Matatizo ya Network Marketing Tanzania

Kwa kweli Dr. Said na KeyserSoze mmeandika the best thread discussion in Network Marketing hapa Jamiiforums. Thread nyingi hazikuwa na hoja zaidi ya watu kuponda, kusifia au kujipigia debe kwa njia nyepesi. Mmejaribu kutoka changamoto na Faida zake.

Niongezee kwa kifupi kwa wale waliopo katika biashara na walio nje, hii biashara si lelemama, ni taaluma inayohitaji ujuzi Kama ilivyo kwa daktari, mwanasheria, mhandisi au fani nyingine yoyote. Tofauti yake ni kuwa elimu hiyo haina shule wala Chuo rasmi.

if possible, moderator ungeweka hii mada kuwa 'sticky' pale juu.
 
Kuhusu kuwepo kwa watu ambao wanafaidika sana na hii mitandao Tanzania ni kweli wapo, ila point yangu hapa je ni wengi wa kutosha, au je wale waliofanya kwa muda mrefu na kupata watu kwanini labda hawajafanikiwa kama ambavyo ingebidi wafanikiwe ?

Ngoja nikupe a Case Study..., Nilikuwa ninamfahamu jamaa mmoja aliyejiunga na aliyehusika na watu wa mwanzo mwanzo kuileta GNLD Tanzania / Mikoani..., huyu bwana alifanya kazi na kupata members wa kutosha (kwa mategemeo ya ile residual income) kwamba watu anaowapata atapata comissions through downlines wao na matumizi yao.., theoretically huyu bwana ni kwamba angekuwa amejitengezea pension (hata kama ambacho angekuwa anakipata ni kidogo kila mwezi, ni bora percent ndogo ya kidogo kuliko percent kubwa ya sifuri..).

Sasa in reality ya kilichotokea wale members aliowapata walikuwa hawatumii products.., inafika wakati wanakuwa inactive members (ingawa huenda zile products zingekuwa affordable kwa members wengi huyu bwana angeendelea kupata pension yake ya kazi kubwa aliyofanya ya kutambulisha watu). Ila mwisho wa siku kilichotokea ni backwards effect, watu wanaanza kukata tamaa hata huyu bwana na yeye mwisho wa siku akakata tamaa, na hii pia ninajua wengi hata walioko Forever, wamefanya kazi nzuri sana mwanzo ila members wanaowapata hawafanyi kazi wala kutumia products.

Ndio maana point yangu kubwa ikawa tusiangalie faida ya mwanzo tu kwamba ni kubwa, kama products zingekuwa affordable kwa watu wengi hata kama recruitment itakaposimama watu bado wataendelea kupata commissions za kutosha through movements of products. Mfano mzuri ni mimi ingawa sio member wa Kampuni fulani ila kuna products zao mbili deodorant na lipsy ninazitumia sababu ni affordable na ni nzuri, kwahio kila zikiisha nampigia simu jamaa ananiletea, sasa wangekuwepo watumiaji wengi hili neno residual income lingekuwa reality na sio hivi sasa ni kama illusion.
 
Nakubaliana na KeyserSoze bei ya hizo bidhaa nyingi ni tatizo kwa matumizi endelevu.

Halafu, kwa bidhaa nyingi za wellness, mantiki ya kuzitumia aidha haipo au haieleweki. Niliwahi kuhoji wakati flani GNLD ikiwa 'hot', kwamba ni kwanini ninunue kikopo cha nyanya au karoti iliyosindikwa niache kununua fresh kutoka 'sokoni'? Bei, wakati huo, ilikaribiana na ya tenga kwa Tanga, DSM, etc.!

Nafkiri kama hizo bidhaa zitazalishwa ndani ya nchi husika au zinazokaribiana kiuchumi/kipato itakua nafuu zaidi.
 

Kweli kabisa mkuu fresh ni bora na ina ubora wake.., sasa kama hizi suppliments zingekuwa bei ndogo watu wasingesita wangekuwa wanazibugia kila mara kama vile peremende.., sasa mtu ukiangalia hizi bei ni kama bajeti ya mtu ya nusu mwezi anaona zi bora akasage mlonge na kubugia au Aloe Vera abugie gamba kutoka shambani kuliko kununua hizi na kuweka pengo kwenye bajeti yake ?,
 
Nashukuru sana Keysersoze, kwa kuanzisha maada hii, ukweli ni kwamba watu wengi wa tanzania hawapendi kusoma na kujifunza njia mpya ya kuongeza kipato kama wengi walivyoelezea hapo juu, mimi binafsi profession yangu ni upande wa kompyuta,na natumia komputer masaa mengi zaidi kwa siku, kwa hiyo nikafanya research ni kampuni gani ambayo unaweza kufanya biashara ukiwa tu mbele ya computer yako na access ya internet, itakayonifanya niweze kujenga network ya watu toka pande mbali mbali duniani,maana kwa nyakati hizi biashara ya MLM usiangalie Tanzania tu, angalia biashara ambayo unaweza kufanya maketing dunia nzima na ukapata commisions huko kwa njia ya internet, maana ndo wenzetu huko majuu wanaishi hivyo, mtu yupo nyumbani na Internet yake anafanya biashara.

