Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Moja ya vitu sitasahau katika maisha yangu ni pamoja na kipindi nilichoishi kwa mtu ambaye ni almost ndugu yangu.
Ilikuwa miezi mitatu tu lakini nilihisi ni milenia tatu!
Na mwisho wa siku sikulipwa mishahara yote!
Nakumbuka nilivyokuwa nikilazimika kumwibia ili nisife njaa. Hiyo inaniuma sana. Wizi wenyewe ni kuiba vyakula, kupika kwa siri, au kuiba matunda ili nisije 'kukata moto'.
Haya yalitokea miaka zaidi ya ishirini iliyopita, lakini nikikumbuka huwa sio poa kabisa.
Ukisoma stori nyingi za wana JF walio-share na sisi stori za maisha yao, ni nadra kukosa vipande vya hadithi za mateso mhusika aliyopata akiwa anaishi kwa ndugu fulani.
Kuishi kwa bro mjini, kuishi kwa dada, kwa mjomba, baba mkubwa/mdogo, shangazi, nk.
Kundi ambalo nimeona likisulubika zaidi ni pamoja na mabinti wanaoishi kwa dada zao mjini.
Naam, dada wa kuzaliwa tumbo moja. Awe ameolewa au hajaolewa, ila unaishi kwake. Kumekuwa na hadithi za mateso sana.
Vijana waliofikia kwa ndugu mjini kusaka maisha, wengi wameteseka sana si kwa sababu ya ugumu wa maisha, bali kwa sababu za kimanyanyaso!
Nisitilie mkazo mjini tu, hata vijijini pia.
Kwa nini ipo hivi? Kwa nini watu wengi wameteswa na ndugu zao hasa waliotangulia mjini?
Kuna siri gani katika hizi familia? Wanaowatesa ndugu zao wanakuwa wanajua wanachokifanya?
Ni ile hali ya mashindano ya kuhakikisha ndugu yako 'hatoboi' awe mtumwa wako tu?
Kuna nini hasa cha kufundishana katika hizi familia zetu?
Karibu kwa mawazo yako, lakini ni vizuri uka-share stori yako kama uliwahi kusulibiwa na ndugu.
Nzuri zaidi, kama unajua uliwahi kumtendea visivyo ndugu yako uliyeishi naye, na sasa umegundua na inakuuma, share nasi hiyo toba yako hapa.
Hii ndio point ya msingi ndugu anaweza kuwa mbaya ila hali itakuwa mbaya zaidi iwapo huyo mgeni mwenyewe hajielewi hasa tabia za uvivu, uchafu, ubinafsi na kutoa maneno kwa ndugu huyu na kuyapeleka kwa ndugu yule. Ila yote kwa yote hakuna mkamilifu ni muhimu kama binadamu kuwa na subra na kuvumiliana.Hizi nyuzi ni nyingi sana humu,ziunganisheni.
Wengine hushindwa kukaa kwa ndugu zao kutokana na tabia zao mbaya hasa ndugu wa mume huona nipo kwa kaka yangu,nipo kwa baba yangu hiyo huwapelekea kuwa na viburi.
Kwa kuwa upo kwa kaka yako hutaki kusaidia kazi za nyumbani,hutaki kujigusa,una tabia chafu nani atakutaka sasa?
Ila hata umasikini wakati mwingine huchangiaMi ningependa simulizi yako ndiyo iwe somo la kujifunza, maana shuhuda zitakazotolewa hapa zipo katika mfumo mmoja, tofauti ni mazingira pamoja na wahusika.
Sasa waje wataalamu wa saikolojia watusaidie kuliweka vizuri jambo hili, huwa inatokeaje umekubali kwa hiari kumpa hifadhi mtu ili kesho naye aweze kusimama kwa kujitegemea, kisha unaanza kumnyanyasa?
Ama umemwajiri beki tatu au H/boy unaanza kumtesa, why!
Huwa nikifika kwenye sherehe na kuona namna watu walivyokusanyika kwa furaha na bashasha nyusoni mwao, utadhani wameumbwa hivyo kwa ukarimu, lakini ukifika majumbani mwao ni mashetani halisi namna wanavyowatendea wategemezi wao.
Wataalamu waje watuambie, ni nini kisababishi cha hali hiyo kisaikolojia?
PUMBAVU/SHENZI... Ndomana TRUMPH anayafukuza, badala ya kutafuta maisha yao yanataka kuhemea/kufugwa kama Mbwa...Moja ya vitu sitasahau katika maisha yangu ni pamoja na kipindi nilichoishi kwa mtu ambaye ni almost ndugu yangu.
Ilikuwa miezi mitatu tu lakini nilihisi ni milenia tatu!
Na mwisho wa siku sikulipwa mishahara yote!
