Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Huwa inasikitisha sana na inauma sana kukata tamaa ingawa inatokea kwa wengi.Kuna wakati tunazokutana na matatizo kiasi cha kutufanya kuamini maisha yetu ndiyo hayo matatizo "so sad news".
Leo sihitaji kukuta moyo ila natamani sana kukujulisha nilichojifunza katika miaka yangu hii machache hapa Duniani.
Matatizo na changamoto ni sawa na mtu anayefanya mazoezi ya bingo mfano mazoezi ya kuinua vitu vizito "mfano Barbell workouts". Hii inakuwa hivi "kadiri unavyiinua vitu vizito na kuhisi maumivu ya misuli ndivyo misuli yako inavyoimarika na kadiri unavyoendelea zaidi unazidi kuwa bora mara dufu ila ukiacha ni kwa hasara yako.
Katika maisha yetu ya kawaida matatizo bila kujali ni makubwa au ni madogo kiasi gani ni sehemu ya mazoezi ili kuimarisha maisha yetu na siyo maisha yenyewe "maisha yanaendelea".
Unapoanguka simama angalia mbele achana na nilipotoka kwa sababu umeshafika na unaendelea mbele " keep going rafiki acha kulaumu wengine na kulalamika ubaya wa wengine inakua futa vumbi lililokuchafua,futa machozi ya maumivu yako usisubiri kufutwa endelea na safari yako.
Kumbuka kila mmoja wanakwenda mbele kwa namna yake usijali wenzako wanakwenda kwa namna ipi wewe jihakikishie unakwenda mbele hata kama unatambaa na kujiburuza wakati wengine wanatembea kwa miguu yao na wengine kwa kutumia vyombo vingine "move forward".
Unachoweza kukitawala ni kilichopo mbele yako kwa sababu ukiangalia nyuma tayari kilishatokea kilivyotokea, ukiangalia sasa ndicho unachofanya kilichobaki ni ambacho kipo mbele yako, tengeneza mazingira ya kukitawala ili kikitokea kisikutawale wewe.
Keep going Brethren.