Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Kitila,

Duuuh!... ama kweli tumeumbuka!

kuna sehemu umesema kwamba hizo nchi ni zile zisizokuwa na demokrasia lakini mimi nadhani ni Nchi ambazo bado LIMBUKENI na tumevamia Ubepari bila kujiandaa. Kwa maana hiyo ndoto na life expectation ya wengi imekuwa na marejeo tofauti kabisa! Tunazidi kwisha kila kukicha.

Tukirudi katika mada hii, ndugu zangu nimegundua kuwa tanzania tuitakayo ni kama vile hadithi ya PEPO. Yoote niliyaweka mwanzoni hayana nafasi kabisa kwani Tanzania ni nchi inayokwenda kwa nguvu za Mungu kama mgonjwa wa Ukimwi anayesubiri gonjwa la kumwangusha. uchumi wetu unakua (unene) kwa sababu ya madawa ya vitamin (misaada) kutuweka hai lakini huko ndani white cells zote zinakwisha kila kukicha.
 
Nilikuwa ughaibuni kitambo kidogo na kwanza nimerejea 'nyumbani' hali inasikitisha hasa ukiangalia maendeleo ya kiuchumi,kisiasa na kijamii ya nchi za wenzetu.Nimegundua wao ni binaadamu kama sisi kimaumbile ila tunatofautiana kwa kiasi kikubwa kwenye utashi kwa kujikomboa na kuwa na maendeleo endelevu,nimeweza kung'amua yafuatayo

- Waliopewa dhamana ya kuongoza wengi hawana utashi bali wamegubikwa na ubinafsi katika kuleta maendeleo.

- Hakuna uwajibikaji bali ni kulindana tu, viongozi wetu hawajifunzi kutoka nchi za wenzetu jinsi viongozi wanavyolazimishwa kujiuzulu wakiboronga..nilidhani kujiuzulu kwa raisi wa benki ya dunia kutawasaidia kufikiri vizuri
-

- Watanzania wengi ni wajinga ((kie limu) wanashindwa kufikiri vizuri ni vipi wajikwamue kutoka kwenye makucha haya.
Ili tuwe na maendeleo ya kweli nadhani wananchi wapewe dhamana ya kuamua nchi iendeshwe vipi, lakini hili litafanikiwa ikiwa tu kama Uongozi wajuu utakubali wananchi ndio wawe na mamlaka ya kutaka nchi yao iongozwe vipi!
ahsanteni.
 
Nimekuwa nikitafakari kwa kina hili suala, lakini ninapata utata mkubwa sana kwa maana aliyeshika kwenye mpini ndiye huyo huyo anayetakiwa kujigeuzia makali. Je, tunaweza kuwa na movement ya kulazimisha hili likafanyika?

Ikitokea Bunge letu likawa "shaken" na nguvu za wananchi, nina imani tunaweza kuona mabadiliko mengi katika mustakabali wa nchi yetu.

Nakumbuka baada ya Bunge la sasa hivi kuanza tu vikao vyao (2005), basi wakaja na ajenda ya kujiongezea maslahi. Wananchi tukanung'unika, wakauchuna lakini habari nilizosikia ni kwamba walijiongezea kimya kimya.

Tumeshuhudia jinsi wanavyoikeketa Tanzania bila huruma kupitia Kamati zao mbalimbali.

Tunashuhudia jinsi wanavyojikopesha magari, tena ya kifahari kwa kisingizio cha kwamba ndiyo yanayokabili hali ya barabara zetu. Serikali inawahonga ili wasiipigie kelele pale inapoboronga. Kwa nini wasiyakatae na hapo hapo waibane serikali itengeneze barabara nzuri zinazopitika wakati wote na zitakazowanufaisha wananchi wote?

Kila baada ya miaka mitano ya ubunge, kuna mafao ya uhakika ambayo katika hali ya Tanzania ni mtaji wa kuanzishia angalau biashara ya kuku na ng'ombe wa maziwa (ukawa mjasiriamali).

Na kwa sababu hii kila "Mtazania" kwa sasa anawaza kuingia kwenye "siasa" ili ajaribu bahati (BINGO) yake. Na ndiyo maana tunashuhudia wanamichezo, "wataalam" wetu, waandishi, "wakulima", n.k. wakipigana vikumbo ili kujisafishia njia ya kuukwaa ulaji huu!!

Wakati huo huo yule mfanyakazi wa serikali, aliyeitumikia nchi yake kwa "uaminifu" mkubwa na kwa muda wa zaidi ya miaka 30 anaachwa akitaabikia mafao yake (tena ambayo amekuwa akichangia kila mwisho wa mwezi) hadi anakufa bila "haki" yake kuipata. Madhara yake ni makubwa na ni funzo zito kwa wanaobaki nyuma yake, maana itabidi wachukue chao mapema yasijewakuta ya mwenzao. "Mwenzio akinyolewa, zako weka maji". Na huo ndiyo mwanzo wa ubadhirifu na hujuma tunayoishuhudia leo hii.

