaan ni Askari au mteja wake kwa mujibu wa Maelezo ya tapeli.

Akitumiwa pesa anahamisha kwenye laini inayo soma majina tofauti na yake na hua haikai hewani kikubwa anahakiki pesa imehama.

Anapanda isafiri anaenda mkoa wa mbali ambapo nauli ni sh 10000 nenda Rudi sh 20000 anatoa pesa kwa wakala Aliye nje ya mkoa wake Kisha anarudi.

Kama katapeli 500,000 katumia nauli 20000 Kisha pamoja na ya makato 8000 inayo baki anahesabu faida.

Tatizo la hawa wanao tumwa kwa MAWAKALA ni wajinga wanawaamini hao matapel Sana.

Mm ni wakala Nina Visa viwili vya wateja wa Aina hii kuja ofisini kutaka kunitapel lakini wote hawakufanikiwa.

Mmoja ni mdada kaja anajiaminisha anayo pesa anataka kutuma laki 300,000 nikamuomba pesa akasema pesa anayo mkononi mm nitume tu, nikamwambia unataka nikutumie pesa wakati pesa unayo taka niitume umeishikilia hutaki kunipa unataka pesa ninayo tuma nitume ipi wakati unayo itaka niitume hutaki kunipa.


Baadae akaondoka akarudi nitumie tu mm nakupa, nikajua kua ni tapeli huyu nikadeshi kutuma nikamtajia jina nikamwambia tayari nipe pesa yangu. Akamuuliza yule Aliye kua akiongea nae lijamaa likasema halijaona pesa. Mm nikakaza nimesha tuma pesa hivyo nqitaka pesa yangu.

Nikamvuta yule dada ndani ya ofisini akaanza kuchezea kichapo watu wakajaa wakataka nimtoe wamgongeshe au wamchome Moto nikakataa kumtoa, wakati huo anavuja dam maana nilimpgia kaubao kana msumali ulimchoma mkononi.

Baadae maaskari wakaja kumchukua na mm mpaka kituoni ndugu wa binti wakaniomba tukayaongee nyumbani kwa bahati nzuri kwao binti ni maskiniiiiii wa kutupwa skulifahamu kabla, tulipo Rudi nyumbani wakanambia watanilipa pesa kwa awamu ila baadae nilimwambia yule mama kua nimesamehe akajua nimesamehe kweli pesa niliyo tuma kumbe nimesamehe hewa.

Ila binti nilimwambia aache smu yake ndogo mpaka leo ninayo na skutaka kumpa hapa nilimkazia maana ningekua mjinga angenisababishia hasara ya 300,000

Kisa cha pili ni dogo mmoja alikuja kutuma 90000 kwa maelekezo kutoka kwenye smu.

Yeye Nate nimeshikiria visimu vyake viwili mpaka ete 90000 yangu ambayo nilimwambia tayari nimeituma na hakua na pesa.

Ila mpaka Sasa sjamuona tangu mwezi wa 12

Shida ya hawa wanaotumiwa kifanya utapeli ni wabishi mm nawakomesha kwa Aina hiyo.

Kingine biashara ya HUDUMA za kifedha Zina changamoto ukisema ufuate utaratibu wa HUDUMA hizi nikweli huwezi poteza pesa ila utakosa wateja.

Hivyo kwa wateja wabishi kutoa pesa kabla ya muamala hua nafanya process zote za utumaji Kisha si ruhusu pesa kwenda ila namtajia tu jina na kumwambia tayari akinipa pesa naihakiki Kisha nairuhusu pesa kwenda.
 
Hakuna uchawi wanakamatwa ufahamu kama ambavyo waganga, mitume na manabii wa uongo wanavyowakamata watu.
Eti unaambiwa usiseme nawe mbio bubu bubu unaulizwa unakimbia Ili wasikuharibie bahati ishaingia milioni unawaza shida zote za Dunia umezimaliza.
SAsa hawa mabinti hio milioni moja uipata baada ya miaka miwili au zaidi .ndicho huwazuzua kumbe ni milioni hewa.
 
Ivi kwanini wakitumiwa izo pesa hewa wasifanye kama wanatoa pesa kuhakiki kama ni kweli katumiwa, alafu ndio sasa amtumie kutoka kwenye pesa aliyotoa🤔
 
Agiza Bear mkuu hapo kwa mangi.
 
utapeli wa aina hii umeota mizizi mtaani ni janga kubwa mnoo na ni mara chache sana kuskia matapeli wa aina hii kukamatwa na kuchkuliwa hatua za kisheria.

Miamala ya kutumiwa na kutoa chap chap au kutuma kwa mtu mwingne ndan ya dakika 1 tu ndicho wanachojivunia hawa matapeli

Ingekuwa laini za wateja haziruhusiwi kupokea pesa na kuituma au kuitoa ndan ya dakika 1
Yaani pesa ikishaingia kwa mteja ikae angalau dakika 5 ndipo aweze kufanya muamala wa kuitoa au kuituma.
Nafikiri kwa njia hii tungeweza kuzuia miamala mingi ya kitapeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…