Umeandika maneno mureeeeefu lakini sioni cha maana humo. Sera ya majimbo ndiyo ilitumika mwaka 1884-1885 wakati wa mkutano wa Berlin wa kuligawa bara la AFRICA, baada ya kushindwa siasa sasa CHADEMA mmeamua kugawana mbao kiaina, sera ya majimbo ndiyo inatumika DRC hadi leo nchi ile imeshindwa kustabilize politically, yaani kweli CHADEMA na akili yenu japo ni ndogo mmefikia kufilisika kiasi hiki.
Naawambia mkipata asilimia 10 ya kura zote basi mkaombe misa ya shukrani, tarajieni kipigo cha kushindwa chenye mshindo. Watanzania hawatakubali kubeba jiko la mkaa unaowaka.
sera ya majimbo ni nafuu mara alfu 10 kuliko sera ya ccm ya kulundika madaraka yote ya nchi kwa mtu mmoja tu anayeitwa Rais. Baba wa Taifa alitahadharisha kuwa sera hii ya ccm ni khatari mno na kwamba chini ya sera hii akipatikana kiongoz dikteta watanzania tutakwisha..maguful amepatikana na kweli watanzania tumekwisha.
Baadhi ya viongozi wa ccm kwa kuiona khatari ya udikteta wa maguful walishtuka na kushauri katibaiandikwe upya ili ipunguze madaraka ya huyu mtu lakin maguful alikataa kata kata kwa kujijua yeye ni dikteta na katiba iliyopo ndo inayolinda udikteta wake. Leo hii maguful anamteua kila kiongoz kwenye nafasi ya maamuz nchi hii kuanzia ngazi ya kijiji mtaa hadi Taifa; hakuna hata chombo au taassisi yoyote inaruhusiwa kuhoji wala kushauri, si bunge si mahakama.
vivyo hivyo maguful anaweza kumfukuza kazi mtu yoyote kama mbwa saa yoyote ile, bila kujali utaratibu wowote wa kisheria wala kikanuni uliowekwa. Anaweza kuchukua pesa za taasisisi (mfano mifuko ya jamii) au mtu yeyote yule binafsi (maduka ya kubadilishia fedha za kigeni), mtu yeyote hata mwanaccm anaweza kukamatwa, akafungwa, akabambikiwa kesi, taasisi yoyote inaweza kufutwa na hata maisha ya mtu yanaweza kupotea na hakuna wa kuhoji.
Imefikia mahali nchi imekuwa na kundi ambalo halijujulikani lipo wap linaitwa "wasiojulikana", kundi hili limetuhumiwa kateka watanzania, kuwatia vilema, kuwatesa na hata kuwaua..watanzania hawana la kufanya, Rais amezifunga pingu mahakama, kalifunga pingu bunge na taasisi zote, yeye ni alfa na omega katika nchi ya watu zaidi ya milioni 55...naam, ni mungu-mtu chini ya sera ya ccm ya kulundika madaraka yote kwa mtu mmoja tu aitwaye Rais.
ni heri utawala wa majimbo mara alfu 10 kuliko utawala huu wa mtu mmoja. Chini ya sera ya madaraka yote kwa mtu mmoja hata wanaccm wamebatizwa kwa maji ya moto wakiwemo kina makamba, kina kinana, nape, membe na wengineo. Wastaafu wote kina mwinyi, kikwete nk wote wametiwa kelbu, yan kwa miaka mitano mwanaume nchi hii amekuwa ni mmoja tu...manguful
Kupitia chadema na ACT watanzania tuseme sasa baaaaas. Inatosha. Ni heri majimbo mara alfu 10. Uwe cdm, uwe ccm, chauma, nccr, TLP tuseme ni Lissu...tuseme ni NiYeye...TUJIKOMBOE.
Watanzania nafasi ni hii, haitakuja mara mbili mpaka miaka 5 iishe tena na kuna khatari ya huyu jamaa kung'ang'ania madaraka...tusipoangalia tutajitumbukiza kwenye shimo kwa mara ya pili ambako hatutokaa tupate nafasi ya kutoka tena mda wote jamaaa atakapokuwa hai...hata nyie ccm mtakuja kutamani kumtoa hamtoweza tena; mkihurumiwa sana mtabakia kupigishwa magoti na kuomba msamaha-rejeeni ya kinana.