Je, tunaweza kuwa na civic pressure ya kuondoa mafao haya ya kisiasa?

Tujadili ....
 
Nilikuwa ughaibuni kitambo kidogo na kwanza nimerejea 'nyumbani' hali inasikitisha hasa ukiangalia maendeleo ya kiuchumi,kisiasa na kijamii ya nchi za wenzetu.Nimegundua wao ni binaadamu kama sisi kimaumbile ila tunatofautiana kwa kiasi kikubwa kwenye utashi kwa kujikomboa na kuwa na maendeleo endelevu,nimeweza kung'amua yafuatayo

- Waliopewa dhamana ya kuongoza wengi hawana utashi bali wamegubikwa na ubinafsi katika kuleta maendeleo.

- Hakuna uwajibikaji bali ni kulindana tu, viongozi wetu hawajifunzi kutoka nchi za wenzetu jinsi viongozi wanavyolazimishwa kujiuzulu wakiboronga..nilidhani kujiuzulu kwa raisi wa benki ya dunia kutawasaidia kufikiri vizuri
-

- Watanzania wengi ni wajinga ((kie limu) wanashindwa kufikiri vizuri ni vipi wajikwamue kutoka kwenye makucha haya.Ili tuwe na maendeleo ya kweli nadhani wananchi wapewe dhamana ya kuamua nchi iendeshwe vipi, lakini hili litafanikiwa ikiwa tu kama Uongozi wajuu utakubali wananchi ndio wawe na mamlaka ya kutaka nchi yao iongozwe vipi!
ahsanteni.

Sijui ni kwa nini kila tunapoona mambo hayendi vizuri katika nchi yetu tunahitimisha kwa kusema kwamba watanzania wengi ni wajinga? Hakuna ukweli katika hili, isipokuwa tu kwa vile tungependa kila mmoja akubaliane na mawazo yetu. Kitu ambacho hakiwezekani kwa mara moja.

Nitakupa mfano mmoja hai: Jimbo la Muleba Kaskazini mbunge wake alikuwa Tegambwage (1995-2000) na tuliwaona wananchi wa Jimbo hilo wana-"elimu" kwa vile wamebadilisha chama (labda na mtu, sijui). 2000-pesent, wakairudisha CCM (Msafiri, Ruth), basi wakawa hawana "elimu" kwa vigezo hivyo hivyo .... na mifano hii ni mingi sana. Sasa sijui inakuwaje hapo? Watanzania ni werevu sana, na wakishagundua kwamba ni "wale wale", then why should they bother?

Lakini, mantiki yangu ni hii: Waache wananchi wachague kiongzi wamtakaye kulingana na jinsi alivyoweza kuuza sera zake kwao na bila kutumia ushawishi mwingine wa rushwa ama vitisho. Kutokuchaguliwa kwa mtu uliyemtaka, kisiwe kigezo cha kuwahukumu wananchi kwamba hawana elimu. Kwa maana hata nawe mwenyewe ukija uchaguzi utamchagua mtu unayemwona anafaa, na itakuwa siri yako. Na hapo ndipo tunapojichanganya kwa kutegemea umati wa watu unaohudhuria mikutano ya kampeni kwamba ndiyo kiashirio cha kura utakazozipata ... wrong!

Nchi yetu inaharibiwa na siasa .... sasa kwa kuwa nawe umeuona mfumo wetu ulivoharibika, usije kushawishika kuingia kwenye siasa ili "unufaike" kwa kupitia migongo ya watanzania "wajinga (kielimu)" .... tunakuhitaji katika kubadilisha hali ya nchi na kuuweka mustakabali wa nchi katika mstari ambao hata vizazi vijavyo "havitatulaani" kama ambavyo "tunalaani".

Kingine, siyo lazima mapambano yahusishe watanzania wote. Tunaweza kuanza na makundi mbalimbali, e.g. wafanyakazi, wanafunzi na some other pressure groups! Lengo likiwa ni kuiweka siasa katika mahali pake.
 
Ilongo,

Utaumiza kichwa chako sana pasipo jawabu!
Binafsi mwanzo nilikuwa nikifikiria sana kuhusu wananchi kuli-shake Bunge na hata kuna wakati nimekubali kuwa labda wapinzani wajaribu maandalizi ya kuwa na wawakilishi wengi Bungeni, lakini mjomba nimegundua kuwa tatizo letu liko deep sana zaidi ya Bunge.
Ikiwa waziri mmoja tu anaweza kusimama Bungeni na kusema swala fulani halihusiani na Bunge ama Bunge halina mamlaka ya kupitia Mikataba ama kuitisha uchunguzi fulani mahala ambapo wameona kuwa sheria imepindwa! well hapa tuna tatizo kubwa.

