Tukiwa bado na muwasho washo wa Kadhi Court, naomba ndugu zangu tujadilini chanzo cha matatizo ambayo Kadhi Court inataka kulipunguza kama sio kuliondoa kabisa.
Mimi kwanza nijua avyo kuna Sheria kama tatu zinazo tawala mambo ya Mirathi
1 Taratibu za asili za makabila yetu, ambapo huko nyuma mrithi anakuwa Kaka wa Marehemu au Mtoto Mkubwa wa Marehemu na kuna wengine Mtoto wa Mwisho wa Kiume, na zaidi ya hapo sheria hizi za kijadi zilikuwa rahisi kuzitekeleza kutokana na watu hao kuishi sehemu moja, huko kijijini.
Lakini siku hizi au hata hizo zilileteleza mifarakano mingi katika jamii nyingi ikiwa msimamizi huyo ni mlevi au ana matatizo mengine.
2. sheria hizi za Mkoloni , au zinazotungwa na Serikali kupitia Bunge
3 Sheria au taratibu za Dini zetu iwe Ya Kikristo au ya Kiislamu, ya kipagani itakuwa kwenye taratibu zetu za asili.
Sasa ukiachilia mbali mifumo hiyo tuio nayo kuna kitu kinacho itwa Wosia, ambacho kinasaidia saana katika kupunguza misuguano ya mirathi. lakini bado ipo kutokana na watu wengine kutoandika wosia au wengine kufikiria kwamba wosia lazima utamwachia kitu? hususana watoto wa kiume ambao mwenendo wao wa maisha haukumfrahisha marehemu.
Sasa ili kutatua au kupunguza matatizo kama hayo ningependekeza serikali kuweka katika somo la uraia skipengele hicho cha wosia na taratibu mbali mbali za kuacha mirathi ili kila mtu ajue njia ipi inamfaa kama ni ya kijadi , taratibu za kidini au sheria za kiserikali wajibu wake wa kuacha wosia na kwa wale wanaoachiwa nao waelewe haki zao na wajibu wao.