Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

et tu brute, kwako Butus, vipande vizito hivyo
 
Sawa,
Labda nitangulize kipande hiki kisha nipate feed back za watu. Wapi nibadilishe ama kipi niongezee maanake unajua tunaweza kutunga kitabu cha pamoja hapa?..mengi yaliyotangulia umewahi kunisikia nikiyasema mijadala iliyotangulia. Kisha lugha ya uandishi mjomba mimi bado kabisa sijaenda shule! ila nakuombeni jaribuni kuipata message!..naandika kama nanyoongea, kazi kweli kweli!

Hata hivyo itachukua miezi kukamilisha kwa hiyo tuanze na kipande hiki kulingana na mawazo yangu mimi binafsi - MJAMAA mimi!

Nimeondoa kichwa cha habari kinachotangulia.

UTANGULIZI

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikisumbuka kuelewa hasa dhumuni la nchi yetu na hasa nchi za kiafrika tulipodai uhuru wetu toka kwa mkoloni ikiwa matokeo ya uhuru huo umekuwa na matunda mabaya sana kwa raia wake kisiasa na kiuchumi. nachopenda kujiuliza kila mara ni kati ya maswali haya:-

Kiutawala:- Je, dhumuni hasa lilikuwa kumwondoa mtawala mlowezi na badala yake kumweka mzawa tukitumia falsafa inayofanana na nguvu ya milki iliyowekwa na mkoloni?

Kiuchumi:- Je, ilikuwa mategemeo ya wengi viongozi kubadilisha mkono wa mtawala wa uchumi toka mlowezi na badala yake kushikwa na mzawa pasipo kuwa na dira yenye malengo ya kumkomboa mwananchi kiuchumi ama tulitegemea kwamba zimwi likujualo halikuli likakwisha!..

Nini hasa maana ya neno UHURU ikiwa wananchi wengi wa nchi zilizo huru wamekuwa na maisha mabaya zaidi chini ya utawala wa mzawa. Adui mkubwa wa maendeleo ya mwafrika imekuwa mwafrika mwenyewe. Umaskini wa mwafrika umezidi kukua baada ya Uhuru na ujenzi wa matabaka baina ya wananchi kiuchumi umeshamiri zaidi ktk siasa zetu.

Leo hii imefikia kuwepo na watu wanaosema - Afadhali ya mkoloni!

Hili ni neno zito sana na lenye uchungu mkubwa kwa mwenye kufikiri, kwa sababu umaskini wa mwafrika ni maradhi ya kujitakia zaidi ya hali halisi na yawezekana kabisa kuwa UHURU wetu umetafsirika vibaya hivyo kupoteza malengo ambayo yalikusudiwa toka awali kwa sababu ya tamaa ya baadhi watu wachache walioshika ama wanaendelea kushika madaraka aidha kwa kuchaguliwa ama kuteuliwa.

Pamoja na maswali yote haya, sio rahisi kupata majibu yake ikiwa tutashindwa kutambua kwanza - Sisi tumetoka wapi na yapi yalikuwa malengo yetu! Kwa kifupi tumetoka wapi na tunakwenda wapi!?

Nini madhumuni ya ubunifu wa Itikadi ambayo ingetuongoza kama dira katika kila hatua ya maendeleo yetu. Nje ya hapo Uhuru kwa mwafrika utakuwa hauna tofauti kabisa na mabadiliko ya sura ya mtawala.

Kiongozi mwafrika ni binadamu mwenye tamaa na hisia zote za kibinadamu kama watawala wengine na kuna kila sababu ya mtawala mwafrika kuwa mbaya sawa ama zaidi ya mtawala mgeni. Kwani mtawala mgeni hutegemea zaidi nguvu ya silaha kuendesha utawala wake wa mabavu, wakati mwenyeji anaweza jificha chini ya rangi yake kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo.


Umaskini wa mwafrika ni maradhi ya kujitakia na yawezekana kabisa kuwa UHURU wetu umetafsirika vibaya toka mwanzo hivyo kupoteza kabisa dira ya uhuru huo. Hii vita kubwa ya kumkomboa mwafrika ktk Umaskini itawezekana tu ikiwa sisi tutaweza kutambua dira na malengo yetu na wapi tumekwama. Na Katika kuyatazama hayo ndipo tutaweza kuweka maazimio mapya, maazimio ambayo yataambatana na uboreshaji wa KATIBA katika vitengo muhimu vya UTAWALA, SHERIA na UWAJIBIKAJI kulingana na hitlafu zitakazo jitokeza.

Katika kifungu hiki nitazungumzia zaidi dira ya kitaifa kwa kuzingatia zaidi msukumo uliotufanya sisi kuchagua dira ya kitaifa baada ya uhuru kuwa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA.

1. UJAMAA ikiwa na maana ya ujenzi wa UMOJA wa Watanzania wote ktk maendeleo na usatawi jamii hiyo.

2.KUJITEGEMEA ikiwa na maana ya ujenzi wa Uchumi wetu ili kutupa uwezo wa kuendesha maendeleo yetu bila kutegemea misaada toka nchi nyingine.