Kusema kweli sioni kabisa mbele zaidi ya kujiuliza hivi kazi ya Bunge ni kitu gani?.. hata kama iwe utunzi wa sheria, je watawezaje kutunga sheria mahala ambapo hawaruhusiwi kutazama chanzo cha maovu?..ati sii kazi yao! sasa tunahitaji bunge la nini?
Je, kesho wapinzani wakichukua Bunge hivi kweli tunategemea kutakuwepo na mabadiliko iwapo leo hii Bunge ni chombo chini ya maamuzi ya serikali na sii kazi yao kupitia, kutazama matatizo na kutoa uamuzi kisheria unaoiwezesha serikali na watu wake kufanya kazi?

Zaidi ya yote haya, nina mashaka sana ktk utekelezaji wa serikali ambayo bunge zima lina wapinzani lakini nafasi ya Mtawala (RAIS) imeshikwa na chama tawala!.. hapa uundaji wa serikali utakuwa vipi ikiwa serikali leo hii ina madaraka makubwa kuliko Bunge..Je, huyu rais na serikali yake watawajibishwa vipi na Bunge ambalo halina nguvu wala mamlaka ya kumwajibisha rais na mawaziri wake!...

Humu ndani ya JF kuna mada nyingi sana zinazotupa picha mbaya sana ya Katiba ya nchi yetu na sielewi ni kipi kinachotakiwa kuwepo ili Katiba iweze kutungwa UPYA!.. majuzi tu kuna waziri kasema nje ya bunge kwa uhakika kuwa Katiba haiwezi kubadilika.... na kweli hiyo ndio IMETOKA!...sheria imewekwa na mtu mmoja tu kuondoa muswada bungeni!..Ebu nambie tutafika?
 
Mkandara,

Nimekupata mkuu. Nimejaribu kuiweka hii mada ili kuangalia siasa yetu na maslahi manono yaliyomo na jinsi yanavyoathiri mustakabali wa Tanzania na Watanzania.

Hoja yako inahitaji umakini mkubwa kuijibu. Nitarudi baadae ...
 
Nilivyokariri kama wananchi ni wajinga na uongozi wajuu lazima uwe tayari kufanya ujinga huu wa wananchi uondoke ili kuleta maendelo ya kweli ni wazi. Jana tu katibu mkuu wa CCM Luteni mstaafu Makamba akijibu hoja kama katika kinyanganyiro kwenye chaguzi za NEC ya CCM tayari harufu ya Rushwa imeshaanza kutawala na akasisistiza kama lazima wanaojihusisha na Rushwa wabainishwe...huu ndo ujinga nilioumaanisha na wananchi lazima wajengwe kifikra kama pesa,fulana,kofia,kanga,pilau nk zisiwe ushawishi wa kuchagua viongozi badala ya uwezo na utashi hasa wa kuleta mabadiliko. Wanzanchi walio wengi bado hawajaelemishwa haya, na nathubutu kuuita ujinga wa wananchi waliowengi.
Je kuna utashi wa kutosha kuwafanya wananchi waondokane na ujinga huu au waachwe tu walale?
 
Nilivyokariri kama wananchi ni wajinga na uongozi wajuu lazima uwe tayari kufanya ujinga huu wa wananchi uondoke ili kuleta maendelo ya kweli ni wazi. Jana tu katibu mkuu wa CCM Luteni mstaafu Makamba akijibu hoja kama katika kinyanganyiro kwenye chaguzi za NEC ya CCM tayari harufu ya Rushwa imeshaanza kutawala na akasisistiza kama lazima wanaojihusisha na Rushwa wabainishwe...huu ndo ujinga nilioumaanisha na wananchi lazima wajengwe kifikra kama pesa,fulana,kofia,kanga,pilau nk zisiwe ushawishi wa kuchagua viongozi badala ya uwezo na utashi hasa wa kuleta mabadiliko. Wanzanchi walio wengi bado hawajaelemishwa haya, na nathubutu kuuita ujinga wa wananchi waliowengi.
Je kuna utashi wa kutosha kuwafanya wananchi waondokane na ujinga huu au waachwe tu walale?

Nadhani ni zaidi ya hayo uliyoainisha ... Kimsingi ushawishi mkubwa unaoweza kuleta mabadiliko ni kuwahamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukabiliana na matatizo ya msingi kama njaa, malazi na maradhi. Vitu ambavyo wakishakuwa na uwezo wa kukabiliana navyo na wakajihakikishia hivyo, basi hakuna mwanasiasa atakayejitapa kwavyo kwamba yeye atawasaidia kuondokana na madhila hayo.

Mkulima azalishe zaidi ya anachohitaji kwa ajili ya kuilisha familia yake, mfugaji afuge kwa mantiki hiyo hiyo, mjasiriamali vivyo hivyo. Na wafanye hivyo kwa malengo ya muda mrefu wakijua kwamba hakuna njia ya mkato katika hilo. Tusichanganye mambo ya msingi na hizi siasa.

Hivi unadhani mtu ambaye ameshinda njaa na kulala njaa utamlisha maneno matupu atakuelewa? Na hicho ndiyo kigezo wanachotumia wanasiasa hapa nyumbani katika kuwalaghai wananchi.

