George Kahangwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2007
- 547
- 148
Sasa hapa ndugu yangu kama CCM pananuka na upinzani hapafai ni nini tumaini la watanzania? Je, tuanze kuipekuwa jamii yetu tuwapate tunaowaamini hata kama hawajaonesha nia ya kugombea au hawako kabisa katika mojawapo ya kambi hizo mbili tuwatume kazi,au tufanyeje?Mmhhh! pole pole mkuu, adui wetu hapa ni ukosefu wa utawala bora unaojali sheria, tungekuwa nao basi kuna viongozi wengi kuanzia upinzani mpaka CCM wasinge-qualify kuwa viongozi, matokeo yake ni tumejaza viongozi wengi wasiokuwa na uwezo walionunua uongozi kwa kutumia utawala wetu wa sheria zisizoheshimiwa, na mwisho kulididimiza taifa.
Uchaguzi sio tatizo ni kuheshimu sheria za uchaguzi, viongozi wengi wa pande zote mbili, wamenunua uongozi kwa kuvunja sheria, hivyo nia na lengo lao ni moja nalo ni kuvuruga uchaguzi ili waendelee na ulaji wao wa ruzuku,
Upinzani kutuongoza kutoka kwenye hili tatizo, I do not think so, maana so far tunasikia matatizo yanayofanana fanana betweeen CCM na Upinzani, kwa upinzani tulio nao sasa siuamini kwa sababu so far waneshindwa kuwashawishi wananchi wasiwapigie kura CCM, maana yake ni moja tu kwamba hawaoni kwamba upinzani una anything new to offer, besides, upinzani wenyewe ni Zitto, Dr. Slaaa, Lisssu, Freeman, na Mnyika, Kitila, na Mwanakijiji, sasa tunawapaje taifa letu watu sita tu?
Ndugi Kite Munganga,Watanzania acheni kuzunguka simtumie shortcut?watu wapo na vitendea kazi vyakumwaga sasa nini?
Tanzania yenye neema inawezekana
SHUKRANI
Mwenyezi Mungu Baba, sisi tulio wanao tunakushukuru kwa kutupa nchi yenye neema na amani. Tunajua kwamba umeipendelea sana Tanzania kwa raslimali ambazo hakuna popote duniani.
Asante kwa kuiumba Tanzania kwa kuizungushia maji makuu-Bahari na Maziwa makubwa, kutupa mbuga za wanyama ambazo hakuna popote duniani, kutupa madini ambayo hakuna popte duniani.
DUA
Na alaaniwe kiongozi yeyote aliyepewa madaraka ya kuiongoza nchi yetu na kuitumia nafasi yake kujineemesha yeye na familia yake kwa hasara ya Wtanzania na Tanzania
Na watu wote waseme Amin!
Na walaaniwe viongozi wote tuliowaamini na kuwapa madaraka ya kutuongoza lakini wanaona nchi ikihujumiwa, wananchi wakiteseka bila kuchukua hatua yoyote.
Na watu wote waseme Amin!
Na alaaniwe mtu yeyote ambaye kwa sababu yoyote anawaunga mkono Mafisadi wanaolitafuna Taifa letu tukufu na kuendelea kuwafukarisha Watanzania.
Na watuwote waseme Amin!
Na alaaniwe mtu yeyote anayetaka kugombea nafasi ya kisiasa kwa ajili ya maslahi binafsi
Na watu wote waseme Amin!
Wabarikiwe, viongozi wenye kuumizwa na hali mbaya ya Watanzania na wenye nia ya kweli ya kupambana na kuutokomeza ufisadi.
Na watu wote waseme Amin!
Tanzania yenye neema inawezekana!
OK.NAOMBA WANA JF KILA MTU ACHANGIE NI TANZANIA YA AINA GANI
AMBAYO UNAITAKA......
binafsi napenda tanzania ingekuwa nchi ambayo...
hakuna malalamiko ya ufisadi kabisa....
watu tunaweza kubadili serikali bila mizengwe ya uchaguzi..
watu ni wapole na wana amani ya moyo....
miji yote iko planned na kuna physical address...
elimu mpaka chuo kikuu ni bure au accessible kwa wengi..
hakuna mabishano ya dini,dini ibaki kuwa suala la mtu binafsi..
wanawake tunawaheshimu na kuwalinda....no sex bribe.no sexual harrasement
watoto wanalindwa na kupewa nafasi ya kuwa watoto
matibabu ni kwa wote...
vyakula havipandi bei kiholela...
bidhaa kama nguo na furniture zinatengenezwa hapa hapa 80 percent
watu wana culture ya kusoma vitabu na kuandika vitabu
clean public transport mijini....
wireless internet free everywhere
music na film industry zipo sawa...
mengine ongezeni....