Hebu waza kwamba una downline wako wapo USA,Canada,Phillipines,Europe,Asia,African country!!,wanaelewa biashara na wanafanya biashara, na wewe kama upline wao unawamanage na kuwafundisha kwa email tu, na kuchati tu, halazimishwi mtu kununua product yeyote, unaweza ukajiunga bure, unapata mafunzo bure, na unapata cheo cha kwanza bila kulipa chochote,ni kwa kufanya baadhi ya activities.

Hii sio get rich quick business, inahitaji mtu anayejua biashara ni nini au anayetaka kujifunza kwa zati, Ukifanya kwa kujicomit vizuri kipato kinakuwa kama ifuatavyo:

$135.30 per month after 6 months ($1,623.60/yr)
$1,458.30 per month after 12 months ($17,499.60/yr)
$3,159.30 per month after 18 months ($37,911.60/yr)
$5,508.30 per month after 24 months ($66,099.60/yr)

Hapo nimekuwa muwazi sana,ntarudia tena hii sio kama Desi Kwamba Unatajirika mwezi ujao,unatakiwa ufanye kazi kwa bidii,ujifunze na kufanyia kazi yale uliyojifunza, pia ujue kiiegereza safi kwa kuwa unawasiliana na ulimwengu wote

Kwa wale ambao wapo makini na kwa kweli walikuwa wanatafuta nafasi kama hii basi, jiunge Bure na click hapa Real Internet Income

Tukutane huko, tufundishane

Nashukuru Sana
 
Hi guys,

Sikujua kama discussion ilendelea tena. Kumbe kuna link ya page ya 2.

Anyway, mimi nataka niwape ushauri kwa yoyote ambaye anayetaka kufanikiwa katika Network Marketing au biashara yoyote:


  1. Sio kila mtu ana sifa ya kuwa mjasiriamali. Research nyingi zilozofanyika marekani zinaonyesha kuwa zaidi ya 90% za makampuni yanayoanzishwa yanakufa. Kwa Network Marketing takwimu ndio hizo hizo. Zaidi ya 90% ya watu kwenye biashara ya mtandao (Network Marketing) hawatotengeza pesa nzuri na sababu kubwa ni kuwa 90% hawana sifa ya ujasiriamali. Hii haijalishi kampuni nzuri kiasi gani. Failure rate itabaki kuwa vile vile. This is how the world economy works. Wachache always watafanikiwa sana kuliko wengi. Hata ufanye nini huwezi kubadilisha. Kujifunza zaidi kuhusu hili unaweza ukasoma Pareto's Principle (80/20 rule) of economics. Kwa hivyo tusijidanganye kuwa kuna kampuni yoyote ambayo ina watu wengi waliofanikiwa kuliko wasiofanikiwa. It just doesn't exist. Kwa hivyo ukitaka kufanikiwa inabidi utoe maamuzi kabla ya kuanza biashara kama unataka uwe katika kundi la 90% au 10%. Na kama unataka kuwa kati ya 10% ya watu wanaofanikiwa basi ni vizuri ukawatafuta hao 10% wakusaidia na wewe ufanikiwe.
  2. Kuna Supply & Demand na wewe ni supplier: Kwenye soko lolote kunakuwa na wauzaji (ambao wanakuwa ni wachacho - usually less than 10%) na wanunuzi (wanakuwa wengi - more than 90%). Na wanunuzi mara zote wananunua bidhaa kutokana na mahitaji. Kama wewe ni mjasiriamali (au Network Marketer) na unaona market imefikia saturation (ingawa ki ukweli kitu saturation hakuna - nitaprove sasa hivi), unatakiwa utengeneze demand.
  3. Kwenye Network marketing, Kuna makampuni yanayolenga maskini, middle class na matajira na yapo mengine yanalonge spectrum nzima (yaani maskini mpaka matajiri). Na bei za products zao zina range kati ya $20 mpaka $20,000 au zaidi. Kama unataka kutengeneza pesa nyingi kwenye biashara ya Network Marketing, ni bora u promote bidhaa zenye thamani kubwa (high ticket products) kwani hizo bidha zinakupa faida kubwa. Tutake tusitake huo ndio ukweli.
  4. Jifunze marketing. Hii kitu nasisitiza kwa wajasiriamali wengi sana lakini wananipuuza. Mike Dillard (founder wa Magnetic Sponsoring) anasema sababu kubwa ya Network Marketers kufeli ni kuwa

    "Network Marketing is a business of Marketing & Promotion run by people with no experience with marketing and promotion".
  5. And offcourse Be professional: Hii ni profession sio upatu. Na mtu huchukua muda kujenga profession.