Hauwezi ukasimama ukawaahidi wananchi kwamba utawaondolea njaa bila kuwaeleza ukweli kwamba wasipojibidisha katika kazi zao wataangamia. Waambie ukweli ili hata kama hawakusikiliza leo, kesho watakukumbuka.

Sasa badala ya kuwaelimisha wananchi wajibu wao, tunatumia matatizo waliyo nayo (tena yaliyo mengi yako within their reach to rectify) kutafuta madaraka ya kisiasa.

CUF walipozindua kampeni zao pale Tabora (2005) walimwaga kila kitu: fulana, kofia, pilau, etc na sera nzuri juu. Lakini, je walipata hata mbunge mmoja pale au angalau hata diwani!!

Hapa Dar es Salaam tuliwahi kuwa na wabunge watatu kutoka upinzani kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 1995 na 2005 (Ubungo-Lamwai, Temeke-Mrema, Kigamboni-Magoba). Leo hii hata diwani mmoja hatuna. Ni fulana, pilau, pesa na kofia? No. It's more than that. Hizi sababu zitaendelea kutolewa na kamwe hazitasaidia chochote. Ingekuwa inawezekana ukajua kura ipi ilitoka kwa nani, ungeshangaa kugundua kwamba asilimia kubwa ya wanaovaa hizo kofia, fulana na kula pilau wala hata kujiandikisha kwenyewe hawajiandikishi. Wanatumika kama "mabango" ya kuwatangaza wagombea. Hilo ni kundi la kwanza.

Kuna kundi la pili linalovaa hivyo vitu, lakini wala siyo kwa sababu ya njaa (au kukosa mavazi), isipokuwa ni wanachama wa chama husika na aidha wananunua kwa pesa yao ama wanapewa katika mgao wa matawi yao ili waweze kujitambulisha katika jamii wako upande gani. Nao wanatumika kama mambango ya matangazo katika kampeni. Mifano ni mingi tu CCM wanazo, CHADEMA wanazo (tena zile za wazee wa kazi kabisa, jeshi mgambo), CUF, etc.

Watanzania tunachohitaji ni kubadilika. It's time for change. Achaneni na siasa; face the reality. Kila mmoja awajibike kwa nafasi yake. Uki-toil na ukala kwa jasho lako halali, utakuwa mkali hata kwa yule anayetaka kukuchezea akili eti atakumalizia matatizo yako uliyo nayo endapo utampa kura yako.

Kuhusu rushwa: Tunapiga kelele kwamba Rais ataje majina aliyo nayo ya wala rushwa na tunashangaa kwa nini hataki kufanya hivyo? Na mimi binafsi nitashangaa sana mwandishi wa habari atakapoandika kwamba fulani (jina tunalo) ametoa rushwa ya pilau, pombe n.k. ili achaguliwe. Kwa nini "jina tunalo"? Taja. Vinginevyo hakuna haja ya kuindika hiyo habari. Hainisaidii mimi mwananchi wa kawaida. Naiona kama ni usanii wa vyombo vya habari kuuza gazeti. Zama hizi tulizo nazo siyo tena za "jina tunalo". Taja ni fulani na alifanya hivyo sehemu fulani ili jamii imjue. Waumbue. Mnaficha nini?
 
Mada nzuri sana hii; nitairudia baadaye nikipata muda wa kutosha kwa vile hii mada ni analytical, inahitaji mawazo yaliyopangiliwa.
 
Ilongo,
Hilo la rushwa nakubaliana na wewe kabisa. Muda umewadia kwa vyombo vya habari kutoboa jinsi mambo yalivyo, si kuhifadhi majina ya wahusika.
 
YANGU MACHO kwani kama rais mwenyewe anawaogopa hao wala rushwa ni mwandishi yupi ataweza kuwataja?

Ni mwandishi yupi huyo ilihali huwa anapanda daladala na hana ulinzi wowote mwenye uwezo wa kuwataja waziwazi?kama rais mwenye ulinzi wote anasema wajirekebishe hii maana yake ni kuwa hawa watu ni WAKUMBWA.
 
YANGU MACHO kwani kama rais mwenyewe anawaogopa hao wala rushwa ni mwandishi yupi ataweza kuwataja?

Ni mwandishi yupi huyo ilihali huwa anapanda daladala na hana ulinzi wowote mwenye uwezo wa kuwataja waziwazi?kama rais mwenye ulinzi wote anasema wajirekebishe hii maana yake ni kuwa hawa watu ni WAKUMBWA.

Kuna haja gani ya kuniandikia fulani ("jina tunalo") katoa rushwa? Itanisaidia nini? Kwa maana nyingine ni kwamba aidha kitu tunachokipigia kelele kwamba ni "rushwa" hakipo ila tunajaribu kutafuta pa kutokea au tumeamua kuihalalisha kwa vile inatuingizia kipato (hata kwa kupamba magazeti yetu ili yapate soko la haraka).