Haya ni maelezo ya uchache kama sababu za kimsingi ambazo zimetokana na historia ya nchi yetu, historia ambayo imetufanya tujifunze mengi mabaya na mazuri chini ya utawala wa mkoloni.

Na kutokana na sababu hizo tulipata msukomo wa kupitisha dira hii ya kitaifa ambayo tuliijengea maazimio na mikakati ili tuweze kwenda mbele kama taifa huru. Hayo Maazimio na Mikakati kwa kiasi ilitusogeza mbele lakini ilifika mahala tukakwama, hazikuweza kuzaa matunda tena kitaifa tofauti na madhumuni yaliyotangulia.

Hapa nikiwa na maana kwamba kwa kiasi kikubwa Tanzania iliweza kujenga nguzo za ujenzi wa UJAMAA kiasi kwamba Tanzania ilikuwa moja ya nchi chache maskini duniani zilizosimamisha UJAMAA wa kweli baina ya wananchi wake lakini tulikuja shindwa baada ya nguzo hizo kuanza kuachia kutokana na kutokuwa na msingi mzuri wenye uwezo wa kubeba uzito wa jumba zima la UJAMAA na KUJITEGEMEA.

Kushindwa kwa nguzo hizi kusimama, kumetokana na uzito mkubwa uliobeba kipengele cha pili cha dira yetu yaani KUJITEGEMEA. Kipengele ambacho wakati wote hakikupewa muda kutazamwa kwa makini zaidi ama kutenganishwa na imani yetu ktk siasa zilizokuwa zimetawala dunia.

Ujamaa badala ya kuwa ni UMOJA wa wananchi wake katika maendeleo ya pamoja ukajengwa kwa kuiga kiutendaji itikadi za wageni zenye malengo ya kujenga ama kuboresha bado uchumi wa dola zao. Baada ya Wakoloni kuondoka, mfumo mpya wa kiutawala ulivumbuliwa, utawala ambao ulizua falsafa mpya ya ujenzi wa makoloni ya kiuchumi kwa njia ya mawasiliano badala ya dola ama milki lakini bado nchi za kiafrika na nyingine maskini ziliendelea kuwa tegemezi wa falsafa za utawala huo wa Kibepari na Kikomnisti.

Ukitazama kwa makini utakuta kwamba Wamarekani, Warusi, Wajarumani, Wareno, Wahispania, Wajapan, Wachina na Waingereza wote walisimama kama mataifa yenye kutaka kutawala, kudumisha na kulinda tawala zao nje ya mipaka yao kwa kutumia mawasiliano ya kiuchumi ambayo haitofautiani na dhumuni la mwanzo la dola ya mkoloni ambalo lilikuwa ni uwezo wao kumiliki uchumi wa nchi nyingine kwa kuweka utawala wa dola ndani ya nchi hizo kuhakikisha mafao ya nchi hizo yanarudi kujenga nchi zao.

Hii ndiyo azma kubwa ya siasa zote za nchi za Ulaya, azma ambayo ilikuja zua vita kubwa baina yao wakitutazama sisi kama ngo'mbe jike linalohitaji fahari wa kumiki zizi. Kila fahari akaingia na rangi zake, makeke na kila vitisho ambavyo vinaweza kumvutia ngo'mbe jike.

Ni tofauti hizi za umilikaji wa uchumi nje ya mipaka yao ndio chanzo kikubwa kilichowasha vita zote kuu za dunia. Tofauti ambazo sisi tulikuja kuzikumbatia na kuzitangaza kwa kuzipigia debe hali misingi ya ujenzi wa rasimu na hata ilani yake haikuwa kwa manufaa ya nchi zetu au kuboresha mazingira yetu bali sisi kutumiwa kama watumishi watawaliwa mithiri ya mchwa wanavyojenga makazi yao kwa manufaa ya malkia.

Ukimwondoa malkia mchwa hana maisha tena kwa hiyo uhai wake unategemea kuwepo kwa malkia ambaye ni unique ktk kizazi.

Tanzania na baadhi ya nchi maskini tukajikuta tukifuata mkondo wa Urusi bila kufahamu kwamba wao walijenga itikadi hii pingamizi kwa nchi za magharibi wakati wakizitawala nchi zote za USSR na ulaya ya mashariki kiuchumi na hata China wakizitawala nchi nyingi za Asia ya mbali kiuchumi.

Kwa kifupi Ujamaa na Ubepari ni mifumo ya kiuchumi iliyojengwa ktk mazingira ya kuboresha nchi zao wakizitumia nchi maskini kama shamba la kuvuna kwa mapana ya mipaka kulingana na mbegu za kisiasa walizopandikiza. Ni katika kuiga hizi siasa Maazimio yasiyo kuwa na hesabu yalijengwa kwa kupotosha madhumuni yaliyotangulia kabla na baada ya uhuru. Matokeo yake tulipoteza kabisa dira na malengo yetu ya awali na kujitwika utumwa wa fikra za kupachikwa ambazo zimedumu hadi leo hii.

