Matatizo tumeishayapatia ufumbuz au na sisi ni sehemu ya matatizo?



MKUU UNAUHAKIKA KUNA MKULIMA ANAYE TAKA KUUZA MAHINDI KENYA? NIJUAVYO MIMI HAKUNA HATA MKULIMA MMOJA ANAYE FANYA HIVYO WAO WANABAKIA KUONA MAGARI YAKO MIPAKANI TU

- Hii biashara ya kuuza mahindI KENYA inafanywa na wafanya biashara walanguzi ambao wao huenda kununua kwa wakulima kwa bei ya chini na wao ndo wanaenda kufaidika huko kenya

-NA HATA WAZIRI ALISHA WAHI ONGELEA HILI KWAMBA HAKUNA MKULIMA ANAYE PELEKA MAHINDI KENYA BALI NI WAFANYA BIASHARA WAJANJA WAJANJA

-That is wahy nasema kungekuwa na Viwanda Vingi vya kusindika mahindi je yangeozea huko RUKWA? Viwanda viulivyopo havina uwezo wa kusindika mahindi yote make kwanza viko vichache sana

2. KILIMO CHA MKATABA
Mkuu kilimo cha mkataba ndo solution, huku ARUSHA KUNA WAKULIMA WAZUNGU WANALIMA KAHAWA NA WANAUZA USWIZI NA WANA CONTRACT MKUU

- Kuna wanao lima maharage na wana soko kabisa linalo fahamika kisheria,

- Mkuu hebu fikilia mwaka huu unalima mahindi, maharage,nyanya, unafuga kuku na kazalika, na huna sehemu ya kuuza ila unaamini tu ukisha lima utayauza na hata huko RUKWA kunasababisha na vitu kama hivi,

- Kwa wakulima wakubwa hakuna anaye weza kulima bila kujua ana muuzia nani, kilimo ni kama kiwanda na hoteli, wewe huwezi anzisha kiwanda au hoteli bila kujua unamuuzia nani chakula ila unaamini kwamba hapa watu watakuja tu
 
1. intaprinua mwanzoni nilifikiri kuanzisha kitu kama gazeti la kilimo kunaweza kusilete faida kumbe kuna wadau kama viwanda vya mbolea, zana za kilimo, wazalisha mbegu, wanunuzi wa mazao, watengeneza dawa za magugu na wadudu na wanunua magazeti pia wote hao wanaweza customers kwa matangazo yao, thanx kwa kunifungua macho.
2. kuhusu swala la ushirika, naona kwenye hivi vyama hakukuwa na equal patnership na mabosi walikua wanafaidika kweli na kuwa matajiri, sasa mkiungana ni tofauti mnajadiliana na kuchagua common course of action na kuepusha malalamishi kama ya huko NICOL sababu kila mtu anajua kinachoendelea mkiona mnapata hasara mnachange course.
3.halafu huwa nafikiria hivi ukitaka kufanya kilimo cha umwagiliaji hauwezi ukatumia wind mills kuvuta maji?
THIS THREAD IS VERY USEFUL!
 
Mkuu una mawazo mazuri sana, sasa ni kwa nini hauchukui hatua? Hapo kwenye RED umenifurahisha sana, kwani suala hili linawezekana na kuna thread moja inayosema Tuwathamini, Tuwaendeleze. One individual can make a Difference
na kuna clip inayomuelezea kijana aliyeweza kukisaidia kijiji chake huko malawi kwa teknolojia hii.

Keep it up
 
Mkuu makampuni ya ununuzi ndo moja ya watu wanao didimiza kilimo huku Tanzania na ndo maana nasema ni lazima tuje na mbinu mbadala za kuweza kumaliza hili Tatizo, hatuwezi endelea kuwategemea wanunuzi ambao wanakuja na bei zao.
...Sasa, katika soko huru linaloendeshwa na nguvu ya soko, nani atanunua hayo mazao?. Je, serikali?

...Unajua, kuna njia nyingi za kupata soko au kuuza hilo zao. Kwanza, kwa wakulima kuwa na umoja kama NGO au Kampuni [hata chama cha ushirika, wenye hisa nacho] na kutafuta masoko wao wenyewe, nje na ndani ya nchi. Pili, kwa wakulima kuongeza thamani katika hilo zao na kuuza moja kwa moja kwa wateja [suppliers, supermarkets, food companies, etc] ndani na nje ya nchi.
Vyama vya ushirika ndo vinaongoza kwa kudidimiza kilimo na bado si suluhisho kabisa kwani ndo wameua kilimo na hatuwezi endelea kutegemea vyama vya ushirika, make viko kisiasa sana, na wakati wake ulisha pita.
...Huu ndio wakati wa ku review utendaji wa hivi vyama na kuangalia namna ya kusaidia wakulima kuviboresha. Wakulima wanahitajika kuvimikili, as in share holding. Bila hivyo, hakutakuwa na maendeleo yeyote katika kilimo, and this is fact. Unafahamu kwamba, katika baadhi ya nchi katika shirikisho la Ujerumani [FRG] kuna vyama very strong vya wakulima na wafugaji?. Unafahamu mafanikio nyuma ya Tanga Fresh?.
 