Mapambano dhidi ya rushwa inabidi yawe ya wazi. Iwapo viongozi wetu wameamua kukaa kimya, isiwe sababu ya sisi kutokuchukua hatua. Nilitegemea katika hili, waandishi wangetusaidia pale wanapogundua kuna tatizo, then watoe taarifa kwa mamlaka husika kama vile tunavyotoa taarifa za wahalifu wengine (kama majambazi, vibaka) ama majanga mbalimbali (kama moto, ajali za baharini na nchi kavu) ili pale wahusika watakaposhindwa kutekeleza majukumu yao, basi hata mimi mwananchi nitawaelewa. Lakini fulani "jina tunalo" katoa rushwa ya pilau, etc. end of the story. So what? Nadhani uandishi wa habari ni zaidi ya hilo. Sishangai kwa maana ndiyo Tanzania.

Rushwa kama hii ambayo imeelezewa hapa (ya kuwapa watu chakula, pombe etc) sidhani kama ilikuwa ni ngumu sana kuifanyia kazi. Vinginevyo, nitashindwa kujizuia kuamini kwamba ni katika mwendelezo wa kuchafua tu majina ya watu almradi mkono uende kinywani.
 
Ndugu yangu Ilongo mamlaka husika ndio hao PCB ambao juzi tuu umewasikia wakisema RICHMOND hapakuwa na rushwa ila palikuwa na uzembe je?huo uzembe unasababishwa na kitu gani kama siyo kupewa ten percent?

Kama ile timu yenye watu wazito kama katibu mkuu wa hazina,mwanasheria mkuu na wengineo ni wazembe unategemea mwandishi akaiambie mamlaka gani?

Tufikiri upya juu ya hatma ya taifa hil haitoshi kuwalaumu waandishi kwani vyombo vyenyewe vya kushighulikia rushwa havipo.
 
M K.

Kimsingi nakubaliana na wewe.
Nchi imekwama: Nakubali.
Taifa limekuwa la vipofu (kwa maana ipi?), isije tukawa tunanyanyapaa!
Tuache kuwa kondoo: Nakubali. Na ndiyo maana nasema, aidha tupe jina ama hiyo habari yako (mwandishi) au endelea kukaa nayo chumbani kwako.

Lakini kwangu mimi, bado zote zinabaki kuwa dhana tu ... tunavyo visingizio vingi na ndiyo maana hatuwezi kujikwamua tulipokwama.

Na kama haiwezekani kuwataja wala rushwa, basi tutakuwa wanafiki pale tunaposema "kijiko kiitwe kijiko" wakati wala rushwa (na watenda maovu wengine) tunawaita "jina tunalo".
 
Ilongo,

Utaumiza kichwa chako sana pasipo jawabu!
Binafsi mwanzo nilikuwa nikifikiria sana kuhusu wananchi kuli-shake Bunge na hata kuna wakati nimekubali kuwa labda wapinzani wajaribu maandalizi ya kuwa na wawakilishi wengi Bungeni, lakini mjomba nimegundua kuwa tatizo letu liko deep sana zaidi ya Bunge.
Ikiwa waziri mmoja tu anaweza kusimama Bungeni na kusema swala fulani halihusiani na Bunge ama Bunge halina mamlaka ya kupitia Mikataba ama kuitisha uchunguzi fulani mahala ambapo wameona kuwa sheria imepindwa! well hapa tuna tatizo kubwa.

Kusema kweli sioni kabisa mbele zaidi ya kujiuliza hivi kazi ya Bunge ni kitu gani?.. hata kama iwe utunzi wa sheria, je watawezaje kutunga sheria mahala ambapo hawaruhusiwi kutazama chanzo cha maovu?..ati sii kazi yao! sasa tunahitaji bunge la nini?
Je, kesho wapinzani wakichukua Bunge hivi kweli tunategemea kutakuwepo na mabadiliko iwapo leo hii Bunge ni chombo chini ya maamuzi ya serikali na sii kazi yao kupitia, kutazama matatizo na kutoa uamuzi kisheria unaoiwezesha serikali na watu wake kufanya kazi?

Zaidi ya yote haya, nina mashaka sana ktk utekelezaji wa serikali ambayo bunge zima lina wapinzani lakini nafasi ya Mtawala (RAIS) imeshikwa na chama tawala!.. hapa uundaji wa serikali utakuwa vipi ikiwa serikali leo hii ina madaraka makubwa kuliko Bunge..Je, huyu rais na serikali yake watawajibishwa vipi na Bunge ambalo halina nguvu wala mamlaka ya kumwajibisha rais na mawaziri wake!...

Humu ndani ya JF kuna mada nyingi sana zinazotupa picha mbaya sana ya Katiba ya nchi yetu na sielewi ni kipi kinachotakiwa kuwepo ili Katiba iweze kutungwa UPYA!.. majuzi tu kuna waziri kasema nje ya bunge kwa uhakika kuwa Katiba haiwezi kubadilika.... na kweli hiyo ndio IMETOKA!...sheria imewekwa na mtu mmoja tu kuondoa muswada bungeni!..Ebu nambie tutafika?

