Habari,mwanangu ana umri wa miaka mitatu sasa lakini amekuwa akisumbuliwa nakifua kisichopona kwa muda mrefu.tatizo lilianza akiwa na mwaka mmoja na miez mitatu alipotumia dawa za minyoo.akaanza kukohoa na dawa nyingi keshatumia za hospitali na za mitishamba lakini zinatuliza tuu tatizo kwa muda mfupi halafu linarudi upya..vipimo kama xray,fbp,allergy,kimeo,vyoote kapima inaonekana hana tatizo ila hali bdo ileile akianza kukohoa mpaka ww uliemshika unalia..na pia hili tatizo huanza pale tuu anapoanza kunenepa.nimewaelezea madaktar wengi,hospitali mbalimbali nao wakimpima wanabaki kusema hii hali itaisha tu.sasa ni rahisi kusema kama tatizo halikugusi naombeni msaada mtoto anateseka sana jamani