Tanzania imebaki kama uwanja mtupu uliojaa tope bila nyasi baada ya vita ya hao mafahari ambao bado hadi leo hii wanatafuta mabaki ya nyasi ktk malisho yao. Vita ya kwanza ya dunia na ile ya pili, zote zilitokea nchi zetu zikiwa bado chini ya utawala wa mkoloni isipokuwa vita hii baridi ya kisiasa kati ya Marekani na Urusi ndio vita pekee ambayo nchi zetu za kiafrika zimeweza kuusikia uzito wake kiuchumi kwa sababu vita hiyo imetukuta tukiwa huru na wenye kuwajibika ktk maendeleo ya nchi zetu. Matokeo ambayo yamekuwa jaribio jipya kwa nchi yetu kiasi kwamba tunadiriki kudai kuwepo kwa mabadiliko ya kiuchumi duniani hali ukweli umesimama kuwa ni mabadiliko ya kisiasa yaliyotangulia mabadiliko ya kiuchumi.

Misingi ya kiuchumi iliyotumika zamani bado ni ile ile toka mkoloni isipokuwa hatukuchukua muda kutafakari mchango wa siasa hizo ktk uchumi wa nchi maskini kama kikwazo kikubwa kilichopotosha malengo ya awali ktk kudai uhuru wetu. Pamoja na mabadiliko yote, misingi ya kiuchumi bado inaendelea kutazama maslahi ya nchi za Ulaya.

Hakuna tofauti kubwa za Kiuchumi kwa nchi maskini kati ya Ukoloni wa kilowezi na Ukoloni mamboleo ila mabadiliko yote ya kiuchumi yalitokana na ukweli kwamba nchi nyingi zilizokuwa zimetawaliwa kuwa huru. Sheria na masharti ya biashara yalipanuliwa zaidi kutokana na kuongezeka kwa teknologia na hasa kulinda soko kubwa la nchi hizo. Hata hivyo bado nchi maskini tunatumiwa kama tulivyokuwa tukitumiwa wakati wa Mkoloni, wakati wa vita baridi na leohii ktk mfumo mpya wa Ukoloni mamboleo.
Huko ndiko tulikotoka!..

Haya waungwana nasubiri dondoo zenu kabla sijaendelea! nadhani mnaelewa naelekea wapi mjamaa miye!
 
TUMESIMAMA WAPI

Ikumbukwe tu kwamba huko nyuma nimezungumzia mataifa makubwa ambayo walitumia Ulowezi kutawala nchi zetu kisha baada ya nchi zetu kupata Uhuru wakatumia mawasiliano ya kisiasa (Ubepari na Ukomunist) ili kushika uchumi wa nchi maskini. Hivyo basi ni muhimu kutazama tena mfumo wao wa kiutalawa umeundwa vipi kuhusiana na nchi zetu maskini.

Baada ya vita baridi nchi hizi hizi walianzisha mfumo mwingine mpya wa kutawala uchumi duniani kwa kuunda chombo cha utawala kiitwacho World Trade Organisation – (WTO). Chombo ambacho kinazitenga tofauti zao za kiutawala na kuwaunganisha pamoja kiuchumi ili wapate kuweka sheria na mgao wa mafao ya biashara ya dunia nzima kwa sababu hakuna tena nafasi za Ulowezi, hakuna tena mfumo wa siasa na itikadi zinazo jenga mawasiliano baina ya mataifa isipokuwa siasa sasa hivi ni BIASHARA yenyewe!. Katika mfumo huu nchi hizi zimeweza kutajirika zaidi kuliko wakati wowote huko nyuma kwa sababu muungano wa nguvu hizi umeweza kukusanya zaidi ya kugombea kusika mataifa ambayo ndani yake kulikuwa na mataifa mengi yaliyokataa kabisa kujiunga na siasa za upande wowote.

Nchi hizo leo hii zimejikuta zikibanwa pia katika mfumo huu mpya ambao unaendeshwa kwa kutumia mabillioni ya fedha wakijenga taasisi mbalimbali za kisheria kuhakikisha kwamba uchumi wan chi zote duniani umekamatwa na wao.

WTO ni chombo pekee cha kimataifa kinachoweka sheria za biashara duniani lakini chombo hiki kina wanachama wachache sana kuiwakilisha dunia nzima. Wawakilishi hawa ni wale wale watawala wetu wakati wote wa mkoloni na ule wa vita baridi. WTO ni chombo cha kati kinachotunga sheria za ugawaji wa mafao kwa nchi hizo na kila mmoja wao hutazama maslahi ya nchi yake kwanza ktk makubaliano yoyote ya sheria za kibiashara. Hakuna nafasi ktk mfumo huu unaotazama nchi maskini kama ilivyokuwa toka mifumo ya kiutawala iliyotangulia.