Mkandara,

Ukimwuliza mtu yeyote anayegombea uongozi wa kisiasa, awe wa CCM au chama kingine chochote kile, nia yake hasa nini: Jibu ni rahisi sana. Ataorodhesha matatizo lukuki waliyo nayo watanzania yakiongozwa na umaskini, njaa, na maradhi.

Je, una mikakati gani ukishapata hiyo nafasi ya kisiasa unayogombea? Jibu: Nitapambana na hayo matatizo ili kuyatokomeza ...

Utatumia njia zipi? Jibu: (eenh eenh). Ni nadra sana kupata jibu hapa. Utapigwa blah blah blah nyingi hadi uchoke mwenyewe.

Hiyo ni kwa ufupi tu. Lakini, hilo wala halijawahi kunikatisha tamaa ya kutokwenda kupiga kura. Labda ipo siku kura italeta majibu sahihi.

Kwa hiyo Bunge linaweza likawa chini ya upinzani, lakini bado likashindwa kutimiza wajibu wake iwapo walio wengi waliingia humo kwa kujali maslahi yao binafsi (na hasa kiinua mgongo cha miaka mitano). Na huo kwangu mimi ndiyo ugomvi wangu mkubwa. Kwa nini siasa ambazo kimsingi hazizalishi, isipokuwa kufilisi nchi, tunazilipa kiasi hicho?

Kwa mantiki hiyo hiyo, Bunge halitaweza kupiga kura ya kuiondoa serikali madarakani iwapo asilimia kubwa ya waliomo wanaangalia "nisije nikapoteza mafao yangu". Maana Rais naye akikasirishwa na kitendo cha kuipigia kura sekali yake, akatumia mamlaka yake kikatiba anaweza kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi upya. Sasa siyo wote watakuwa na uhakika wa kurudi. Na hapo ndipo linakuja hilo suala lako la Katiba.

Serikali imelihonga Bunge(kwa kuwalipa mafao manono) ili lisitekeleze kazi zake; pia serikali kupitia Bunge hilo hilo ikavionga vyama vya siasa vyenye wabunge, ili visitekeleze wajibu wake. Hizi ruzuku za mamilioni kwa chama cha siasa chenye mbunge (na mwakilishi, I'm not sure), ni hongo kwa viongozi wa vyama vya siasa. Halafu wao hawaoni kwamba huo ni uchafu, wanaushabikia!! Ni mojawapo ya chanzo chao cha mapato binafsi.

Lakini bado nina dukuduku langu ambalo hasa ndilo limenisukuma: Je, tunaweza kufanya lolote la kushinikiza Bunge liwajibike? Kwa maana kama haliwezi kuyafanya hayo ambayo tulitegemea litusaidie kuibana serikali, basi kuna haja gani ya kuwepo kwake?
 
Ilongo
Nazidi kukupongeza kwa jitihada zako za kuzidi kutetea kwa kujichaganya. Ila ninazidi kupata wasiwasi wakutushauri tujisihusishe na siasa na tuendelee na uliyotaja kama shughuli mbalimbali, km kilimo, nk. Ndugu yangu lazima tuwe na interest ya kutaka kujua mchakato wa wanasiasa na kuingia kwao madarakani. Kwani hawa ndo wapangaji wa sera hizo za kiuchumi, ulizozitaja. Ikiwa tuna wanasiasa wanaoingia kwa rushwa unadhani hata hizo shughuli zote ulizozitaja za kujiletea maendeleo zitafanikiwa?Chukulia mfano, kiongozi huyu mla rushwa hatakomea hapa..anaweza pia kujihusiasha na mikataba ya rushwa kwa lengo lile lile eti la kutaka kuleta maendeleo.

Ujinga wa wananchi ni dhambi kutumika na kundi lolote lile la kisiasa, nimefurahi mfano ulioutoa kuhusu CUF kama iliwalisha watu pilau kule Tabora na kuwavisha,fulana,nk. Kama walifanya hivi kwa lengo la kuwarubuni wapiga kura lazima itakuwa ni dhambi kubwa, labda huenda gharama yake waliopata ndio hiyo ya kukosa hata mbunge mmoja bara, yawezekana pia kama walishindana na waliotoa pilau nyingi zaidi, ikawa mwenye kisu kikali ndio mla nyama. Ushauri wangu ni uleule na kama alivyokaririwa kutamka hayati mwalimu, Rushwa ni adui wa haki.

Nikisema kama wananchi wapewe majukumu ya kutaka nchi yao iongozwe vipi ni muhimu. Ikiwa wananchi watawezeshwa hivi, wanasisiasa kamwe hawatothubutu kuendelea kuboronga kwani wanafahamu fika kama gharama yake ni kubwa. Tanzania ya leo dhati hii ya kutaka wananchi waamue nchi iongozwe vipi ina walakini mkubwa. Miongoni mwa sababu kubwa ni hili la kukosa elimu ya uraia na kukomaa kwa rushwa.
 
