Matatizo tumeishayapatia ufumbuz au na sisi ni sehemu ya matatizo?

Matatizo tumeishayapatia ufumbuz au na sisi ni sehemu ya matatizo?

SIKUTAKA KURUDI HAPA KWA SASA, lakini nimelazimika


Katika context (muktadha) wa Tanzania kwenye siasa na maendeleo vipo pamoja. Hivyo huwezi kusema kujengewa mazingira, hasa kwa kilimo you will need something. Mfano, endapo unahitaji mkopo say unawekeza kwenye samaki wa kufuga utahitaji ardhi, unless you got tittle dead au hata CCRO - customary certificate of right of occupancy. This is a process hasa kwa mtu mmoja mmoja. Serikali inapaswa kuwekeza kufanya upimaji wa ardhi - itoe certificate kwa vijiji viwe na land registry ndo viweze kutoa CCROs. Hili litamwezesha mtu kutumia ardhi kama collateral - hapa pia ina maana ni jukumu la serikali kuhakikishia mabenki kuwa ardhi hata ile ya vijijini inaweza kutumika kama collateral! Huu ndo uwezeshwaji wa serikali nilio-maanisha. Pia endapo mtu unafunga samaki utahitaji huduma za vyumba baridi/cold roooms! Hii haiwezekani kama hakuna umeme! Huu ni uwezeshaji pia wa serikali.

Kimsingi tunaongea kuleta mapinduzi ya kifikra kutoka kilimo cha kujikimu kuja kwenye kilimo cha biashara. Sasa graduate hata kama anaanza mwenyewe, ni lazima yawepo mazingira bora yanayohamasisha kuwekeza

Likewise mfanya biashara hana mkataba na mlimaji, lakini anaweza kushawishika kuingia biashara kama mazingira ni bora. Nijuavyo mimi kilimo cha mkataba sio mwarubaini -panacea ya matatizo ya soko na ubora wa mazao. Katika mfumo wa sasa zipo avenues nyingi sana za kufanya biashara, but sisi tumeendelea kuangalia njia moja! Wakati mwingine natamani niache kazi nijikite kabisa kwenye kilimo -mazao au mifuko (amid challenge ya upatikanaji wa maji na malisho).

La mwisho, kuna Enterpreneur (nadhani- sikumbuki nani humu) ameongea kuhusu export ban (sio bun). Jambo hapa muhimu kujua ni kwamba we are not totally against it, BUT should not be done by violating farmers and or traders' right! What do I mean here? Serikali iki-impose ban iwe tayari kununua kwa bei ya soko tena pasipo usumbufu. FINITO! Wale ambao wanaimpose ban, lazima wanakuwa na mechanism za kuuza. Mkutano wa wiki hii hapa Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alilalamika SANA kuhusu unsold consignment ya mahindi - over 600 tonnes!Waziri akakataa kuwa kiasi hicho hakipo. Alipoulizwa mtu wa Grain reserve hakuwa na takwimu! Sasa ban zinazoenda bila enough data unategemea nini
Mchana mwema


MKUU UNAUHAKIKA KUNA MKULIMA ANAYE TAKA KUUZA MAHINDI KENYA? NIJUAVYO MIMI HAKUNA HATA MKULIMA MMOJA ANAYE FANYA HIVYO WAO WANABAKIA KUONA MAGARI YAKO MIPAKANI TU

- Hii biashara ya kuuza mahindI KENYA inafanywa na wafanya biashara walanguzi ambao wao huenda kununua kwa wakulima kwa bei ya chini na wao ndo wanaenda kufaidika huko kenya

-NA HATA WAZIRI ALISHA WAHI ONGELEA HILI KWAMBA HAKUNA MKULIMA ANAYE PELEKA MAHINDI KENYA BALI NI WAFANYA BIASHARA WAJANJA WAJANJA

-That is wahy nasema kungekuwa na Viwanda Vingi vya kusindika mahindi je yangeozea huko RUKWA? Viwanda viulivyopo havina uwezo wa kusindika mahindi yote make kwanza viko vichache sana

