Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

NINAWEZA SEMA HII NI KATI MAMBO YA MSINGI SANA TUNAYOTAKIWA KUJADILI.......HIZI KELELE ZOTE HUMU JF SI ZA BURE.......(unless kuna watu wametumwa kama inavyosemekana) TUJADILI MUSTAKABALI WETU KAMA TAIFA.....NA SI CHAMA,DINI,KABILA AU KIKUNDI....!
SASA BASI SULUHISHO LA MATATIZO YA TANZANIA KWA UPANDE WANGU NINA PENDEKEZO MOJA.....!
AJIRA:SERIKALI IWE NDIO MWAJIRI MKUU ILI KUPUNGUZA LINDI LA JOBLESS.....(zamani nilifikiri neno jobless ni jambazi kwani wazazi wangu walikuwa wakiwaita vijana fulani kuwa wale ni jobless) KWA KUWA AJIRA ITAKUWA INAPATIKANA SERIKALINI( wasisahau kurudisha jeshi kwa mujibu washeria)HUKU TUNA VIJANA WAZALENDO.....NATUMAI MISHAHARA ITAKIDHI HAJA YA FAMILIA NYINGI(tukumbuke waafrika ttuna extended families) KWANI KATIKA FAMILIA MOJA YENYE FAMILI MEMBA SEI 10....5 WANA AJIRA YA UHAKIKA SERIKALINI....WATU HAWA WATAJENGA,WATAKULA,WATATIBIWA(utaratibu wa kutibu famili memba wa mfanyakazi nk)HIVYO KUINUA HALI YA KIUCHUMI YA MTU MMOJA MMOJA.....!
 
Ndugu mahesabu,
Ahsante sana kwa kuchangia mada.Jambo ulilolitaja la ajira ni kweli ni moja ya mambo ambayo yanapaswa kutazamwa sana. Ni kweli pia kwamba serikali inao wajibu wa kutimiza hapa. Lakini hapo kuna tatizo ndani ya tatizo,serikali ya viongozi hawa hawa ambao co mission yao ni kujinufaisha tu wao wenyewe. Labda useme wazi serikali ipi ya watu wapi.
Aidha, nikudokeze kuwa mbali na sekta ya umma ambayo inaongozwa na serikali, katika sekta binafsi,hususan ile inayooshikiriwa na wawekezaji toka nje,wamekuwa wakitaja kwamba nchini kwetu kuna uhaba wa raslimaliwatu wenye ujuzi unaoendana na shughuli ambazo wawekezaji hawa wanakuja kufanya.Tatizo linadaiwa kuwa kubwa kiasi kwamba wanalazimika kuja na watu wao toka ng'ambo. Hapo napo lazima tutafute dawa.

Vile vile fikiria juu ya sekta kuu inayowaajiri vijana wetu kwa sasa hasa hasa mijini(uchuuzi au umachinga), je hii ni sekta sahihi na kama si sahihi mbadala ni nini, je,tuwaelekeze vijana wetu katika sekta kama vile kilimo?
 
bwana Kahangwa

dawa ya Tanzania ni system!. system imekufa, inabidi tuisuke upya.tena si kuisuka upya tu, inabidi tuisuke kisawasawa,
taasisi karibu zote Tanzania zinakwenda kiujanja ujanja. just imagine!,

kama chuo kikuu chenyewe ambako ni kitivo cha wasomi vyoo vimekufa na hakuna juhudi za kudumu za kuboresha sanitation utaweza kweli kumshauri mwananchi wa kijijini mwenye kutumia kichaka kumaliza haja zake kuhusu umuhimu wa choo bora?.
 
Tatizo letu kubwa bongo ni kukosa respect kwa rule of law, ninaaamini siku tutakapoelewa hilo na kulitimiza, the rest vitafuata vyenyewe.
 
Ndugu Gamba la nyoka,
Nakubaliana na wewe kuhusu ubovu wa systems(mifumo) tuliyonayo na haja ya kuisuka upya(hapo waweza rejea mada yangu ya pasaka ya Tanzania haijawadia bado,ambamo nilidokeza baadhi ya mifumo ya kubadilishwa). Hata hivyo swali kuu linabaki, ni nani atafanya huo usukaji upya? Katika mchango wako unasema inabidi tu...je, ni watanzania wote tuhusike katika hili, tuanzie wapi tuanzeje na lini tuanze, na tena wako wapi hao wa kuongoza mageuzi hayo? kwa ufupi bila watendaji hapo huoni tutabaki kuwa na good wishes tu?
 