What have you done to realize Tanzania you want? or you have delegated to others to do it on your behalf?
napenda tanzania iwe:
Yenye demokrasia na uwazi. Fursa za uchumi (kama uwekezaji) ziwe kila mkoa chini ya mkakati wa kitaifa. Kwa mfano, kama mkoa fulani una rasilimali fulani nyingi kuliko mwingine basi ufanywe kuwa maarufu kwa sekta hiyo. Tanzania, ingekuwa na mkoa makao makuu ya masuala ya fedha, mkoa makao makuu ya masuala ya utalii, mkoa makao makuu wa masuala ya kilimo, mkoa makao makuu wa masuala ya elimu ya juu, mkoa makao makuu wa maswala ya utawala, mkoa makao makuu kwa masuala ya viwanda vikubwa, mikoa yenye viwanda vya kusindika mazao ya kilimo n.k.
Tanzania ya namna hiyo ingekuwa na mandhali nzuri kila mkoa nchini, ajira kila mkoa nchini, dar es salaam isingekuwa na magari mengi kuliko huduma ya barabara zilizopo, watu dar es salaam wasingekuwa wengi kiasi hicho. Na uchumi wa watanzania ungekuwa juu zaidi.
Tanzania yenye rais asiyekuwa menyekiti wa chama tawala, tanzania yenye kusamini wasomi kama rasilimali adimu na muhimu kwa maendeleo ya nchi. Tanzania yenye taasisi kama takukuru iliyo huru, tume ya uchaguzi ya taifa iliyo huru kwamba wakurugenzi wake siyo wateule wa rais.
Na kwa mazingira hayo, tanzania ingekuwa na huduma bora za kijamii na miundombinu imara zaidi na ya kiushindani wa kimataifa kibiashara. Kisingekuwa na hata ufisadi maana nchi ingetawaliwa na demokrasia na utawala wa uwazi zaidi. Nani angeweza kuiba mali ya umma katika mazingira hayo? Hakuna!!
what have you done to realize tanzania you want? Or you have delegated to others to do it on your behalf?
Tanzania ninayoitamani ni ile ambayo hakuna ubaguzi wa aina yoyote ile bali viongozi wa siasa wanachaguliwa kwa misingi ya upendo na uchungu kwa nchi ya Tanzania. Tanzania ambayo watu hawabaguani kwa imani ya kisiasa, dini wala kabila. Ni Tanzania hii ambayo itafuata kigezo cha utumishi wa mtu uliotukuka kama wa Dr Slaa. Ambapo watu bila kujali dini, kabila, na chama cha mtu, mtanzania Dr Slaa mwenye utumishi uliotukuka anakuwa rais wa nchi yetu.
Hivi jamani bado mpaka leo kiswahili kinawapa tabu baadhi ya wakazi wa maeneo mengi ?Tatizo hapa watu wametia zege za masikio hawawezi kusikia tena kwa kifupi Dr Slaa hata kama atashinda kwa kishindo ambacho hajawahi kushinda Rais yeyote yule katika Ulimwengu huu tunaoishi, ushindi huo hautowafanya CCM wampe Urais Dr slaa,Hilo msahau CCM wapo very very Advice wacheni nyinyi ,binafsi naomba kwa Mmungu Dr slaa awe Rais atalivuwa Taifa hili na watu wake watabadilisha hali ya maisha na kuwa maisha ya Kibinadamu hasa walio vijijini wanaoshi maisha kama vile ya wanyama pori , lakini hapa pia tuwe wakweli wengi wetu hatujuwi wapizani wake wapo Desperate kiasi gani ,kwanza tuombe afike hiyo siku ya Uchaguzi (usilivuke Daraja Kabla hujalifikia)
Kama watanzania wengi wataamua kulinda haki yao na kukubali lolote naliwe lakini haki itendeke, tutaweka utaifa mbele na kutumikia taifa kwa mfano wa Dr Slaa. We need changes in our country especially kwenye uongozi, tunajitia umasikini sie wenyewe bila kujua.
Ushabiki wa kisiasa, danganya toto na kuendelea kuwalea watu ambao tayari wanazo, watanzania tunaona tumebadilika ila kijijini ni bado. Watu wanaonewa, hawafanyiwi haki kwa vile hawajui haki yao.