Nakumbuka nilivyokuwa nikilazimika kumwibia ili nisife njaa. Hiyo inaniuma sana. Wizi wenyewe ni kuiba vyakula, kupika kwa siri, au kuiba matunda ili nisije 'kukata moto'.
Haya yalitokea miaka zaidi ya ishirini iliyopita, lakini nikikumbuka huwa sio poa kabisa.
Ukisoma stori nyingi za wana JF walio-share na sisi stori za maisha yao, ni nadra kukosa vipande vya hadithi za mateso mhusika aliyopata akiwa anaishi kwa ndugu fulani.
Kuishi kwa bro mjini, kuishi kwa dada, kwa mjomba, baba mkubwa/mdogo, shangazi, nk.
Kundi ambalo nimeona likisulubika zaidi ni pamoja na mabinti wanaoishi kwa dada zao mjini.
Naam, dada wa kuzaliwa tumbo moja. Awe ameolewa au hajaolewa, ila unaishi kwake. Kumekuwa na hadithi za mateso sana.
Vijana waliofikia kwa ndugu mjini kusaka maisha, wengi wameteseka sana si kwa sababu ya ugumu wa maisha, bali kwa sababu za kimanyanyaso!
Nisitilie mkazo mjini tu, hata vijijini pia.
Kwa nini ipo hivi? Kwa nini watu wengi wameteswa na ndugu zao hasa waliotangulia mjini?
Kuna siri gani katika hizi familia? Wanaowatesa ndugu zao wanakuwa wanajua wanachokifanya?
Ni ile hali ya mashindano ya kuhakikisha ndugu yako 'hatoboi' awe mtumwa wako tu?
Kuna nini hasa cha kufundishana katika hizi familia zetu?
Karibu kwa mawazo yako, lakini ni vizuri uka-share stori yako kama uliwahi kusulibiwa na ndugu.
Nzuri zaidi, kama unajua uliwahi kumtendea visivyo ndugu yako uliyeishi naye, na sasa umegundua na inakuuma, share nasi hiyo toba yako hapa.
Tulia hukoHapo ndio mnapokosea, tofautisha kusaidia na kuwekeza. Ndugu wengine wanakaba mpaka mtu anakata chain. Unakuta ndio kaanza maisha kapata kazi juzi tu,tayari anaanza kuzogwa na kupewa majukumu. Hapo ni kumtia umasikini
Bila shaka ulisaidia, hukuwekeza kama mradi na sasa unataka kuvuna. Kama ndiyo, basi usione kama una haki ya kusaidiwa. Ana mke, watoto na wazazi ambao ni haki yao. Wengine ibaki kuwa utashi wake tuTulia huko
Wameshatusua
Mkienda kwa watu mjitahidi kusaidia kazi sasa mgeni unakuwa huna tofauti na nyau, unataka ulale tu na kuangalia tv huku ukisubiri chakula kipikwe na hapo unakaa week mbili, Bado siku ya kuondoka hata kufua mashuka uliyolalia hutaki, hapo lazima ndugu wakuchoke hayo kwa uaminifu hatakut
Asante kwa balance nzuri.Ukiishi kwa ndugu jitahidi uact kama house boy/house girl, kazi yoyote unayoiona mbele yako ifanye, usitegee.
Ingawa pia unaweza kufanya yote hayo lakini bado usipewe thamani kubwa kama wazaliwa wa hapo.
Niliwahi kuishi kwa ndugu si zaidi ya mmoja, house gal akiamka naamka naye ingawa alikuwa hapendi kuniamsha lakini hofu yangu ilikuwa nikikutwa na mama mwenye nyumba nimelala itakuwaje?
Nilikuwa nikipatiwa nguo za baba mwenye nyumba kuzipiga pasi hata kama mtoto wa kiume yupo (Kwa madai najua kupiga pasi nguo) nilikuwa napiga pasi fresh tu bila manung’uniko.
Walikuwa ni msaada mkubwa kwangu, ninaamini bila wao nisingefika hapa nilipo. Walinifundisha kujitegemea na kufanya majukumu yangu pasipo kunung’unika mbona fulani hafanyi.
Mwenyezi Mungu awabariki sana na kuwapa maisha marafiki Kwani hata sasa ninaweza kusimama mwenyewe na kupambana na yaliyo mbele yangu pasipo utegemezi.
Hakuna anayefanya kusaidia kazi kwa uaminifu na bado akakumbana na manyanyaso?Mkienda kwa watu mjitahidi kusaidia kazi sasa mgeni unakuwa huna tofauti na nyau, unataka ulale tu na kuangalia tv huku ukisubiri chakula kipikwe na hapo unakaa week mbili, Bado siku ya kuondoka hata kufua mashuka uliyolalia hutaki, hapo lazima ndugu wakuchoke