2. KILIMO CHA MKATABA
Mkuu kilimo cha mkataba ndo solution, huku ARUSHA KUNA WAKULIMA WAZUNGU WANALIMA KAHAWA NA WANAUZA USWIZI NA WANA CONTRACT MKUU

- Kuna wanao lima maharage na wana soko kabisa linalo fahamika kisheria,

- Mkuu hebu fikilia mwaka huu unalima mahindi, maharage,nyanya, unafuga kuku na kazalika, na huna sehemu ya kuuza ila unaamini tu ukisha lima utayauza na hata huko RUKWA kunasababisha na vitu kama hivi,

- Kwa wakulima wakubwa hakuna anaye weza kulima bila kujua ana muuzia nani, kilimo ni kama kiwanda na hoteli, wewe huwezi anzisha kiwanda au hoteli bila kujua unamuuzia nani chakula ila unaamini kwamba hapa watu watakuja tu
 
1. intaprinua mwanzoni nilifikiri kuanzisha kitu kama gazeti la kilimo kunaweza kusilete faida kumbe kuna wadau kama viwanda vya mbolea, zana za kilimo, wazalisha mbegu, wanunuzi wa mazao, watengeneza dawa za magugu na wadudu na wanunua magazeti pia wote hao wanaweza customers kwa matangazo yao, thanx kwa kunifungua macho.
2. kuhusu swala la ushirika, naona kwenye hivi vyama hakukuwa na equal patnership na mabosi walikua wanafaidika kweli na kuwa matajiri, sasa mkiungana ni tofauti mnajadiliana na kuchagua common course of action na kuepusha malalamishi kama ya huko NICOL sababu kila mtu anajua kinachoendelea mkiona mnapata hasara mnachange course.
3.halafu huwa nafikiria hivi ukitaka kufanya kilimo cha umwagiliaji hauwezi ukatumia wind mills kuvuta maji?
THIS THREAD IS VERY USEFUL!
 
1. intaprinua mwanzoni nilifikiri kuanzisha kitu kama gazeti la kilimo kunaweza kusilete faida kumbe kuna wadau kama viwanda vya mbolea, zana za kilimo, wazalisha mbegu, wanunuzi wa mazao, watengeneza dawa za magugu na wadudu na wanunua magazeti pia wote hao wanaweza customers kwa matangazo yao, thanx kwa kunifungua macho.
2. kuhusu swala la ushirika, naona kwenye hivi vyama hakukuwa na equal patnership na mabosi walikua wanafaidika kweli na kuwa matajiri, sasa mkiungana ni tofauti mnajadiliana na kuchagua common course of action na kuepusha malalamishi kama ya huko NICOL sababu kila mtu anajua kinachoendelea mkiona mnapata hasara mnachange course.
3.halafu huwa nafikiria hivi ukitaka kufanya kilimo cha umwagiliaji hauwezi ukatumia wind mills kuvuta maji?
THIS THREAD IS VERY USEFUL!
Mkuu una mawazo mazuri sana, sasa ni kwa nini hauchukui hatua? Hapo kwenye RED umenifurahisha sana, kwani suala hili linawezekana na kuna thread moja inayosema Tuwathamini, Tuwaendeleze. One individual can make a Difference
na kuna clip inayomuelezea kijana aliyeweza kukisaidia kijiji chake huko malawi kwa teknolojia hii.

Keep it up
 
Mkuu makampuni ya ununuzi ndo moja ya watu wanao didimiza kilimo huku Tanzania na ndo maana nasema ni lazima tuje na mbinu mbadala za kuweza kumaliza hili Tatizo, hatuwezi endelea kuwategemea wanunuzi ambao wanakuja na bei zao.
...Sasa, katika soko huru linaloendeshwa na nguvu ya soko, nani atanunua hayo mazao?. Je, serikali?

