Wamba de Wamba
Member
- Sep 2, 2013
- 16
- 2
Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Dr.Shukuru Kawambwa., Mheshimiwa Waziri, ofisi ya waziri mkuu Tamisemi anayeshughulikia elimu,Kassim Majaliwa., Mheshimiwa waziri wa wizara ya maendeleo, jinsia na watoto., Mheshimiwa waziri, ofisi ya Rais utawala bora.Kwa hakika, naamini fika kila niliyemtaja hapo, anatambua majukumu yake. Kutokana na matatizo makubwa yaliyopo katika shule hii na ambayo kila niliyemtaja hapo juu yanagusa wizara yake naomba niseme hivi, ebu jambo hili lichukulieni uzito kwa kila mmoja wenu kufika eneo tajwa kujionea matatizo yaliyopo. Wanakijiji, watoto na watumishi ndiyo wahanga wa matatizo katika shule hii. Taarifa za matatizo haya zilishafikishwa hata halmashauri lakini , inaonesha halmashauri kutokutilia maanani kutokana na kile kilichozoeleka yaani mambo ya kishikaji. Watanzania wenzangu, siko hapa kumuchafua mtu ila nasema kile nilichonacho uhakika kwa lengo la kusaidia hususani hawa watoto wetu waweze kupata elimu bora iliyojengwa katika maadili bora.Naamini ufatiaji juu ya kubaini matatizo haya utafanyika. Na mimi sipendi kushoboka kwa leo matatizo haya mpaka pale wenye dhamana ya kufuatilia watakaposhindwa nitayaleta hapa hapa hadharani na nitaomba wanaharakati wa haki za binadamu wanilinde.