Matapeli wenitapeli lak 1 niliagiza maharage ya njano kilo 50

Matapeli wenitapeli lak 1 niliagiza maharage ya njano kilo 50

na maanisha anatumia jina gani hapa jamiiforum?
Jamii forum sijui jina analotumia ,,,ila Facebook alienitapel anatumia jina la ramsek na biashara
 
Attachments

  • Screenshot_20231205-161050.png
    Screenshot_20231205-161050.png
    394 KB · Views: 17
Nilitoa tangazo la kuhitaji maharage ya njano jamii forum na nikaweka namba yangu
Kumbe hujatapeliwa kupitia jamiiforum?
Ni vizuri kuutaadharisha uma kuwa huyo jamaa huko facebook ni utapeli, nakushauri m-ripoti polisi.
 
Nimetapeliwa laki 1 ,nilitoa tangazo nahitaji maharage ya njano , mwenye namba hii 0789242824 ajanitumia meseji inbox akanambia anamjua anayeuza maharage ya njano yupo kyela ,mbeya na akanipa namba yake ,akanambia ni muaminifu na niwe na amani ntapata maharage ya njano, akanitumia namba za anayueza maharage 0659158964

Nikawasiliana na anayeuza maharage (0659158964) Kwa njia ya meseji (sms) ,akanambia anauza maharage ya njano kilo 2000 ,nikamwambia nataka kilo 50 ,nikamtumia laki moja kwenye namba yake , baada kumtumia akanambia maharage yatafika kesho ,kesho ikafika akanambia mzigo wanashusha Moro , kesho yake Tena namtafututa na kumpigia simu hapokei inaita tu na Wala meseji hajibu mpaka sasa hajibu sms Wala nikimpigia hapokei

Facebook anatumia jina la ramsek na biashara
Namba anayotumia ni 0659158964
Kanitapeli pesa yangu ya mtaji wa biashara
Aisee pole sana. Wakati mwingine usikubali kufanya biashara na mtu usiye mfahamu, na pia asiye na rekodi ya uaminifu. Hapo kubali tu umepigwa.
 
Tuna changamoto ya uaminifu watanzania.

Linda pesa yako
Tunza pesa yako
Haswa biashara za mitandao

Zimedumazwa kwa kiasi kikubwa na matapeli.

Biashara zingekua nyingi sana kama utapeli ungedhibitiwa.

Watu wengi wanaogopa biashara za mitandao.

Binafsi nimeshanunua vitu vingi sana mitandaoni nje na ndani ya Tanzania,

Kutapeliwa kama kutapeliwa sijawahi, ila imeshatokea kuletewa bidhaa nisiyoitaka, mfano uagize mafuta ya taa uletewe diesel.

Ila huwa nakua makini kuangalia na kufatilia taarifa za muuzaji, cah kwanza naangalia kama anayo ofisi,

cha pili tukisha kubaliana kila kitu kuhusu bei namwambia ntakupa namba ya mtu atakuja kuchukua mzigo hapo ulipo, mara nyingi matapeli hawapendi hizi habari, wanataka kutumiwa pesa chap.

Kingine MUHIMU ZAIDI wabongo wengi wanapeda bei za chini na asilimia kubwa ya wanaotapeliwa na kuvutwa na bei zisizo na uhalisia, kitu cha milion 2 kipya unaambiwa kinauzwa lakin 4, kwa tamaa zako za mambo rahisi unatuma pesa na kutapeliwa, kwa tujifunze kujua vitu na thamani yake, chunguza bei mara mbili mbili, huwa nawaambia watu wengi sana hata wanaoagiza mizigo alibaba bei zisiwapumbaze, ukihadaika na bei kuna asilimia kubwa ya kukumbwa na haya mawili upate mali mbovu au utapeliwe.

Kwa hivyo hitimisho langu

Kwa biashara za mitandao ni hit or miss

Na kwa wale wafanyabiashara kupitia mitandao najua matapeli wanaharibu soko lenu kwa kiasi kikubwa kwa maana watu wengi wanaona biashara za mitandaoni utapeli ni mwingi.

Zingatia haya kwa mfanya biashara wa mitandao.

Kuwa na ofisi rasmi iliyosajiliwa na mamlaka husika, TRA, nk
Kuwa na lipa namba za mitandao yote, kuna baadhi ya wateja hutumia hii njia kujidhihirisha kama kweli wewe ni biashara halali au chenga.
 
Mkuu ww ni me au ke mbona unadanganywa kama mwanamke mwenye nyege unaitikia tu kama zoba vipi asee..... Jitafakari sana na kuja huku kulia lia kwa mtaji wa laki alooo unasafari ndefu sana..... Pole
 
Nadhani humu Kuna miongozo ya kufuata kabla ya kufanya biashara na mtu.Dah nakusikitikia rahisi ghali,pole kwa kutapeliwa Nadhani umejifunza kutokutuma pesa kwa mtu usiyewahi kumuona wala kumfahamu.Online business Tanzania bado saana.
 
Unapigwa vipi wakati mtu kaweka namba yake ya simu,nenda Police waeleze kama ulivyoelezea humu,watakusaidia tu sababu namba ya simu ni sawa na Kitambulisho.
Umeshauri vema sana kiongozi. Wengine wanamshambulia vikali sana. Nadhani yatupasa tuelelewe kuwa kwenye mitandao biashara zinafanyika Kwa uaminifu zaidi zaidi. Ilitokea mtu ametapeliwa ni utapeli kama utapeli mwingine.. siyo dhambi kufanya biashara Kwa Imani na Kwa uaminifu.
 
Nimetapeliwa laki 1 ,nilitoa tangazo nahitaji maharage ya njano , mwenye namba hii 0789242824 ajanitumia meseji inbox akanambia anamjua anayeuza maharage ya njano yupo kyela ,mbeya na akanipa namba yake ,akanambia ni muaminifu na niwe na amani ntapata maharage ya njano, akanitumia namba za anayueza maharage 0659158964

Nikawasiliana na anayeuza maharage (0659158964) Kwa njia ya meseji (sms) ,akanambia anauza maharage ya njano kilo 2000 ,nikamwambia nataka kilo 50 ,nikamtumia laki moja kwenye namba yake , baada kumtumia akanambia maharage yatafika kesho ,kesho ikafika akanambia mzigo wanashusha Moro , kesho yake Tena namtafututa na kumpigia simu hapokei inaita tu na Wala meseji hajibu mpaka sasa hajibu sms Wala nikimpigia hapokei

Facebook anatumia jina la ramsek na biashara
Namba anayotumia ni 0659158964
Kanitapeli pesa yangu ya mtaji wa biashara

View attachment 2835835View attachment 2835837View attachment 2835842
Pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana, next time utakuwa makini, fanya malipo ukipata bidhaa kwa kuikagua vizuri ndio ulipe.
 
Biashara za mitandaoni mimi ni mgumu sana kushawishika. Nina option moj tuu. Mhusika alete mzigo au asafirishe, nalipa on delivery. Nakuja stend kupokea mzigo nalipa. nje ya hapo tusameheane
 
Back
Top Bottom