Tanzania bado hatujajifunza kuheshimu sheria, in fact inaonekana kuna sheria mbili, moja ya matajiri na viongozi, nyingine ya masikini, as the results waliotuibia kwenye Richimonduli, wameishia kujiuzulu tu, huko BOT wameambiwa kuzirudisha tu hela walizoiba, that is what I am talking about, maana tukiendelea hivi, hata siku moja hatutakuja kupata maendeleo wala mabadiliko muhimu kwa taifa letu, na ni kwenye hiki kipengele cha kukosa respect kwa rule of law, ndipo tunapoishia kupata viongozi wengi wabovu ambao wanavizia weakness zetu kwa sheria na kununua uongozi, ndio maana ninasema Tanzania tunahitaji only one big step forward, nayo ni kuheshimu utawala wa kisheria.

ya serikali inayotumia mabilioni COMORO huku inashindwa kuchonga bara bara kule mufindi?

Nafikiri hiii sio mahali pake hapa, si kuna thread yake tayari mkuu, au?
 
GT Comoro AU inafoot bill, kwa hiyo hakuna issue ya Tanzania kutumia hela.
 
Ndugu Gamba la nyoka,
Nakubaliana na wewe kuhusu ubovu wa systems(mifumo) tuliyonayo na haja ya kuisuka upya(hapo waweza rejea mada yangu ya pasaka ya Tanzania haijawadia bado,ambamo nilidokeza baadhi ya mifumo ya kubadilishwa). Hata hivyo swali kuu linabaki, ni nani atafanya huo usukaji upya? Katika mchango wako unasema inabidi tu...je, ni watanzania wote tuhusike katika hili, tuanzie wapi tuanzeje na lini tuanze, na tena wako wapi hao wa kuongoza mageuzi hayo? kwa ufupi bila watendaji hapo huoni tutabaki kuwa na good wishes tu?
hili vugu vugu unaloliona katika jf, na katika duru mbali mbali za wananchi ni miongoni mwa viashiria chanya kwamba jamii ya watanzania imeanza kuona kwamba some thing must be done.

kwa kuanzia tu, lazima tufanye reform kubwa katika suala la Chakula nchini. wananchi wakishiba hawatababaishwa na wanasiasa uchwara na takrima zao, wakishiba watafanya kazi zenye tija, wakishiba watafikiri na kuvumbua au kuboresha.

then lazima tufanye reform katika elimu, elimu yetu inageza mifumo ya kizungu na output ni watu wachache wenye theory nyingi kichwani lakini mchango usiotosha katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo, watu wanashabikia vyeti badala ya uwezo, ndo maana watu wako radhi kuchongesha vyeti bila kujali kuulizwa utaalamu wao ni upi?.

hizi front mbili ukianza nazo utagundua kwamba nyingine zinategemea sana hizi mbili.

tunaweza pia kuwa na jeshi dogo lakini la kisasa, ambalo tutalipa vifaa vya kutosha na vya kisasa, halafu gharama itakayopunguzwa iingizwe katika elimu bora.
 
Tanzania bado hatujajifunza kuheshimu sheria, in fact inaonekana kuna sheria mbili, moja ya matajiri na viongozi, nyingine ya masikini, as the results waliotuibia kwenye Richimonduli, wameishia kujiuzulu tu, huko BOT wameambiwa kuzirudisha tu hela walizoiba, that is what I am talking about, maana tukiendelea hivi, hata siku moja hatutakuja kupata maendeleo wala mabadiliko muhimu kwa taifa letu, na ni kwenye hiki kipengele cha kukosa respect kwa rule of law, ndipo tunapoishia kupata viongozi wengi wabovu ambao wanavizia weakness zetu kwa sheria na kununua uongozi, ndio maana ninasema Tanzania tunahitaji only one big step forward, nayo ni kuheshimu utawala wa kisheria.