...Unajua, kuna njia nyingi za kupata soko au kuuza hilo zao. Kwanza, kwa wakulima kuwa na umoja kama NGO au Kampuni [hata chama cha ushirika, wenye hisa nacho] na kutafuta masoko wao wenyewe, nje na ndani ya nchi. Pili, kwa wakulima kuongeza thamani katika hilo zao na kuuza moja kwa moja kwa wateja [suppliers, supermarkets, food companies, etc] ndani na nje ya nchi.
Vyama vya ushirika ndo vinaongoza kwa kudidimiza kilimo na bado si suluhisho kabisa kwani ndo wameua kilimo na hatuwezi endelea kutegemea vyama vya ushirika, make viko kisiasa sana, na wakati wake ulisha pita.
...Huu ndio wakati wa ku review utendaji wa hivi vyama na kuangalia namna ya kusaidia wakulima kuviboresha. Wakulima wanahitajika kuvimikili, as in share holding. Bila hivyo, hakutakuwa na maendeleo yeyote katika kilimo, and this is fact. Unafahamu kwamba, katika baadhi ya nchi katika shirikisho la Ujerumani [FRG] kuna vyama very strong vya wakulima na wafugaji?. Unafahamu mafanikio nyuma ya Tanga Fresh?.
 
3.kuhusu masoko naona ndani soko ni dogo sana ukilinganisha na potential tuliyonayo kwenye sekta ya kilimo, hapa tatizo wapanga sera, tukianza na kilimo cha mazao ya chakula, serikali imeweka vikwazo ku export haya mazao hivyo wakulima kuuza ndani kwa bei ndogo kitu ambacho kinawakatisha tamaa watu kulima hasa wale wenye mitaji mikubwa kwa mtindo huo uzalishaji wa chakula unapungua na badala ya kuzuia njaa tutajikuta tunaleta njaa, cha kufanyika ni kumuacha mkulima auze atakako hilo linaweza kumuongezea kipato hata akaweza kusindika, wengi watavutiwa kulima, pia wawekezaji wa ndani watavutika kufungua viwanda vya kusindika kwa sababu ya upana wa soko jamaa wanasema tuwe bread basket but they dont mean it
...Thanks, for this piece.

...Nafarijika nikikutana na wale tunaofikiria katika mwelekeo mmoja. Naamini, tutafika kwenye nchi yenye maendeleo ya kweli, siku moja. Haitakuwa kesho. Inaweza kuwa kesho kutwa au siku ya mbele yake. We've got a lot of work ahead, in laying the foundation.

...Back to the main issue. Kama ulivyokwisha elezea, hakuna incentives za watu kulima, zaidi ya kutafuta chakula na hela kidogo ya kubadilisha mboga. Ni mpaka pale kutakapokuwa na uhuru wa kweli wa soko katika mengi ya mazao ya wakulima wetu, na wao wenyewe kumiliki vyama vyao na mifumo ya uongezaji thamani, ndipo tutaona maendeleo ya kweli kwenye sekta hii.

...Hebu tujiulize. Je, kungekuwa na kilimo cha maana cha mboga kule Spain, kama wasingeweza kuuza kwa majirani zao [soko zima la EU], kisa wakiuza figiri au sukuma wiki zinapanda bei nyumbani? Lazima tufike sehemu tuache kuchezea soko as we wish. Labda tulichezee kwa uangalifu mkubwa, baada ya kupima athari zake na sio kutaka ku gain political mileage at the expense of peasants.
 
1. Hoja ya kuwa na Gazeti la Kilimo. Hii ni hoja nzuri lakin wewe unavyoizungumzia, ni kama ni wajibu wa serikali kufanya hivyo. Kwani private sector kama wewe na mimi hatuwezi kuichukua hii kama business Opportunity na kuifanyia kazi? Hasa ikizingatiwa kuwa Tayari Serikali imeshaonyea nia kubwa zaidi ya kuwa na Benki ya Kilimo
...Private sector pakee yenye uwezo wa kufanya hivi ilikuwa Tanganyika Farmers Association. Nadhani sasa i dhoofu bin hali. Hamna wakulima Tanzania! tuna peasants, who can not afford to publish a paper.