Hivyo basi, baada ya uchambuzi mrefu uliotangulia, sasa tumefika katika kipindi kigumu zaidi. Kwa hiyo kabla sijaendelea mbele ni muhimu kwetu kujiuliza nafasi yetu katika mfumo huu. Tanzania Tumesimama wapi?.
Tanzania imesimama wapi katika safari yake ndefu ya Kujitegemea (Independence) toka tuupate uhuru huo. Hakika Tanzania bado ni nchi tegemezi na maskini kama alivyotuacha mkoloni. Naposema bado maskini kama alivyotuacha mkoloni naomba ieleweke kwamba nafasi yetu kimataifa bado kabisa haijabadilika. Kabla ya mkoloni hajaondoka Tanzania ilikuwa nchi moja maskini sana pengine ktk nafasi kumi za mwisho na leo hii baada ya miaka zaidi ya 40 bado imesimama ktk fungu la mwisho.

Tukumbuke pia kwamba kila hatua tuliyopiga mbele ni hatua ya makuzi yaani mabadiliko ya kimaumbile. Tulianza kwa kutambaa, kisha tukasimama dede, na mwisho tumeweza kutembea lakini ktk mazingira mabaya sana. Kuna makundi ya watu ambao hupima maendeleo ya nchi zetu kwa kutumia umri kama kielelezo cha maendeleo ya nchi ktk kufuta umaskini hali ukweli ni kwamba hakuna kipimo cha kuondoa umaskini ama kufikia kujitegemea kinachotokana na makuzi ya Umri ila ukubwa wa maumbile ya mwili yanaweza kutokana na umri.

Wale wote wanaodai kwamba nchi yetu bado changa ndio maana bado tu maskini, hakika hizi ni sababu finyu ambazo zinatazama ukuaji wa nchi kwa umri ili kufikia utu uzima ambacho ni kipimo tofauti kabisa wala hakina uhusiano na kipimo cha umaskini wa nchi. Kuna mataifa yenye umri mdogo sana ktk uhuru wao kuliko sisi lakini yameweza kusonga mbele yetu kiuchumi na kuna mataifa ya zamani sana ambayo yanayumba kiuchumi. Hata binadamu kwa maisha yetu wapo vijana wadogo sana waliokuwa na utajiri wa hali na mali kuliko watu wazima na pia wapo watu wazima wengi ambao maisha yao ni maskini wa hali na mali toka wazaliwe.

Pamoja na kufahamu wapi tumesimama bado swali letu halijapata jibu? Kwa nini nchi yetu bado maskini hadi leo mbali na kuwa huru chini ya dola inayo ongozwa na wazawa tukiwa na mamlaka yote ya rasilimali zetu tukijumuisha na fungu kubwa la misaada ya fedha na teknologia zilizofungashwa na mikakati iliyoandaliwa na wataalam vyote hivi kumiminika nchini mwaka hadi mwaka?

Hivyo basi tunapo angalia nafasi na maslahi ya Tanzania ktk mfumo huu mpya unaotawala uchumi wa dunia, dhahiri hatuwezi kupata jawabu nje ya kujitazama sisi wenyewe kwanza tumejifunza nini katika historia yetu na sio kusahau ama kuizika historia yote. Hatuwezi kuondoa Umaskini nchini ikiwa hatutaweza kutafuta mbinu dhidi ya mfumo huu wa kiutawala unaodumisha kuhodhi uchumi wa nchi maskini kama mifumo iliyotangulia. Ni muhimu sana kutazama nafasi na maslahi ya Tanzania ktk mfumo huu kinyume cha kutazama mfumo huu ili kuibadilisha Tanzania..

Wachina wana msemo usemao:-

To seek the truth from Facts!– To look for economic and Political solutions that have practical application rather than those based on Political ideology.

Ikiwa na maana ya kutafuta ufumbuzi wa kisiasa na kiuchumi ambao unaweza kufanya kazi kiutendaji kuliko ufumbuzi ule uliojengwa kutokana na itikadi za kisiasa.

Haya ni maneno mazito sana kwa mwenye upeo mkubwa hasa tukizingatia huko tulikotoka. Mfano mzuri sana wa msemo huu ni ule uliotutokea miaka ya 70 hadi 80 wakati wananchi walipokuwa wakipanga mistari madukani kununua vitu muhimu kama sukari, chunvi, Unga na mafuta. Vitu hivi vyote vilikuwa vikizalishwa ndani nchini lakini kwa sababu sera nyingi za serikali wakati ule zilikuwa zikitungwa kwa kutumia itikadi za kisiasa tulizofungiwa ktk mabahasha tulishindwa kabisa kujikwamu kwa zaidi ya miaka 10.

Hata wale washauri wa mwalimu wakati ule walichofanya kumshauri mwalimu ilikuwa kuacha itikadi moja ya Kichina na kupendekeza itikadi nyingine pingamizi ya nchi za magharibi. Mwalimu Nyerere hakukubali kabisa mfumo wa nchi za magharibi kiuchumi lakini pia hakuweza kutazama nje ya itikadi za mashariki ya mbali ambazo zote hizi ni mifumo iliyotungwa ktk mazingira ya nchi zao kuhusiana na nchi zetu zinazo zalisha. Haikuwa mifumo iliyolenga maendeleo ya nchi zinazo zalisha bila kuwahusisha wao kama ndio wagawaji wakubwa wa utajiri unaopatikana toka nchi zetu.