Nafikiri hiii sio mahali pake hapa, si kuna thread yake tayari mkuu, au?


doesnt matter

zote zinahusiana
 
Ndugu Field Marshal na Game Theory,
Nawashukuruni kwa kuchangia. Utawala wa sheria ni muhimu sana,lakini ni muhimu zaidi sheria zenyewe ziwe ni zile zinazotenda haki(rejea thread ya haki huinua taifa, sehemu inayozungumzia sheria)tena kuwe na utaratibu thabiti wa kuwashughulikia kisheria wanaohuika kuzitunga kisha wao wenyewe wakazivunja. Inabidi pia tuondokane na utararibu wa watu fulani kuwekewa kinga au kuwa juu ya sheria.
Naomba mtafakari na hili pia, kwamba utaratibu wetu wa kisheria uko kwa maslahi ya nani.Chukulia mfano wa watu kadhaa wanaopoteza haki zao kwa sababu ni maskini hivyo hawawezi kumudu kuwalipa mawakili wazuri wa kutetea haki zao katika vyombo vya sheria.
Aidha,kama tuna watawala na wanajamii wasioheshimu sheria, chimbuko la tatizo hilo ni nini(mzizi wa fitina) ili tuuchimbue usiendelee kulitesa taifa?
 
Aidha,kama tuna watawala na wanajamii wasioheshimu sheria, chimbuko la tatizo hilo ni nini(mzizi wa fitina) ili tuuchimbue usiendelee kulitesa taifa?
mzizi ni malezi!.
hatuna sera ya malezi Tanzania, sera ambayo ingempa mwongozo mzazi bila kujali mzazi huyo ni masikini au tajiri jinsi ya kumkuza mtoto katika hatua mbali mbali za ukuaji.


tungejuwa na sera hiyo, bila shaka tungekuwa na mwongozo mzuri wa kutrain watoto katika kufahamu mambo kadhaa kila wanapofikia hatua fulani ya ukuaji,hii ingesaidia kuwafundisha watoto wetu haki zao na majukumu yao kwa taifa. ila kwa system tuliyanayo ya kila mtu kivyake bila common grounds, watoto wetu wanakua katika mazingira tofauti tofauti ambayo hayan spirit inayorandana.

pasi na sera ya malezi madhubuti,elimu ya msingi pekee haitoshi kuadress malezi bora kwa watoto wote,bimaana mtoto wa masikini na wa tajiri
 
Hatujachelewa sana, tunaweza tukaamka tukiamua. Tunapaswa kuanza kuweka mfumo utakaweka bayana wajibu wa serikali na rai wake. Kwa sasa ni kama vile wananchi wanaamini kwamba serikali inapaswa kuwafanyia kila kitu na serikali nayo inafikiri kwamba haiwezi kufanya lolote bila michango ya wananchi. Matokeo yake: wananchi wanailaumu serikali na serikali inawalaumu wananchi. Palipotakiwa kupeleka hela za kodi hatupeleki, pale ambapo hatukutakiwa tupeleke ndipo tunatupeleka.

Ili tuanze safari yetu ya kujikwamua na madubwana tuliyojitengenezea tunahitaji uongozi. Uongozi hauwezi kuwa huu wa CCM ambao wanasema hata chanzo cha umaskini hawajui. Kwa hiyo tunarudi kulekule, hatua yetu ya kwanza kabisa ya kutoka hapa tulipo ni kuiweka CCM pembeni, tuanze na chama kingine. Sasa tutazunguka weeeeeeee, ukweli unabaki palepale bila kubadilisha chama (mfumo), tutaendelea kucheza mdori na hii forum itajaa malalamiko yetu mpaka ipasuke.

Kwa hiyo basi mada hii inapaswa, pamoja na mambo mengine haya, kujadili:

i) namna ya kuwa-mobilise wananchi waelewe hatari wanayozidi kujitengenezea kwa kuendelea kuichagua CCM

ii) namna ya kuwatia ujasiri wanasiasa wenye mwelekeo, uzalendo na uwezo wa kiuongozi kujiunga na upinzani ili kuimarisha na kuvijenge taswira chanya vyama vya upinzani ikiwa ni njia ya kuviandaa kupambana na CCM na hatimaye kuongoza mabadiliko tunayotaka

Summary: adui wetu hapa ni CCM. Fursa peke tuliyo nayo wa kummaliza huyu adui ni uchaguzi. Silaha yetu hapa ni kura za wananchi. Jemadari wetu ni upinzani. Kazi yetu hapa JF ni kumpa mafunzo huyo jemadari ili aje atuongoze katika kumteketeza adui.
 
