Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Mzee MMJ,

Heshima mbele mkuu, lakini kwenye hili hauko sawa Tanzania tuna political system kama ya UK na pia US, nayo ni the winner takes all, na hiyo system ilizaliwa pale Ikulu mwaka 1990, siku viongozi wa CCM na Upinzani walipotia sahihi mkataba wa kuanzishwa kwa system ya siasa ya vyama vingi Tanzania, na moja ya vipengele vya makubaliano hayo ambayo yalikubaliwa baada ya mikutano mirefu na mingi, kati ya CCM na upinzani ni kuwa na system ya winner takes all ambayo tunayo sasa hivi, sasa sielewi exactly unatokea wapi na hii hoja ya kuwajumusha kina Lipumba kwenye serikali ya CCM?

Kwa kuongeza tu, labda ungemtaja msomi mwingine wa upinzani, lakini Lipumba, Seif, na Mrema walishawahi kuwa viongozi wa juu wa CCM, ni kitu gani hawakukifanya then watakifanya leo tofauti?

Lipumba aliwahi kuwa mshauri wa uchumi wa rais wa awamu ya tatu, rais Mwinyi, je uchumi ulikuwa bora then than now?

Katika demokrasia tulinayo Tanzania leo, kuna njia moja tu ya kupata madaraka, nayo ni kushinda uchaguzi kwa kura nyingi kuliko vyama vingine, hakuna short cut, au njia ya mkato ambayo unaoenkana kujaribu kuipendekeza kwa taif letu.

Ahsante Mzee!
 
Kulikoni,'
Hivi unajua kwa nini Wassira alirudi CCM? Alikuwa na biashara zake za samaki na kila kona akiwekewa mikwara. Nusura afilisike. Amerudi CCM mambo yake yamemnyookea.
 
Mzee MMJ,

Heshima mbele mkuu, lakini kwenye hili hauko sawa Tanzania tuna political system kama ya UK na pia US, nayo ni the winner takes all, na hiyo system ilizaliwa pale Ikulu mwaka 1990, siku viongozi wa CCM na Upinzani walipotia sahihi mkataba wa kuanzishwa kwa system ya siasa ya vyama vingi Tanzania, na moja ya vipengele vya makubaliano hayo ambayo yalikubaliwa baada ya mikutano mirefu na mingi, kati ya CCM na upinzani ni kuwa na system ya winner takes all ambayo tunayo sasa hivi, sasa sielewi exactly unatokea wapi na hii hoja ya kuwajumusha kina Lipumba kwenye serikali ya CCM?

Kwa kuongeza tu, labda ungemtaja msomi mwingine wa upinzani, lakini Lipumba, Seif, na Mrema walishawahi kuwa viongozi wa juu wa CCM, ni kitu gani hawakukifanya then watakifanya leo tofauti?

Lipumba aliwahi kuwa mshauri wa uchumi wa rais wa awamu ya tatu, rais Mwinyi, je uchumi ulikuwa bora then than now?

Katika demokrasia tulinayo Tanzania leo, kuna njia moja tu ya kupata madaraka, nayo ni kushinda uchaguzi kwa kura nyingi kuliko vyama vingine, hakuna short cut, au njia ya mkato ambayo unaoenkana kujaribu kuipendekeza kwa taif letu.

Ahsante Mzee!

Mzee Es
Kuhusu winner takes all system tunayoifuata, swali ni kama inatufaa. Mimi naona kama uwanja wa siasa hapo Bongo unafanana kidogo na ule wa huku Scandinavia. Yaani vyama vingi vidogo vidogo; na kikubwa labda kimoja. Ushindi(lower limit) huamuliwa kwa asilimia. Wakati huko kwa watawala wa dunia hii, piga ua vyama vikubwa ni viwili tu. Wengine ni wasindikizaji by all standards.

Hiyo itakuwa ni sehemu tu ya mabadiliko ya katiba ambayo mimi naamini ni muhimu kwa demokrasia ya Tz.
 
Mzee Invincible,

Unajua kuwa siku zote heshima mbele mkuu, kama ninakuelewa vizuri and I could be wrong,

Tunahitaji mabadiliko ya katiba, labda hii thread ingesema hivyo, maana kisiasa ku-come out na kichwa cha hii mada ni a serious na very big statement!
 