Huwa napenda sana kutumia msemo mmoja unaosema, Ni ujuha kufikiria kuijaza chupa maji wakati huna maji ila ni rahisi kufikiria ujazo wa chupa ikiwa unayo maji. Kwa maana hii inatufundisha sisi kujenga mbinu za uzalishaji zinazo wezekana kutekelezeka kulingana na mazingira yetu badala ya kutumia siasa zilizojaa dhana na imani ya mazingira ya nje yasiyo shabihiana na mazingira yetu. Msemo huu hautofautiani sana na ule msemo wa Kichina niliouweka hapo juu.

Hii ndio imani yangu ya kwanza inayotangulia sababu zote za msingi kwa nchi maskini zilizojipatia uhuru wake kisha zikashindwa kuacha ibada mbaya ambazo tuliamini mwanzo kuwa ni potofu. Nitatanguliza mfano mwingine mdogo sana kwa kutumia imani ya dini. Ikiwa mtu ama watu wamekubali mafundisho ya dini fulani kwa madhumuni ya kuondokana na madhambi, wakasilimu (Kubatizwa) lakini bado matendo yao ni yaleyale nje ya mafundisho ya dini hiyo basi watu hawa watakuwa wamepotea na wamejidanganya wenyewe kwani hapakuwepo sababu toka mwanzo ya wao kubatizwa.

Vilevile wale watao ondoka dini ama dhehebu moja na kujiunga na imani nyingine lakini wakashindwa kuacha imani na mafundisho ya dini iliyotangulia watu hawa watakuwa wamekosa ama kupotosha mwongozo wa nafsi zao. Hawa watu hawawezi kuwa waumini wa kweli hata kama watabeba majina makubwa ya dini zao mpya kama vile tunavyobeba itikadi nzito ya Ujamaa na Kujitegemea hali bado tukifanya ibada zetu kwa sala za mkoloni.

Kwa maana ndefu ni kwamba chini ya Utawala wa Mwalimu tulikuwa na dira yetu yenye malengo lakini bado tulifuata itikadi (dini) za wageni. Kilichobadilika hapo zaidi ni kutokuwa na mtawala mlowezi kisha tukachagua dini moja ya mkoloni tukiwa chini ya kiongozi mweusi. Kibaya cha imani ya dini hii ya kisiasa ni kwamba malipo yake ni hapa hapa duniani tofauti na imani ya dini za kweli ambazo malengo yake ni sisi kuwa binadamu wema wenye kupendana hapa duniani kwa malipo ya akhera!..
Ikawa kila tunalofanya lazima tutazame nje huko kwenye makao makuu ya dhehebu letu kabla hatujatunga sheria ama sera kwa manufaa ya Watanzania. Mchango wetu mkubwa ktk imani ya maendeleo yetu ukaendelea kuwa tegemezi la siasa na sheria zinazotungwa nje hata kama mazingira baina yetu hayakuwa sawa.

Ukitazama sera zote ndani ya imani ya Ujamaa na Kujitegemea zilibuniwa kutokana na imani za mafundisho ya Kikommunist. Kuna zilizoweza kufanya kazi na nyingine zilishindikana kabisa kwa sababu ya tofauti za kimazingira. Tulishindwa kwenda mbele bila kufahamu kilichotuangusha zaidi ya kusingizia nchi za magharibi ama mashariki kwa siasa zao wakati ilikuwa ni uchagzui wetu wenyewe kufuata siasa hizo.

Baada ya Nyerere tulijikuta tena tukifungiwa kanyaboya jingine la Uongozi wa chama chetu CCM wamekuwa wakipandikiza mbegu mpya ziliyojengwa na hao watawala wa mwanzo. Mbegu ambayo zimetufanya sisi sote tuamini kuwa kuna mabadiliko ya kiuchumi duniani bila kuzingatia kwamba mabadiliko haya ya Kiuchumi yanayodaiwa yametokana na Mabadiliko ya siasa za nchi hizo. Kifo cha vita baridi kati ya nchi za magharibi na zile za mashariki ndio sababu kubwa ya kuwepo kwa mabadiliko ya kiuchumi duniani.

Aidha kuna watao dai kuwa kifo cha Siasa za nchi za mashariki kulitokana na uchumi mbovu wa nchi hizo, bila kuzingatia tena kuwa uchumi wa nchi za USSR na China usingekuwa mbovu kama sio msimamo mbaya wa siasa zao za kiutawala.

Hivyo basi mzizi ama mbegu chafu ya umasikini wetu ni kuendelea kukumbatia msahafu (mwongozo) ambao umejengwa na mataifa yanayotaka kuendeleza utawala wa uchumi wa dunia. Hakuna hata taifa moja kati yao linaloweza kukataa ukweli huu, isipokuwa wanaokataa ukweli huu ni sisi watawaliwa ambao elimu yetu inategemea vitabu vinavyoandikwa na watawala. Elimu yoyote ile na hasa ya uchumi inatambuliwa tu kama imetokana na mtazamo wa nchi hizi.