hili vugu vugu unaloliona katika jf, na katika duru mbali mbali za wananchi ni miongoni mwa viashiria chanya kwamba jamii ya watanzania imeanza kuona kwamba some thing must be done.

kwa kuanzia tu, lazima tufanye reform kubwa katika suala la Chakula nchini. wananchi wakishiba hawatababaishwa na wanasiasa uchwara na takrima zao, wakishiba watafanya kazi zenye tija, wakishiba watafikiri na kuvumbua au kuboresha.

then lazima tufanye reform katika elimu, elimu yetu inageza mifumo ya kizungu na output ni watu wachache wenye theory nyingi kichwani lakini mchango usiotosha katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo, watu wanashabikia vyeti badala ya uwezo, ndo maana watu wako radhi kuchongesha vyeti bila kujali kuulizwa utaalamu wao ni upi?.



hizi front mbili ukianza nazo utagundua kwamba nyingine zinategemea sana hizi mbili.

tunaweza pia kuwa na jeshi dogo lakini la kisasa, ambalo tutalipa vifaa vya kutosha na vya kisasa, halafu gharama itakayopunguzwa iingizwe katika elimu bora.

Hakika umegusa maeneo nyeti tena yenye uhusiano, chakula na elimu.Tena haipaswi kuwa chakula ili mradi bali lishe bora kabisa ili walao wajengeke kiakili waweze kupokea kisawasawa maarifa na stadi wapatazo kwa njia ya elimu.
Nimedokezwa na wataalamu kwamba asilimia 40 ya watoto wa kitanzania wa sasa wamedumaa kiakili.Wamedumazwa na nini? -lishe duni, bila shaka hawa hata ungekuwa na mitaala iliyoshushwa kutoka peponi haitasaidia.
Uko kuchinga vyeti ni indcator nyingine ya mfumo wetu wa elimu kushindwa kujenga taifa la watu wenye maadili.Tuendelee kutafakari
 
Ndugu mahesabu,
Ahsante sana kwa kuchangia mada.Jambo ulilolitaja la ajira ni kweli ni moja ya mambo ambayo yanapaswa kutazamwa sana. Ni kweli pia kwamba serikali inao wajibu wa kutimiza hapa. Lakini hapo kuna tatizo ndani ya tatizo,serikali ya viongozi hawa hawa ambao co mission yao ni kujinufaisha tu wao wenyewe. Labda useme wazi serikali ipi ya watu wapi.Aidha, nikudokeze kuwa mbali na sekta ya umma ambayo inaongozwa na serikali, katika sekta binafsi,hususan ile inayooshikiriwa na wawekezaji toka nje,wamekuwa wakitaja kwamba nchini kwetu kuna uhaba wa raslimaliwatu wenye ujuzi unaoendana na shughuli ambazo wawekezaji hawa wanakuja kufanya.Tatizo linadaiwa kuwa kubwa kiasi kwamba wanalazimika kuja na watu wao toka ng'ambo. Hapo napo lazima tutafute dawa.

Vile vile fikiria juu ya sekta kuu inayowaajiri vijana wetu kwa sasa hasa hasa mijini(uchuuzi au umachinga), je hii ni sekta sahihi na kama si sahihi mbadala ni nini, je,tuwaelekeze vijana wetu katika sekta kama vile kilimo?

SERIKALI INAPOAMUA KUAJIRI NI TARATIBU TU KUFUATWA( samahani ninapotaja serikali na maamuzi yake si mawaziri ambao ni wanasiasa zaidi)NAFASI ZINATANGAZWA AU SELECTION KUFANYIKA KUPITIA KILA KIJIJI AU KILA KATA.....VIJANA WENYE UJUZI NA ELIMU TOFAUTI...WANAPOANDIKISHWA(utopia?) WANAPELEKWA NATIONAL SERVICE...HUKO NI MAJINA TU(ikiwezekana kwa alphabet) "A" MPAKA "H" HESABU NAMBA.......NYIE MFATENI AFANDE ALFONSI......MTAENDA CHUO CHA KILIMO KWA AJILI YA KUWA MABWANA SHAMBA "H" PEKE YAO MFATENI AFANDE MWITA.....HAWA NI WAHASIBU......"G"MPAKA "T" NYUMA GEUKA...MBELE TEMBEA...HAWA WANAENDA BUTIMBA TTC......NK...NK...NK...(nafasi zote hizo kwa kuzingatia elimu ili tuzalishe wataalam)

