Benitho Richard
Member
- Aug 30, 2022
- 5
- 3
Kuna watu ambao walipitia shida nyingi sana enzi za utotoni na ujanani mwao; kuanzia kula yao, kusoma kwao, kulala kwao, kuvaa kwao, nk kulikuwa ni kwa shida sana. Kiufupi tu ni kwamba walipitia maisha magumu sana. Watu hawa waliushinda umasikini kupitia elimu, biashara au shughuli nyingine na mwisho wa siku walitoboa. Wengi wao wanapokuja kuanzisha familia huwa wameathirika kisaikolojia na yale maisha ya zamani; hivyo huwa na sura moja kati ya hizi mbili;
1. Huwa hawatamani kabisa kuona na hata kuskia watoto wao wakipitia shida walizopitia wao. Ili wajiskie vizuri, huhakikisha kuwa familia zao ni paradiso muda wote kwa kuwapa watoto wao kila wanachotaka. Kwa bahati mbaya sasa, watoto wao hudhania kuwa duniani hakuna shida hivyo huishi maisha ya anasa na yenye kudekezwa sana sababu wazazi wapo na wanawapa kila wanachotaka.
Watoto wanafikisha umri wa miaka 18 hata hawajui maana ya magimbi, kunguni, chawa, fimbo, mbigili, ukurutu, kilaka, magaga, ukoko, moshi, kibuyu nk. Wanadhani hii ni misamiati ya waganga wa kienyeji. Watoto wanasoma shule za bei ghali zaidi ya tano ndani ya muda mfupi sana sababu ya kuhamishwa shule kila wakifanya utovu wa nidhamu shuleni; yaani kinidhamu hawako vizuri sababu ya kiburi cha pesa za wazazi. Wanahitimu chuo kikuu lakini hawataki ajira sababu hawakuandaliwa kujitegemea na wanahisi watapata tabu kuishi peke yao. Muda wote wapo na magari ya baba yao club au maeneo mengine ya kula bata.
2. Kuna wale wazazi ambao baada ya kutoboa tu kimaisha, familia zao hugeuka ni jeshi au jela. Watoto ni lazima wakimbie mchaka-mchaka asubuhi, wateke maji ndoo tano au kumi kila mmoja, wakamwagilie bustani, wakalishe mifugo na kisha waoge maji ya baridi ili waende shule baada ya kunywa chai na mihogo, magimbi au viazi vitamu.
Watoto wa familia hii hawajui maana ya chocolate, pizza, burger, school bus, pop corns, nk. Ukiwapa hii misamiati watadhania kuwa ni majina ya wacheza movie za kimarekani. Wazazi pesa wanazo lakini historia yao imewaathiri sana. Wazazi wa familia ya namna hii hutaka watoto wao wajue kujitegemea na waonje pia ugumu wa maisha kwa namna ambayo ina makosa kadhaa. Watoto kuchapwa fimbo ni jambo la kawaida kabisa, kutishiwa laana ni kama wimbo vile, kula viporo, ukoko au mlo mmoja kwa siku ni jambo la kawaida sana. Hakuna haja ya kuwa na stoo kwa sababu vyumba vya watoto vinaweza kutunza pia vifaa kama majembe, sululu, chepe, nyundo, mafagio na vilago.
•••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Naomba kuwakumbusha wazazi wapya na wale makonki. Dunia inabadilika kila siku. Wewe kama mzazi, tumia muda wako kuwapa elimu wanao kwa kuwafundisha maadili mema na uwape hofu ya Mungu. Wafundishe pia kazi mbalimbali za mikono pasipo kuwaumiza. ACHA KUWALEA WANAO KWA HISTORIA YAKO.
Suala la kusema kuwa ulitembea kilometa 20 wakati unasoma hivyo wanao watembee pia kutoka Temeke hadi Ilala sio sawa. Eti kwa kuwa ulishindia uji enzi hizo, ndio uwashindishe wanao na mlo mmoja sio sawa.
Na wewe mzazi uliepitia magumu enzi zako halafu unatuletea pigo za kizungu kwa wanao sio sawa. Afrika hata haijabadilika sana; mashangazi bado ni wakorofi, ndugu bado wanagombania mali, roho mbaya ipo palepale, ushirikina bado upo, fitna kama kawaida na Afrika huwa hatupendani kiviiile; mapenzi ni Ulaya hukoooo. Sasa we dekeza tu hao watoto, wataijua dunia ukifa. Kama kuzimu kuna TV basi utayaona mapito ya wanao ukifa. Waoneshe wanao pande zote mbili za dunia, hata siku umekufa wanajua wanaanzia wapi na sio wabaki wakikulilia mzazi kaburini kila wakipitia changamoto.

Upvote
0