Raphael Mtui
Member
- Nov 26, 2024
- 78
- 204
Moja ya vitu sitasahau katika maisha yangu ni pamoja na kipindi nilichoishi kwa mtu ambaye ni almost ndugu yangu.
Ilikuwa miezi mitatu tu lakini nilihisi ni milenia tatu!
Na mwisho wa siku sikulipwa mishahara yote!
Nakumbuka nilivyokuwa nikilazimika kumwibia ili nisife njaa. Hiyo inaniuma sana. Wizi wenyewe ni kuiba vyakula, kupika kwa siri, au kuiba matunda ili nisije 'kukata moto'.
Haya yalitokea miaka zaidi ya ishirini iliyopita, lakini nikikumbuka huwa sio poa kabisa.
Ukisoma stori nyingi za wana JF walio-share na sisi stori za maisha yao, ni nadra kukosa vipande vya hadithi za mateso mhusika aliyopata akiwa anaishi kwa ndugu fulani.
Kuishi kwa bro mjini, kuishi kwa dada, kwa mjomba, baba mkubwa/mdogo, shangazi, nk.
Kundi ambalo nimeona likisulubika zaidi ni pamoja na mabinti wanaoishi kwa dada zao mjini.
Naam, dada wa kuzaliwa tumbo moja. Awe ameolewa au hajaolewa, ila unaishi kwake. Kumekuwa na hadithi za mateso sana.
Vijana waliofikia kwa ndugu mjini kusaka maisha, wengi wameteseka sana si kwa sababu ya ugumu wa maisha, bali kwa sababu za kimanyanyaso!
Nisitilie mkazo mjini tu, hata vijijini pia.
Kwa nini ipo hivi? Kwa nini watu wengi wameteswa na ndugu zao hasa waliotangulia mjini?
Kuna siri gani katika hizi familia? Wanaowatesa ndugu zao wanakuwa wanajua wanachokifanya?
Ni ile hali ya mashindano ya kuhakikisha ndugu yako 'hatoboi' awe mtumwa wako tu?
Kuna nini hasa cha kufundishana katika hizi familia zetu?
Karibu kwa mawazo yako, lakini ni vizuri uka-share stori yako kama uliwahi kusulibiwa na ndugu.
Nzuri zaidi, kama unajua uliwahi kumtendea visivyo ndugu yako uliyeishi naye, na sasa umegundua na inakuuma, share nasi hiyo toba yako hapa.