...Kama ulivyosema, hii si kazi ya serikali. Tatizo ni kuwa magazeti haya yako pale ambapo kilimo kimeendelea na ni cha kisasa kama South Africa. Hawa wana gazeti la wiki na website nzuri, ona Farmer's Weekly | Home
Lakini kabla sijaenda mbali zaidi, naomba niulize swali. Hivi model hii ya kuunganisha nguvu haikuwahi kutumika kipindi cha nyuma? (Rejea, Vyama vya ushirika). Je ni kitu gani kiliua vyama hivi? Mbona tulikuwa na vyama vya ushirika vyenye nguvu na sasa vimekufa. Nauliza haya, ili watu wajue tulijikwa wapi na kuchukua hatua muafaka kwani bila ya hivyo hata hizi juhudi tulizonazo za kuanzisha SACCOS zitapotelea gizani kwa kiwango kikubwa
...Vyama vya ushirika kabla ya uhuru vilimilikiwa na wakulima. Baada ya uhuru vika binafsishwa na serikali -ikiwa, pamoja na sababu nyingine, kuhamisha faida katika sekta hiyo na kujengea viwanda na miradi mingine ya kitaifa, ya maendeleo- na kuwekwa chini ya watawala wasio na maslahi ya moja kwa moja katika kilimo. And they failed, just, because of this.

...Kitu cha pekee kitakachofanya SACCOS au VICOBA ziendelee ni transparency na strict codes of conduct. Halafu, lazima ziwe community owned.
 
Hivyo basi, kuendeleza kilimo ni kuondoa umasikini na uhaba wa chakula ni kufikia malengo ya mkukuta na milenia.
...Hii kitu ndio ya hovyo kabisa. Inajali zaidi namba na si ubora wa hizo namba. Mfano, ripoti ya elimu itasema imetekeleza kwa kiasi fulani lengo la milenia katika kuandikisha watoto shule. Swali, Je, watoto hao wanajua kusoma na kuandika? angalau jina lao? Je, shule wanazosoma zina viwango stahiki?. Hivi majuzi waziri mdogo wa TAMISEMI aling'aka juu ya ubora mbaya kabisa wa maabara -kama sijakosea- katika moja ya shule huko Chato au maeneo hayo.

...Tukirudi kwenye sekta husika. Hivi lile josho lililojengwa kule Chato, limemnufaisha mfugaji?. Ila, litaingia kwenye takwimu za milenia! Hii kitu ya MDGs ni scam. We are being made poorer. Tutaona hii vizuri zaidi after some years.
Sasa endapo wakulima wangejipanga vizuri, bila shaka wangedai fidia.
...Wajipange vizuri kwa kuchagua viongozi watendaji, kwanza. Kama hawataweza hilo, hii itakuwa nyimbo maarufu.
Mimi ni mkulima wa nanasi na machungwa. Wakati wa msimu huwa nauzia shambani au naleta mjini. Bei ni tofauti. Lakini najiuliza kama Azam angenipa mkopo wa kuzalisha nanasi/machungwa tani kadhaa na kwa ubora kadhaa kwa wakati fulani, kisha serikali ikaniambia nisiuze mananasi hayo kwa Azam sijui inaweza kuwaje! Hii inaweza kusababisha mtu kujinyonga hivi hivi
...Kilimo cha nanasi na embe kinakuwa kwa kasi kwasababu hakiingiliwi. Soko ndilo linaamua, na kwasasa bado ni zuri.
Mwuliza Mh Mpya mwenyekiti wa bodi ya Korosho (Anna) hata yule aliyepita (Kitwana) bodi zimefanya nini kutafuta real markets badala ya kutegemea hawa wachuuzi/watu wa kati? Kwa nini viwanda 11 vya kubangua korosho vilivyo binafisishwa hadi leo zaidi ya nusu havifanyi kazi? Why can we add value to our korosho, create employment and secure the market? Kwa nini tulenge ulaya wakati tunajua hata tungelenga makampuni ya ndege za Afrika tungeuza korosho kiasi kizuri tuu?
...Nyingi ya hizi ni mzigo tu, hazina faida inayoonekana kwa mkulima. Zilikuwa na nafasi wakati wa command economy, not anymore.
Inatia uchungu. Nitarudi kesho kutwa!
...Rudi, tufaidike na michango yako!
 