Hatukuomba uhuru wetu kwa kutazama maisha ya Urusi, Uingereza ama Marekani bali tuliomba uhuru wetu kwa kutazama nafasi yetu nje ya kutawaliwa na hao hao wahusika. Hivyo ni muhimu kuweka sawa malengo yetu ya awali kabla na baada ya Uhuru. Hapa narejesha upya utangulizi wa maelezo yangu ya awali kuwa ni lazima tukubali ukweli uliotangulia ili kujikumbusha upya sababu zilizo tusukuma hadi kupigania uhuru wetu na hata kufikia Ubunifu ya falsafa UJAMAA na KUJITEGEMEA kama dira ya kitaifa…
 
Bob Mkandara!
Asalaam Aleykum!

Nime-print hizi articles mbili ili nizisome kwa utulivu!
Mdogo wako hapa ni MJAMAA mwenzio!
Umenikuna!
 
UTAWALA.

Kabla hatujagusia kipande hiki cha Utawala naomba ieleweke kwamba sikupendekeza falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea kujenga hoja za mustakabali wa taifa. Ikumbukwe kuwa ubunifu wa Ujamaa na Kujitegemea ulitokana na viongozi wetu walio tutangulia chini ya chama kimoja kwa manufaa ya taifa huru. Majukumu yao yalijikita zaidi kwenye harakati za kupigania uhuru, kujenga umoja wetu unaokusanya makabila yote kutupa isimu jamii itakayo ungana kama Waswahili, kuondoa ujinga, kuleta haki na usawa, kujenga na kudumisha amani, kuendeleza ukombozi wa Afrika, kupambana na ukoloni mamboleo.

Haya yote ni mafundisho yaliyotangulia ambayo ni muhimu sana kwetu kuyakumbuka na kuyatambua. Katika utawala wa nchi yetu historia inatukumbusha kuwa waasisi wetu walichukulia swala la Utawala kama ni swala la Ukombozi wa mwafrika kutokana na utumwa. Hawakufuata falsafa inayofanana na ile ya milki zilizotawala ama walowezi isipokuwa walipingana nazo. Walijenga majukumu yao kwa vipaumbele ktk ukombozi wa mwafrika dhidi ya Utawala uliokuwa sugu kumthamini mwafrika kama binadamu anayestahili maendeleo yake. Hadhi ya mtu mweusi ilipotea zaidi pale umaskini ulipozidi, hadhi ambayo haikujaliwa na mkoloni kiasi kwamba walidiriki hata kutuita sisi Kifao. Kiongozi yeyote asiyefahamu na kuthamini historia hii, akashindwa kutambua ni hatua zipi taifa letu limepitia hadi kuwa hapa tulipo, huyu sio kiongozi tunayemhitaji.

Kwa hiyo mbali na historia ya nchi yetu ambayo tumeitazama huko nyuma kuna historia pia ya viongozi waasisi wetu ambayo pia imepotea.

Wakati wa Nyerere, Ikulu hapakuwa mahala pa kila mtu…na kiti cha urais hakikuwa kiti cha mwanasiasa yeyote yule ambaye amesoma ana hadhi, umaarufu na sura ya kuwa rais. Lakini leo hii Kiti cha Urais kila mwanasiasa anakiona kama ni moja ya viti vilivyoandaliwa ktk meza ya chakula. Hakuna kipimo cha vigezo kinachotumika katika kutafuta rais ama viongozi wa ngazi za juu toka utawala wa Mh. Mwinyi.

Tumekuwa na baadhi viongozi walioshindwa ktk nyadhifa nyingine ambao waliondolewa ama kulazimika kujiuzulu. Leo hii wamerudi kwa nguvu mpya na usanii ambao haukubaliki kwa wananchi. Wapo viongozi ambao wamediriki hata kuibadilisha historia yetu wakipindua pindua katiba waliyoapishwa kuilinda kwa manufaa ya nafasi zao katika uongozi. Wapo ambao walishindwa hata uchaguzi mdogo wa ubunge katika wilaya zao bado wanatafuta nafasi pana ya kuwa rais wa Jamhuri ama waziri kwa kutumia mbinu chafu katika kugombea Ubunge. Viongozi ambao kamwe hawawezi kusema kwa ndimi zao kuwa majukumu yao hata kwa uchache ni pamoja na kulinda maslahi ya wakulima na wafanyakazi. Viongozi ambao leo hii wameturudisha katika makosa yale yale yaliotangulia Uhuru wetu kupotosha malengo na identity ya mwafrika kwa sababu viongozi hawa hawana sifa ya uongozi ila wanatumia elimu inayomhukumu mwafrika kuwa ni kiumbe mwenye mapungufu ya kufikiri na kiutendaji.

Uongozi ni kipaji kinachohitaji elimu ya kuelewa mafundisho na jinsi mafundisho hayo yanavyoweza kufanya kazi ktk jamii husika. Kiongozi ni mbunifu, mzalendo mwenye kuheshimu falsafa iliyotangulia ili utendaji kazi wa wale anaowaongoza uwe ktk mfululizo wa ibada zinazozingatia mustakabali wa taifa.