Mzee ES,
Hapana. Mzee Ndesa hawawezi kumgusa pale Moshi. Refer uchaguzi uliopita. CCM walimwaga pesa na Ndesa naye alikuwa na maaskari wake wa miavuli CCM wakalamba chini. Juu ya biashara wote wako above board. They pay their taxes na hawawapi CCM loophole yoyote ya kuwatia hatiani. Mwulize Freeman next time he is in NY atakuambia.
 
Hayo ya NY sielewi unachosema, na sikutegemea mtu kama wewe utakuwemo kwenye hayo ya location za wanaforum na ID zao, za kwako ninazo tena mpaka the ugly ones za personal yako je ungependa niziweke hapa? Heshima ni kitu cha bure ndugu yangu, hii at the end of the day ni forum tu au burudani kwenye bulogu!

Back on the ishu kama ninakuelewa vizuri, una maana kutetereka kwa biashara za Wassira na mpaka kuamua kurudi CCM, hakuhusiani na CCM, mana kuna kina Freeman na Ndesamburo, ambao biashara zao zinaendelea bila ya matatizo katika utawala wa CCM, au?
 
...............................
Back on the ishu kama ninakuelewa vizuri, una maana kutetereka kwa biashara za Wassira na mpaka kuamua kurudi CCM, hakuhusiani na CCM, mana kuna kina Freeman na Ndesamburo, ambao biashara zao zinaendelea bila ya matatizo katika utawala wa CCM, au?

Au ana maana kuwa kama wangekuwa CCM, basi zingefana zaidi ya hapo zilipo sasa na bila kelele kama Manji, Dewji, RA, Chande, etc.
 
Mzee ES.. Tanzania ni ya wana CCM peke yake? Sizungumzii suala la utawala tu, nazungumzia mentality nzima ya uongozi.
 
Mzee MMJ,

Heshima mbele mkuu, all is good na fair na ushauri wako, lakini ni vigumu kufanyika bila ya kuwa na guidance za kisheria, ambazo ninaziona zina-luck kwenye kulitekeleza hapa bongo,

Ushauri wako ni msumari, lakini kwa maoni yangu ili ufanyike vizuri ni lazima kuwe na mabadiliko ya kikatiba yetu!


Mzee Kiungani,

Hiyo ni a little bit tooo much, damn!
 
Mzee Es, nakubaliana na wewe. Hata hivyo kwa mfano wa serikali ya Kitaifa Katiba haikatazi. Ibara 55:4 inasema kuwa Mawaziri watateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa Wabunge. Kipengele hicho hata hivyo hakisemi kuwa watoke kwenye chama cha Wabunge wengi zaidi au chama tawala! Na kipengele kinachofuata kinasema mawaziri watafanya kazi kwa ridhaa ya Rais (at the pleasure of the President) ina maana Rais anaweza kumteua Mbunge yoyote kuwa Waziri!

Kwanini basi, marais wetu wanafikiri kuwa wanatakiwa kuteua watu toka kwenye chama chao tu? Ndio maana binafsi naona tuna na utaratibu kuwa endapo chama cha kisiasa kitashinda kura zaidi ya asilimi 50 basi chaweza kuunda serikali itakayo, lakini kikishinda kwa kura chini ya 50 (hatuna run off election TZ) basi serikali itakayounda ni lazima iwe ya Kitaifa!

Kwa vile sheria hiyo haipo kwa sasa, mwongozi ni Katiba, Rais akiamua kumteua Mbunge wa TLP au CUF na kumpa Uwaziri au unaibu Waziri hatakuwa amevunja Katiba! Hivyo, kuna yanayowezekana sasa hivi ambayo hayahitaji kusubiri mabadiliko ya Katiba au Sheria.

Ukiondoa hilo la Uwaziri kuna mambo mengi ambapo serikali inaweza kushirikiana na wale wasio katika CCM na mambo yakawa mazuri tu. Zanzibar wangeondoa matatizo mengi kama wangefikiri angalau kwa dakika chache kuwa Zanzibar ni yao wote siyo ya CCM peke yake!
 