Sasa nikija kwenye issue ya saturation. Saturation is only true for the 90% of inexperienced Network Marketers.

Off course ukijenga biashara yako kama 90% ya wenzake unakuwa huna USP (Unique Selling Proposition). Wewe unakuwa kama ma elfu ya wengine.

Let me give you a real case study.

Kuna Kampuni ilikuwa launched November 2010 iitwayo Empower Network. Kampuni hii ilikuja na system mpya ya ulipaji ya 100% commision (yaani 100% ya mauzi analipwa muuzaji) [Jinsi gani kampuni inavyotengeneza pesa ni discussion ya thread nyengine lakini wewe jua kuwa kampuni iliamua kuwalipa members wake 100%]

Kitu kilochotokea ni kuwa watu walimiminika kwenye hiyo kampuni kwa kasi kubwa kupita maelezo. Baada ya mwaka members walilalamika kuwa kampuni imefikia saturation na walikuwa wanahangaika ku recruit new members.

December mwaka 2011 alijiunga kijana mmoja aitwae Vic Strizheus (you can google him if you want) akafanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika ndani ya profession ya Network Marketing.

Ndani ya siku 28 baada ya kujiunga, alitengeneza commission ya $710,000 ambayo ni record kwenye Network Marketing. I won't go deep amefanya nini kuweza kugenerate massive income ya namna hiyo. Kwa maelezeo zaidi unaweza kutembelea website yako hapa: The '$710,000 In 28 Days' Case Study

In short kitu kikubwa anachofundisha ni kuwa kitu saturation hakuna hasa ukijua jinsi gani ya kuji position kwenye market. Makampuni yote makubwa wanaelewa. Ndio maana unakuwa yanadumu kwa miaka mingi sana.

Ni hayo tu kwa leo. Natumai mmenufaika

Dr. Said
 
Nimesoma tena na tena bandiko Na. 25 & 26, waingereza wanasema, 'if it is too good to be true...'! Halafu zimekazia zaidi kupata pesa haraka - 'Get rich quick schemes/scams'. Si kwamba siamini kuhusu kufanikiwa huko, bali wakati mwingine ni kama 'ladder games' tu (DECI, Upatu, n.k.)

Hua wanatumia mifano ya wachache sana waliofaidika sana (mara nyingi ni wale walioingia mwanzoni, ama waliokuja baadae na fikra/utaratibu fulani mbadala) kuvutia hiyo miradi. Ugumu uliopo hua haupewi nafasi kabisa. Wanaofuatia hua wanafaidika kawaida ama hasara kabisa. Natamani wajitokeze wabongo wengi waliofanikiwa sana na haya mambo ili akina Tomaso washawishike.

Mwishowe, sio kila kitu ni kwa kila mtu. Wenye nia, uwezo, ujuzi na ari ya MLM/NM ndio watafanikiwa ila pia ni kwa jitihada kubwa tu kama ilivyo kwa biashara halali za aina nyingine.
 
Faida kubwa ya Network marketing ni ile Network / Connection....

Hivyo ukijiunga Network Marketing yoyote tumia network yako kuwauzia / kuwapa service ya vitu vyako...

Hata kama haujajiunga Network Marketing katika Maisha jaribu kuwa na Network
 
Kwa kweli Dr. Said na KeyserSoze mmeandika the best thread discussion in Network Marketing hapa Jamiiforums. Thread nyingi hazikuwa na hoja zaidi ya watu kuponda, kusifia au kujipigia debe kwa njia nyepesi. Mmejaribu kutoka changamoto na Faida zake.
Hakuna kitu ambacho hakina Pros and Cons..., ila kuna kitu kama kina mianya ya watu kufanya abuse na wakifanya abuse hupelekea kila kitu kionekane hakifai
Niongezee kwa kifupi kwa wale waliopo katika biashara na walio nje, hii biashara si lelemama,
Sio lelemama sababu watu wanafanya kitapeli na nyingi ya hizi sio product centered au service centered bali ni recruitment groups; yaani kinachofanyika ni kupata pesa kwa mgongo wa membership fees
ni taaluma inayohitaji ujuzi Kama ilivyo kwa daktari, mwanasheria, mhandisi au fani nyingine yoyote. Tofauti yake ni kuwa elimu hiyo haina shule wala Chuo rasmi.
Mimi hii sipendi kuiita Biashara per-se bali kwanza iwe ni mtu kujipatia products au services biashara ije afterwards kama ingefanyika kama inavyotakiwa hakuna kitu rahisi kama hiki sababu wewe utajiunga sehemu ili upate services au products pesa inakuwa ni matokeo ya baadae...

Lakini ukitaka upige pesa tumia network yako kuuza bidhaa zako au services nyingine au kunuifaka zaidi usiuze tu products au services za Kampuni yako....

Use your Network for Leverage....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…