KUHUSU MAPONJORO WANAOSEMA KUWA LABOURFORCE HAITOSHI NA KUKIDHI KIWANGO HIVYO KUJA NA WATAALAM WAO 90%NI WAONGO...WENGI WAO HUJA NA KUFUNDISHWA KAZI NA WAMATUMBI KISHA WAO KULIPWA ZAIDI KWA MADAI NI WATAALAM TOKA NJE......HIYO10%ILYOBAKI AMBAYO HUENDA KWELI HATUNA WATAALAM WA KUTOSHA .......WE HAVE TO INVEST IN EDUCATION ILI KUKOMBOA TAIFA LETU....(free education-socialism ilifanikiwa kwa hili)

KUHUSU CHINGA.....HIYO WANAYOFANYA SIDHANI KAMA NI UKOMBOZI KWAO KWANI WANAFANYA....HAND TO MOUTH....KILIMO NI JAWABU TOSHA KWA WENZETU HAWA (sio cha jembe la mkono au ng'0mbe...ni tractors,sowers,weeders,harvesters,etc NA KILIMO KIWE CHA IRRIGATION...MASHAMBA YAWE FROM 100 ACRES A PIECE ONWARD.....!
DOING THIS AND OTHER BUSINESSES WILL GIVE "SOLUTIONS TO TANZANIA PROBLEMS"
 
Mkuu Kahangwa,

Sheria Tanzania, tunazo tena nzuri sana, lakini hazijawahi kutekelezwa na hili linaanzia kwenye awamu ya kwanza, tunaaambiwa Mwalimu, alijua kuwa kiongozi fulani ni mwizi na mla rushwa, lakini never of what he did kufuata sheria,

Kule kuna sehemu Mzee Kisori, with all due respect to him na article zake, inasikitisha sana kuwa the man anasema maneno mengi sana ambayo yanahusu viongozi wabovu ambao Mwalimu alikuwa akiwajua wazi, lakini hasemi kwa nini hata yeye hakumshawishi Mwalimu kuwafikisha kwenye sheria, I mean mimi binafsi nilishamsamehe Mwalimu, kuwa aliyoyafanya alifanya, yanayotokea sasa ni yetu wenyewe hana anything to do with it,

Hili la sheria ndilo hasa linaloturudisha nyuma mkuu, wananchi wasioheshimu sheria, hawawezi kuleta maendeleo kwa taifa, kwa sababu watasubiri njia za mkato katika kutafuta maisha, sheria tunazo nzuri sana na zingine zinatakiwa kufanyiwa marekebisho, lakini tulizonazo zikifuatwa na kukemewa kwa makini, ninaaamini tutasonga mbele, unakumbuka Marehemu Sokoine alifikia mahali alianza kuhudhuria vikao vya mahakama kila alipoona kesi ni nzito na ina wasi wasi wa hakimu kupewa rushwa, pole pole mchezo wa rushwa ulianza kuisha, mahakimu walifikia mahali walianza kukataa rushwa,

I mean can you imagine Lowassa na Karamagi, Msabaha, wangekuwa jela saa hizi au kesi zao ziko mahakamani ingekuwaje? Hakuna kiongozi ambaye angefanya mchezo tena, lakini wao ndio kwanza wanaenda kutucheka wananchi na kebehi kibao kwenye magazeti yao, sasa unategemea wananchi wa kawaida wanaooona haya watafanya nini ni lazima waibe nao mkuu.

Tunahitaji utawala wa haki na kisheria kwanza, the rest will follow.
 
Hatujachelewa sana, tunaweza tukaamka tukiamua. Tunapaswa kuanza kuweka mfumo utakaweka bayana wajibu wa serikali na rai wake. Kwa sasa ni kama vile wananchi wanaamini kwamba serikali inapaswa kuwafanyia kila kitu na serikali nayo inafikiri kwamba haiwezi kufanya lolote bila michango ya wananchi. Matokeo yake: wananchi wanailaumu serikali na serikali inawalaumu wananchi. Palipotakiwa kupeleka hela za kodi hatupeleki, pale ambapo hatukutakiwa tupeleke ndipo tunatupeleka.

