Matapeli waoneeni huruma Watanzania

Hakika mkuu umenena Vyema
 
Kama kuna namba wanazohamishia pesa dakika moja baada ya kupokea pesa Ili ziwe nyingi wakatoe maeneo ya mbali, ni rahisi kuwapata, ile laini yenye pesa ambayo wanajua uhifahamu kampuni za simu zinaijua ni kuziblock. Kisha tapeli atapiga simu kampuni husika ataombwa taarifa zake, kisha ataambiwa aende ofisi ya karibu ya kampuni husika Ili kufuatilia suala lake kwann laini yake imefungiwa, sababu Ina pesa ataenda akifika tu kule anadakwa.
 
ungempata mtu wa mtandao husika yan mhudumu wa mtandao wa hizo namba mshikishe chochote atrack hizo namba mtapata tu pa kuanzia
 
..."Anapiga hatua kama mtu anayenunua plot"... 😆😆😆😆!Nimecheka kifala sana waalah.
 
Mimi nitoe ushauri wa bure
Biashara ya fedha za mtandao, ni Biashara inayohitaji ujuzi au uelewa wa kutosha juu ya masuala ya kifedha kama vile cashier wa Bank (mtoa pesa wa Benki)
Sasa mtu anatoa dada kijijini anampa mafunzo ya wiki moja tena ya kuunga unga halafu anamuachia aendeshe Benk unategemea nini?
ukifuatilia wizi wa kitapeli kwenye vituo vingi unaona kabisa mengi ya matukio yanaonesha aliyetapeliwa hakuwa na uelewa wa kutosha juu ya masuala ya kifedha. Tuanze kwa kuboresha hiyo idara ya nani akae dukani ili tusiendelee kupata hasara na kubakia kuwalaumu watu ambao hawana ujuzi......
 
Aisee
 
Kuna rafiki yangu alimkomesha tapeli wa mtindo huu kistaa Sana. Alimdanganya kwamba kashafika Kwa wakala lakini network inasumbua Sana!

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
Alifanyaje?

Hata hivyo tapeli kujiexpose ni vigumu sana, ni sawa na Ibilisi Shetani kuvaa sura ya mtu na kujidhihirisha hadharani!
 
Ipo milioni 3 ya haraka mwenye kuweza kunikamatia huyo tapeli anichek private.
Nataka nionane nae live nimuonyeshe yeye ni boya tu ujanja wa kishamba. Nimetangaza dau popote alipo TANZANIA tutafika.
Tatizo dhana na uhalisia mara nyingi hutofautiana!
Waweza kamatiwa huyo tapeli na ukija kumuona, hata ile muhu ya kumchapa inakupotea!
 
polisi hawezi deal na kesi ya kipumbavu kama hizo zinazo zinazozalishwa na tamaa yako, utaulizwa tu, "kwanini umtumie pesa mtu ambaye humjui ?" hapo polisi kamaliza
"Kuuzia kesi Polisi" anamaanisha Polisi wadili naye kwa manufaa yao.
 
Alifanyaje?

Hata hivyo tapeli kujiexpose ni vigumu sana, ni sawa na Ibilisi Shetani kuvaa sura ya mtu na kujidhihirisha hadharani!
Wahalifu wote uamini wao ni smart kuliko wengine thus uishia 18 za watu.
Hakuna uhalifu usioacha alama ya kukamatwa.
Hakuna muhalifu asiye mzinzi mlevi au mvutaji kimoja wapo lazima umnase
 
Ivi kwanini wakitumiwa izo pesa hewa wasifanye kama wanatoa pesa kuhakiki kama ni kweli katumiwa, alafu ndio sasa amtumie kutoka kwenye pesa aliyotoa[emoji848]
Staili hiyo unatapeliwa kirahisi mno.

Tapeli anaweza kukutumia pesa na akaiblock muda huo huo.

Utakapouliza salio figures zitaonekana pesa ipo lakini utapotaka kuitoa hauwezi utaambiwa "salio lako halitoshelezi" na baada ya masaa72 tarakimu hizo hupotea na kurudi kawaida.

Kama itakuwa una kiwango cha kutosha kwenye simu waweza kuhadaika baada ya kujiridhisha kuangalia salio na ukatuma kwa tapeli kumbe hela uliyotumiwa haipo.

Sijui kama nimeeleweka vizuri.
 
Safi.
Ama wangeliweka masharti kuwa pesa inapoingia kwenye akaunti husika haiwezi kutoka kwa withdraw ama kutumwa namba nyingine hadi ipite saa moja nzima.
Hapo matapeli wangeliishiwa pozi.
 
Ivi kwanini wakitumiwa izo pesa hewa wasifanye kama wanatoa pesa kuhakiki kama ni kweli katumiwa, alafu ndio sasa amtumie kutoka kwenye pesa aliyotoa[emoji848]
Ukitaka kuhakiki unaenda kwa wakala kabisa kutoa, kung'uta zote ndiyo utaupata ukweli.

Vinginevyo ukiishia kuangalia salio ama kujifanya unatoa na kujiridhisha kuona kiwango kilichoongezeka, hatua hiyo haikusaidii kuzuia kutapeliwa.

Acha msg hizo hewa za miamala zilizozoeleka, tapeli anaweza kuingiza cash kwako kweli na kisha kuiblock kwa mantiki ya kukosea kutuma.

Wewe utapoangalia salio, utakuta "kivuli" cha hiyo pesa kipo na utasadiki kumbe fedha hapo kiuhalisia haipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…