Uongozi uliopo leo hii unadai kuwa wa kizazi kipya, kizazi ambacho kina makundi mawili ndani yake. Kuna kundi la wazee ambao bado wanatumia siasa peke yake katika maswala ya uongozi kwa sababu bado wanatumia imani na misingi iliyojengwa chini ya siasa ya kijamaa. Viongozi hawa hawawezi kuachia madaraka ambayo yamewapa nafasi ya utawala kwa zaidi ya miaka 50 pamoja na kwamba siasa za duniani zimebadilika kabisa
.
Kundi jingine ni hilo la vijana wanaotumia elimu zao kukumbatia mfumo mbaya wa kiuchumi unaotungwa nje kwa sababu hawa vijana wamesahau ama wameisha fukia ma kaburini historia iliyotangulia ambayo tuliachiwa na waasisi wa uhuru wetu.

Matokeo ya kuwa chini ya viongozi hawa, Tanzania imekuwa kama chombo kinachoelea baharini kikifuata mkondo wa maji yaendayo kwa kasi (current). Makundi haya yote mawili yanapotosha ama yanapishana katika ubunifu wa mbinu za kumkomboa Mtanzania kutokana na ADUI UMASKINI.

Nadhani kwa mtiririko wa maelezo yote haya lazima tuwe na mwelekeo mpya, mwelekeo ambao utazingatia makosa yaliyotendeka awali kupotosha maana ya Uhuru halisi ili tujenge misingi mipya na imara itakayo zingatia mazingira, rasilimali na utamaduni wetu kwa ushirikiano wa kimataifa.

Kinachotangulia ni ubunifu na kuunda upya Dira ya kitaifa inayozingatia historia yetu kwa kutukuza dhumuni kuu la waasisi wetu ambao nia zao za dhati walitaka tujikomboa kutoka katika makucha ya kutawaliwa kiuchumi, kurudisha hadi yetu na uwezo wa kuendesha serikali zetu wenyewe ktk ujenzi na kustawisha jamii yetu. Wazee wetu walipinga kabisa Utawala unaondelea kutumia raslimali zetu kwa ajili na manufaa ya Malkia. Kodi na maliasili vyote vilikuwa chini ya himaya zao. Hata miundombinu haikujengwa kwa makusudio ya kumwendeleza Mwafrika ila kurahisisha uchukuzi kwa faida ya miliki zao. Upinzani huo hau na tofauti na upinzani ambao unapinga kutumia rasilimali zetu kwa manufaa ya kundi la watu ama uhuru wetu kuwa chini ya himaya za baadhi viongozi.

Katika mchakato uliotangulia ni muhimu sana kutazama nafasi yetu duniani kama taifa huru lenye malengo yake tukizingatia mambo muhimu ktk ujenzi wa siasa zetu za ndani ya vyama utakao zingatia kwamba ufumbuzi wa matatizo yetu hauwezi kutegemea siasa za nje ama ndani bila kutanguliza uchumi na maslahi ya wananchi. Ikumbukwe tu kwamba leo hii SIASA ni UCHUMI na ubora wa UCHUMI wa nchi yeyote hutazamwa kwa vigezo ambavyo ndivyo chimbuko la wazee wetu kupigania uhuru wetu.

Kwa maana hiyo, mabadiliko yoyote ya dira na mfumo wa Uongozi ni muhimu kuzingatia kwa makini maudhui yale ya isimu jamii ya Watanzania kama watu huru wenye uwezo wa kubuni mbinu za kiuchumi kulingana na mazingira yetu bila kutegemea wageni kama wataalam wa mahitaji yetu.

Seek the truth from Facts:- Kutafuta ufumbuzi wa kisiasa na kiuchumi ambao unaweza kufanya kazi kiutendaji kuliko ufumbuzi ule uliojengwa kutokana na itikadi za kisiasa.

Hiki ni kigezo kikubwa cha mwongozo katika kutafuta ufumbuzi wa kutatua matatizo yetu. Mafanikio yetu ni muhimu yatokane na majaribio zaidi kuliko falsafa za kisiasa. Badala ya kutangaza maazimio kwa taifa zima ni bora azimio hilo lifanyie majaribio katika wilaya ama mkoa mmoja ili kutazama mafanikio yake kwanza kabla ya kulijengea ngome za kisheria kuwa mujibu kwa kwa taifa zima. Huu ni mwongozo ambao unahitaji elimu zaidi ya siasa.

Viongozi wetu leo hii ni katika makundi ya waumini wa dini mbili, wale wamebeba majina makubwa lakini hawafuati ibada za dini zao wakihofia mabadiliko ya vigezo vya kiongozi dunia ambavyo vinapingana na uwezo wao. Na kundi jingine ambalo limepoteza kabisa historia yetu isipokuwa wanachotumia ni elimu ya kukodisha toka nchi za nje kiasi kwamba wanaonekana kama wasanii wa ktk mchezo wa sinema ya maendeleo ambayo haina ukweli zaidi ya ubunifu wa dhana zinayofurahisha roho.

Hawa wote wamesababisha chombo hiki Tanzania kiwe hakina tena mwelekeo zaidi ya kuhakikisha kinaelea baharini huku wakiomba kudra za mwenyezi Mungu. Nguvu za wananchi katika upigaji kasia pia zimekuwa za mchanganyiko wakihofia zaidi nguvu ya maji kutopindua mashua kuliko kutazama kule chombo kinako elekea. Kuna makundi yanayoamini kwa dhana kuwa mbele ni shwari na wengine wanahaha kwa kuhofia maporomoko ya maji kama yale ya Livingstone kule Zambia.