Ili tuanze safari yetu ya kujikwamua na madubwana tuliyojitengenezea tunahitaji uongozi. Uongozi hauwezi kuwa huu wa CCM ambao wanasema hata chanzo cha umaskini hawajui. Kwa hiyo tunarudi kulekule, hatua yetu ya kwanza kabisa ya kutoka hapa tulipo ni kuiweka CCM pembeni, tuanze na chama kingine. Sasa tutazunguka weeeeeeee, ukweli unabaki palepale bila kubadilisha chama (mfumo), tutaendelea kucheza mdori na hii forum itajaa malalamiko yetu mpaka ipasuke.

Kwa hiyo basi mada hii inapaswa, pamoja na mambo mengine haya, kujadili:

i) namna ya kuwa-mobilise wananchi waelewe hatari wanayozidi kujitengenezea kwa kuendelea kuichagua CCM

ii) namna ya kuwatia ujasiri wanasiasa wenye mwelekeo, uzalendo na uwezo wa kiuongozi kujiunga na upinzani ili kuimarisha na kuvijenge taswira chanya vyama vya upinzani ikiwa ni njia ya kuviandaa kupambana na CCM na hatimaye kuongoza mabadiliko tunayotaka

Summary: adui wetu hapa ni CCM. Fursa peke tuliyo nayo wa kummaliza huyu adui ni uchaguzi. Silaha yetu hapa ni kura za wananchi. Jemadari wetu ni upinzani. Kazi yetu hapa JF ni kumpa mafunzo huyo jemadari ili aje atuongoze katika kumteketeza adui.

Hii summary yako ni ujumbe kwa wapiga kura, na hilo unalowahabarisha sharti liwafikie na walielewe ili walifanyie kazi.Nakubaliana na wewe kuhusu mobilization.Kama kambi ya jemedari uliyemtaja itasubiri tu kusambaza ujumbe wa namna hii wakati wa kampeni ni dhahiri muda hautatosha.Hapo panahitajika pia support ya JF katika kuueneza ujumbe nchi nzima.
Aidha jemedari umtajaye sharti awe msafi mbele ya wapiga kura.Pengine kama ulivyosema mafunzo watakayopewa au wanayopewa yahusishe pia haja ya watu wotye kambini kuwa wasafi.
Nimedokezwa pia kwamba wananchi wanalalamika vyama vya upinzani viko vingi vinawachanganya,unadhani wanaJF waweke msukumo katika kuunganisha kambi ya upinzani?
 
Summary: adui wetu hapa ni CCM. Fursa peke tuliyo nayo wa kummaliza huyu adui ni uchaguzi. Silaha yetu hapa ni kura za wananchi. Jemadari wetu ni upinzani. Kazi yetu hapa JF ni kumpa mafunzo huyo jemadari ili aje atuongoze katika kumteketeza adui.

Mmhhh! pole pole mkuu, adui wetu hapa ni ukosefu wa utawala bora unaojali sheria, tungekuwa nao basi kuna viongozi wengi kuanzia upinzani mpaka CCM wasinge-qualify kuwa viongozi, matokeo yake ni tumejaza viongozi wengi wasiokuwa na uwezo walionunua uongozi kwa kutumia utawala wetu wa sheria zisizoheshimiwa, na mwisho kulididimiza taifa.

Uchaguzi sio tatizo ni kuheshimu sheria za uchaguzi, viongozi wengi wa pande zote mbili, wamenunua uongozi kwa kuvunja sheria, hivyo nia na lengo lao ni moja nalo ni kuvuruga uchaguzi ili waendelee na ulaji wao wa ruzuku,

Upinzani kutuongoza kutoka kwenye hili tatizo, I do not think so, maana so far tunasikia matatizo yanayofanana fanana betweeen CCM na Upinzani, kwa upinzani tulio nao sasa siuamini kwa sababu so far waneshindwa kuwashawishi wananchi wasiwapigie kura CCM, maana yake ni moja tu kwamba hawaoni kwamba upinzani una anything new to offer, besides, upinzani wenyewe ni Zitto, Dr. Slaaa, Lisssu, Freeman, na Mnyika, Kitila, na Mwanakijiji, sasa tunawapaje taifa letu watu sita tu?
 
Back
Top Bottom