Ka nchi kananuka sana.
By Nthelezi Nesaa | Published Today | Nthelezi Nesaa | Unrated
Na HabariTanzania.com
Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kutamka maneno hayo hapo juu mwishoni mwa miaka ya 90 wakati wa awamu ya pili iliyoongozwa na shehe Ali Hassan Mwinyi maarufu kama mzee Ruxa.

Mwalimu aliyasema hayo kwa hasira na mfadhaiko baada ya kuwa vinaripotiwa visa vya wizi,ujambazi na kila aina ya ufisadi serikalini na Mwinyi asichukue hatua. Baya zaidi wakati ule safu hii inakumbuka, kiunganishi kikuu, kwa mujibu wa tuhuma za wakati ule, ilikuwa ni ikulu yenyewe ambapo bi mkubwa alituhumiwa kutumiwa na marafiki zake na wafanyabiashara wachafu kuliibia taifa.

Bahati nzuri wakati ule waswahili walikuwa hawajazoea pesa. Maana malalamiko yalituama juu ya kupata vidala dala kadhaa na viwanja vya nyumba. Mwalimu kama ada hakuacha kusema. Alizidi kumuonya Mwinyi mpaka wapambe wa Mwinyi wakasema Mwalimu alikuwa anamuonea wivu Mwinyi kwa maendeleo aliyokuwa amefikia. Wenye akili walijiuliza Mwalimu angemuonea wivu Mwinyi kwa lipi iwapo ndiye aliamua kwa makusudi kumuachia nchi.

Wakati ule Mwalimu alikuja na kombora jingine. Baada ya kuona wafanyabiashara wa kihindi wameigeuza ikulu kijiwe cha kufanyia dili, Mwalimu alisema “Ikulu siyo sehemu ya kufanyia biashara…………… patakatifu pa patakatifu”


Tufupishe simulizi tuje kwenye mantiki ya maneno ya gwiji huyu. Je hali ya nchi yetu kwa sasa ikoje? Kusema ukweli inanuka kuliko wakati wa Mwinyi. Kama ni harufu basi wakati wa Mwinyi ulikuwa mchafuko mdogo wa tumbo kuliko huu uoza wa mwili mzima.

Tutatoa sababu. Nani anaweza kubisha kuwa kwa sasa nchi yetu inakabiliwa na kashfa nyingi tena kubwa ambazo kwa bahati mbaya wakubwa wanazifutika chini ya busati. Tukumbushane. Ilianza kashfa ya rada, ndege,Richmond, BOT, sasa tunasikia na Bwana mkubwa na bibi yake mpenda pesa walikuwa wakifanyia biashara patakatifu pa patakatifu chini ya jahazi liitwalo ANBEN!

Kinachoumiza zaidi ni kwamba waliofanya uchafu huu ni wale wale waliofikishwa patakatifu pa patakatifu na Mwalimu mwenyewe! Kama ni usaliti basi huu ni mchafu kuliko hata ule wa Yesu na ndugu yake Yuda. Awamu ya tatu na inavyoonekana ya nne, ni awamu zitakazoingia kwenye historia kama awamu ya maanguko makubwa ya taifa letu.
Tutatoa sababu. Awamu ya kwanza maarufu kama ya ubinafsishaji, ilifanya kazi ya kuuza mali za umma kwa bei ya kutia mashaka wengine husema karibu na bure au tajiri kalewa. Baya zaidi wakati wananchi walipojaribu kuisaidia kwa kuionya hivyo sivyo walijibiwa kwa nyodo na matusi kibao!

Awamu ya tatu iliasisi urafiki na kujuana kutumika kama vigezo vya kuteuana. Hatuichukii au kuitwisha lawama kwa vile imeishafutika. Hasha. Nani alijua sababu za mtu aliyekuwa hafai kwenye cheo cha uwaziri mkuu kama waziri mkuu mstaafu kukalia kiti hicho pamoja na shutuma kwa miaka kumi? Sababu zilikuwa wazi kuwa alikuwa anafahamiana na Rais na isitoshe wake zao walikuwa wakitoka kabila moja. Huu ni upuuzi kiasi gani.

Ukiachana na kuteuana kwa kujuana, awamu ya tatu iliasisi mchezo unaoanza kuota mizizi wa kutawala kwa maneno badala ya vitendo. Mkapa alizoea kuiita awamu yake ya ukweli na uwazi wakati kimatendo ilikuwa ni uongo na ufichi. Rejea uongo wa mchana wa Mkapa kwenye mradi wa wakubwa wa kununua rada ambayo imetokea kuwa kashfa na donda kwa wananchi. Rejea ununuzi wa ndege mbovu lakini aghali ya Rais.