...Thanks, for this piece.

...Nafarijika nikikutana na wale tunaofikiria katika mwelekeo mmoja. Naamini, tutafika kwenye nchi yenye maendeleo ya kweli, siku moja. Haitakuwa kesho. Inaweza kuwa kesho kutwa au siku ya mbele yake. We've got a lot of work ahead, in laying the foundation.

...Back to the main issue. Kama ulivyokwisha elezea, hakuna incentives za watu kulima, zaidi ya kutafuta chakula na hela kidogo ya kubadilisha mboga. Ni mpaka pale kutakapokuwa na uhuru wa kweli wa soko katika mengi ya mazao ya wakulima wetu, na wao wenyewe kumiliki vyama vyao na mifumo ya uongezaji thamani, ndipo tutaona maendeleo ya kweli kwenye sekta hii.

...Hebu tujiulize. Je, kungekuwa na kilimo cha maana cha mboga kule Spain, kama wasingeweza kuuza kwa majirani zao [soko zima la EU], kisa wakiuza figiri au sukuma wiki zinapanda bei nyumbani? Lazima tufike sehemu tuache kuchezea soko as we wish. Labda tulichezee kwa uangalifu mkubwa, baada ya kupima athari zake na sio kutaka ku gain political mileage at the expense of peasants.
 
...Private sector pakee yenye uwezo wa kufanya hivi ilikuwa Tanganyika Farmers Association. Nadhani sasa i dhoofu bin hali. Hamna wakulima Tanzania! tuna peasants, who can not afford to publish a paper.

...Kama ulivyosema, hii si kazi ya serikali. Tatizo ni kuwa magazeti haya yako pale ambapo kilimo kimeendelea na ni cha kisasa kama South Africa. Hawa wana gazeti la wiki na website nzuri, ona Farmer's Weekly | Home ...Vyama vya ushirika kabla ya uhuru vilimilikiwa na wakulima. Baada ya uhuru vika binafsishwa na serikali -ikiwa, pamoja na sababu nyingine, kuhamisha faida katika sekta hiyo na kujengea viwanda na miradi mingine ya kitaifa, ya maendeleo- na kuwekwa chini ya watawala wasio na maslahi ya moja kwa moja katika kilimo. And they failed, just, because of this.

...Kitu cha pekee kitakachofanya SACCOS au VICOBA ziendelee ni transparency na strict codes of conduct. Halafu, lazima ziwe community owned.
 
Hivyo basi, kuendeleza kilimo ni kuondoa umasikini na uhaba wa chakula ni kufikia malengo ya mkukuta na milenia.
...Hii kitu ndio ya hovyo kabisa. Inajali zaidi namba na si ubora wa hizo namba. Mfano, ripoti ya elimu itasema imetekeleza kwa kiasi fulani lengo la milenia katika kuandikisha watoto shule. Swali, Je, watoto hao wanajua kusoma na kuandika? angalau jina lao? Je, shule wanazosoma zina viwango stahiki?. Hivi majuzi waziri mdogo wa TAMISEMI aling'aka juu ya ubora mbaya kabisa wa maabara -kama sijakosea- katika moja ya shule huko Chato au maeneo hayo.

...Tukirudi kwenye sekta husika. Hivi lile josho lililojengwa kule Chato, limemnufaisha mfugaji?. Ila, litaingia kwenye takwimu za milenia! Hii kitu ya MDGs ni scam. We are being made poorer. Tutaona hii vizuri zaidi after some years.
Sasa endapo wakulima wangejipanga vizuri, bila shaka wangedai fidia.
...Wajipange vizuri kwa kuchagua viongozi watendaji, kwanza. Kama hawataweza hilo, hii itakuwa nyimbo maarufu. ...Kilimo cha nanasi na embe kinakuwa kwa kasi kwasababu hakiingiliwi. Soko ndilo linaamua, na kwasasa bado ni zuri. ...Nyingi ya hizi ni mzigo tu, hazina faida inayoonekana kwa mkulima. Zilikuwa na nafasi wakati wa command economy, not anymore.
Inatia uchungu. Nitarudi kesho kutwa!
...Rudi, tufaidike na michango yako!
 
Ijapo kuwa hii mada ni ya miaka kadhaa iliyopita naomba nitoe credit kwenu wakuu ... mkoo vizuri ama hakika Tanzania ina baadhi ya vijana wenye fikira madhubuti sana ... lakini mfumo kandamizi uliopo madarakani hautaki kuwapa nafasi vijana hao ili waweze kuzitumia skills zao vyema zitakazo weza kuivusha nchi hapa tulipo kwama
 
Hahaa ..hiyo aya ya mwisho nimecheka sana ... mkuu uko vizuri sana " siku hizi hauitendei haki jf kabisa ...kwa kutokana na kushinda kwako kwenye Yale majukwaa ya yenye umbea umbea .. jamii yetu inahitaji mawazo kama haya ili iweze kujikwamua kwenye changamoto zinazo izunguka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…