...Bube, hicho kikao ni cha ndani au cha wadau wote?. Maana, usikute inabidi mjipange kama serikali, kabla hamjashirikisha watu binafsi kama wakulima, vyama vya ushirika, makampuni ya madawa na mbegu, wanunuzi wa mazao, n.k. ...Ni kweli kabisa, serikali pekee haiwezi kuleta maendeleo kwenye kilimo. Na hii yetu, imekuwa inarudisha nyuma maendeleo ya kilimo bila kujua, hasa pale inapoingilia nguvu na utaratibu wa soko, ili kufurahisha wakulima au walaji. ...Tunategemea walipofanya hivyo walikuwa na soko mbadala la korosho hizo. Kama hali si hiyo, basi ni kiama kwa wakulima huko. ...Haiwezi kujikosoa, kwani hakuna utaratibu huo Afrika. ...Na hapa ndipo serikali inabidi kushika hatamu, kwa kushirikiana na wadau.
Ijapo kuwa hii mada ni ya miaka kadhaa iliyopita naomba nitoe credit kwenu wakuu ... mkoo vizuri ama hakika Tanzania ina baadhi ya vijana wenye fikira madhubuti sana ... lakini mfumo kandamizi uliopo madarakani hautaki kuwapa nafasi vijana hao ili waweze kuzitumia skills zao vyema zitakazo weza kuivusha nchi hapa tulipo kwama
 
mkuu chasha umeongea kitu kizuri,ila naogopa hata kuchangia sababu mawazo yangu mengine ni ushauri kwa hii serikali kiziwi hivyo naweza kuonekana bado nalalamika anyway nianze hivi.
1. kuhusu elimu ya kilimo naona TBC huwa wanavipindi vya kilimo japo huwa na doubt kama wanamaanisha, pia nashangaa nchi ya wakulima haina gazeti linalo husu kilimo! ningeona waanzishe gazeti la kilimo walau once per week, information zilizoandikwa zinaeffect kuliko za tv na redio
2.kuhusu mitaji ya kilimo naona watu mnaweza mkajikusanya kwenye vikundi vya watu wenye mitaji kama watu 2,3,4, 10 hadi 100 na mkachanga labda laki tano na kuendelea na mkatafuta mradi ambao ni feasible kwa hela yenu cha muhimu muwe na sheria zinazoeleweka na watu wasiegemee sana kwenye mradi kama source ya mapato especially siku za mwanzo
3.kuhusu masoko naona ndani soko ni dogo sana ukilinganisha na potential tuliyonayo kwenye sekta ya kilimo, hapa tatizo wapanga sera, tukianza na kilimo cha mazao ya chakula, serikali imeweka vikwazo ku export haya mazao hivyo wakulima kuuza ndani kwa bei ndogo kitu ambacho kinawakatisha tamaa watu kulima hasa wale wenye mitaji mikubwa kwa mtindo huo uzalishaji wa chakula unapungua na badala ya kuzuia njaa tutajikuta tunaleta njaa, cha kufanyika ni kumuacha mkulima auze atakako hilo linaweza kumuongezea kipato hata akaweza kusindika, wengi watavutiwa kulima, pia wawekezaji wa ndani watavutika kufungua viwanda vya kusindika kwa sababu ya upana wa soko jamaa wanasema tuwe bread basket but they dont mean
NOTE: ku work hard kunahusisha kuthink hard, tukiwork hard tutawaajiri watu kama DAR si LAMU! jina lenyewe linaonyesha mtu mwenye mawazo hasi
Hahaa ..hiyo aya ya mwisho nimecheka sana ... mkuu uko vizuri sana " siku hizi hauitendei haki jf kabisa ...kwa kutokana na kushinda kwako kwenye Yale majukwaa ya yenye umbea umbea .. jamii yetu inahitaji mawazo kama haya ili iweze kujikwamua kwenye changamoto zinazo izunguka
 
Back
Top Bottom