Mzee ES,
Wassira biashara zake zilikuwa ndipo zinaanza tu, huku akiendesha upinzani. Ilikuwa rahisi kumwekea vikwazo/mikwara etc. Akina Ndesa na Free biashara zao ni established kwa muda mrefu hata kabla ya kuingia kwenye siasa. That was the difference.
 
hivi kwa mfano Mzee Mengi angejitangaza kuwa yeye yuko upinzani... mnafikiri angepata shida? sidhani...
 
Naona malalamiko ya Mengi kuhusu kukatiwa umeme kila siku siku, ya uhusiano wowote na "UPINZANI"? Naona matangazo yake yanasema hali ikiendelea hivi itabidi awe anafungua station mara chache!. Wapo watu walioko upinzani wanaoendelea na biashara zao. Lakini wapo pia ninao wafahamu walioko upinzani ambao miradi yao ilihujumiwa kwa sababu za kisiasa na wapo ninaowafahamu kwa majina ambao walifikia hatua hata ya kuamua kujiunga CCM. Kwa hiyo hili si suala la kweli. Ni changamoto kwa wote walioko upinzani ama wanaotaka kuingia upinzani ama wanaopenda kuona upinzani ukiendelea kushamiri.

Civil service sio chombo cha makada wa kisiasa. Katika nchi zilizoendelea civil service ni institution inayofanya kazi na chama chochote...lakini hapa Tanzania mfanyakazi wa serikali unalazimishwa na mazingira ama kuwa CCM au kusema huna chama.......pamoja na Waraka wa Lumbanga kutoa haki kwa watumishi wa umma kujiunga na vyama lakini hali ni tofauti..........mfano mdogo tu...kwa hiyo kuna tatizo la kushughulikia hapa..tusiipuuze tu hii hoja kirahisi rahisi............

Na ukitaka kujua upana wa hii hoja tazama wakuu wa wilaya(read civil servants) wanavyolazimishwa kikanuni na kimuundo kuwa wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama za CCM huku wakati huo huo wakiwa wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za serikali...........katiba haimlazimishi rais kuteua makada kuwa wakuu wa wilaya...is it by coincidence kwamba wanaoteuliwa ni wanachama waandamizi wa CCM? Huu ni mfano tu........
 
finally.. you are getting my drift... serikali kuwa ya CCM haina maana nchi ni ya wana CCM peke yao au na wale wenye mahusiano mema nayo!
 
CUF ikiingia madarakani itabidi kufanya a bit of "de-Baathification" which, for all we see now in Mesopotamia, is almost impossible.
 
Mbaya zaidi hii inahamia mpaka kwenye biashara. Angalia orodha ya makampuni yanayopewa tenda nyingi kubwa za kiserikali, utakuta the likes of MO, RA etc....

Kwa kweli CCM wanadhani wanahatimiliki juu ya nchi hii. Na haka kaugonywa kanashuka mpaka kwenye halmashauri..angalia tenda zinakwenda kwa kina nani.........na hii ndio sababu ya udiwani kupiganiwa kwa nguvu zote ingawaje una 'kaposho kadogo'!

hii inashuka chini zaidi....hata balozi wa nyumba kumi naye anajiona ni sultani kwenye kuweza kuamua hatma ya wananchi katika eneo lake........

"UCCM" ni ugonjwa unaofunika uwezo wa kufikiri kama Taifa!. This guys should get out of the box!

Hali inakuwa mbaya zaidi pale ambapo taifa linagawanywa katika makundi makubwa mawili- CCM na Wapinzani....kwamba hata mtu wa HAKIELIMU akiipinga serikali naye anaitwa mpinzani!....

CCM wanapaswa kujua kuwa ni watanzani less than 20 ambao wako ndani ya vyama vya siasa.........more than 80% wanajiita neutral..........suluhisho la kudumu ni kutenganisha kati ya chama na serikali........na hii inaanzia katika katiba ya nchi...TUNAPASWA KUEPUKA KUWA NA CHAMA DOLA.....CCM NI CHAMA DOLA, bado kunaendeshwa na imani kwamba chama tawala ni kila kitu na hata fikra za viongozi wao ziko namna hiyo..."You are either for them or against them. ...they do not think "WIN WIN"
 
Back
Top Bottom