Sasa tuangalia hali ya sasa. Kwanza hakuna ubishi kuwa tangu awamu ya nne iingie imeingia na kashfa na kimtindo. Kwanza wakubwa hawakutangaza mali zao angalau tuweze kulinganisha wapi wameongeza na kwa nini na wapi wamepunguza ingawa kwa nchi ya bwerere kama Tanzania kupunguza hakupo.

Rejea kashfa ya Richmond ambayo pamoja na kuja na viini macho vya Taasisi ya Kukuza Rushwa ( TAKURU), bado watanzania wanajua kuwa wakubwa tena walioko kwenye ulaji mkubwa walivuta chao na kutuachia hilo shipa ambalo hata sasa hakuna anayejua kinachoendelea. Wao badala ya kutusuta na kutudanganya kama alivyokuwa akifanya Mkapa wameamua kuja na mtindo wa kuunda uchunguzi kiini macho na kusafishana!

Ukiachia Richmond, ANBEN, WAMA, EOTFL, kuna kashfa ya upotevu wa matrilioni kwenye wizara mbali mbali na hakuna mtu hata mmoja aliyekwishafikishwa mahakamani. Pia kuna hili baba lao la Benki kuu (BOT) ambapo vyombo vya habari vinasema kuwa ni kuanzia dola milioni 130 hadi 800 milioni! Jamani kwa ka nchi kama haka maskini hii siyo pesa ndogo. Lakini pamoja na ukubwa wa pesa hii nani anajali?

Maana kwa taarifa toka bungeni,serikali ilitaka hata kuwazuia wabunge wasijadili wizi huu? Hapa kwanini ka nchi kasinuke tena sana sana?

Kuna sakata la wakubwa kuuziana nyumba za watu wasio na nyumba. Nani anajali kutoa majibu? Hapa kwanini ka nchi kasinuke?

Kuna hili baba lao jingine. Madawa ya kulevya. Watu mbali mbali wamemtaka Rais aweke wazi kama anayo majina ya vigogo wa mihadharati awataje na kama hana aseme. Lakini mtukufu kaamua kuuminya! Juzi juzi alipokufa Amina Chifupa ambaye inasemekana alikuwa akipambana na madawa hayo, ndipo tunasikia tena nadhiri mpya! Hapa kwanini ka nchi kasinuke? Mpaka watu wenu waanze kufa ndipo mtasikia na kufanya mambo ya maana badala ya "rongo rongo" uchwara!

Ukirejea kwenye kupeana vyeo, hapo ndipo utashika kichwa na kujiinamia kama umepigwa ngumi ya tumbo. Nani mtu mwenye akili alitegemea mtu kama Lowassa anayejulikana kwa tamaa zake angekuwa waziri mkuu wa nchi? Ama kweli Kikwte kajua kutuchoka na kututumia!

Serikali licha ya kuwa kubwa, imejaa marafiki na watu wenye rekodi mbaya sana za kila aina ya ujambazi kwenye ofisi za umma.. Safu hii siyo ya kwanza kuliongelea suala hili. Hili limegeuka wimbo kutaka serikali ipunguzwe. Nani anasikia? Kwanini ka nchi kasinuke?

Kwa machache hayo katika mengi, tuhitimishe kusema kuwa nchi yetu isiposafishwa itaoza na kumong’onyoka na kupotea. Viongozi waanze kujenga utamaduni wa kuwasikiliza wananchi badala ya kuwaburuza na kuendelea kufanya makosa. Wahusika watoe majibu yenye mantiki tena kwa wakati badala ya kunyamaza. Maana hilo siyo jibu. Nchi yetu inanuka sana sasa. Kila tunapobadili uongozi tunazidi kuzama je ni kwanini?

Nchi imeanza kukosa hata maana. Wakati wakubwa wanashindana kuchuma na wageni hasa wa kihindi nao hawako nyuma. Wako nyuma yao. Maana kila uchafu unaofanyika serikalini nyuma yake lazima wawepo wahindi. Kwanini? Je wananchi wetu wataendelea kuwa mashahidi wa jinai hii. Chonde chonde ka nchi kananuka sana. Wahusika safisheni ka nchi. Na patakatifu pa patakatifu pasigeuzwe patakakitu pa patakakitu.
Tuonane wiki ijayo inshallah.
 
kwa kifupi ni kuwa hali ilivyo tanzania ni time bomb.
 
Kweli inanuka- ila naona ni too generealised ikapindia sana upende mmoja! ila jamani yaani kwa miaka yote hii tusiwe na kitu (let alone ushindi wetu Burkinafaso!) cho kujipa moyo?
Nimekuwa naangalia Transparancy International -Report 2006, Corruption, Tz ranked 98 kati ya nchi 180. Wenzetu Rwanda 128 na Kenya 144. South Afrika wenyewe afadhali 51 na pia Namibya 56.
Kumbe kuna wengine wanatuona tuna uafadhali katika kuoza kwetu? Tahadhari- sikiwango chetu ya uozo- uozo ni uozo Tu!
http://www.infoplease.com/ipa/A0781359.html
 
Back
Top Bottom