Hii ndio sababu inayonipa shauku katika utangulizi wangu kuhoji kama dhumuni hasa la kugombea uhuru wetu Kiutawala lilikuwa kumwondoa mtawala mlowezi na badala yake kumweka mzawa tukitumia falsafa inayofanana na nguvu ya milki iliyowekwa na mkoloni? .
 
Kuna baadhi ya watu ambao kwa namna fulani wanafikiri kuwa au wamejiambia hadi wakaamini kuwa Tanzania ni ya kwao peke yao na uzao wao! Hili halikubaliki, tutalipinga, na kukumbushana kuwa nchi hii ni yetu sisi sote na wakati umefika kwa wale waliomadarakani kuanza kuufanyia kazi ukweli huu.

Kuna mawazo ndani ya watawala wetu kuwa mtu yeyote ambaye hajapiga magoti na kusujudu kwenye altare ya CCM basi mtu huyo hafai kupewa nafasi ya kuitumikia nchi yake! Hivi kuna sababu yoyote ya msingi ya kwanini serikali isimtumie Prof. Lipumba katika nafasi fulani? Je kuna sababu yoyote kuwa wasomi walioko nje ya CCM (kwenye upinzani au kwingineko) hawafai na hawastahili kuaminiwa na kupewa nafasi ya kutumikia nchi yao?

Inavyoonekana ni kuwa katika Tanzania ya sasa wanaotaka kufanikiwa na wanaopaswa kufanikiwa ni wale wenye "kuvaa kijani na njano" vinginevyo ni kuwa watu "wameula wa chuya"!

Wakati umefika kwa serikali kupanua mawazo yake kuhusu nani ni Mtanzania haswa na ni nani ana ujuzi, vipaji au uwezo wa kushiriki katika uongozi wa Taifa lake! Hatutaweza kupata mawazo tofauti na changamoto za dhati kama sehemu ya Watanzania inawekwa kando kwa vile tu ati siyo Wana CCM!

Ni nani aliyesema kuwa wana CCM ndio Watanzania wazalendo, wenye uwezo zaidi na wanaostahili zaidi!!

Kikwete alipigiwa kura milioni 9, CCM ina wanachama kama milioni tano (wenye kadi).. wale milioni tano waliompigia kura wanawakilishwa vipi katika uongozi wa Taifa lao!!!!??

Naendelea kwa kina hapa: http://mwanakijiji.podomatic.com
 
Hongera sana Mzee Mwanakijiji kwa Hoja yako, nakuunga mkono mia kwa mia, ni kweli kuna haja ya CCM kubadili huo utaratibu wao wa Kiimla na kuwatumia wasomi wengi tu wa nchi hii ambao si lazima kuwepo ndani ya CCM ndio wawaone ni wenzao.
Maendeleo ya nchi hii ambayo ni yetu sote yanahitaji sana uwepo wa Wasomi hao, ambao wengi wao kama si wote wamesomeshwa na pesa za walipa kodi wa Nchi hii yetu sote, kwanini wasipate nafasi ya kuitumia Elimu hiyo kwa faida ya Taifa hili?
 
CCM wao akili yao yoooooooooote ni kwamba kama wewe si mwana CCM basi hata kazi ama uongozi na maisha yako ndani ya Tanzania ni batili .Hata JK ndiyo mawazo yake hana tofauti na Kingunge wala Mwema ambaye polisi wake wamewapiga watu sana huko Tunduru kisa kajimbo .
 
Wakati umefika tuanze kulipigia hili kelele, ama sivyo kuna kizazi cha Watanzania ambacho kimewekwa nje ya utumishi wa Taifa lao kisa tu wao "Sio wana CCM". Haiwezekani watu milioni nne, waamue hatima ya watu milioni karibu 40!!
 
Kuwa mpinzani ni sehemu mhimu sana ya kulitumikia taifa la Tanzania. Lipumba au msomi yeyote yule hakatazwi au hanyimwi haki ya kutoa mchango wake wa kuiendeleza Tanzania.
Unless niwe sikukupata vizuri katika lengo la mada yako; maoni yangu ni kuwa haikatazwi kwa kila mtu kuchangia. Au una maana ya kuwa na Serikali ya mseto (Govt of National Unity) ? Ikihusisha vyama vya upinzani? Hapa nadhani sijakupata sawa sawa. Kuniradhi.
 
Kalamu, maana yangu ni kuwa kuna wasomi, kuna watu wenye vipaji ambao wangeweza kutumiwa na serikali katika nafasi mbalimbali. Watu hao kwa sababu za "CCM kushika hatamu" wamewekwa nje katika utendaji wa serikali. Bila ya shaka umesikia suala la Mwanasheria Mkuu wa Marekani ambaye anadaiwa kufukuza kazi wanasheria kadhaa kwa sababu za kisiasa. Ingawa ni kweli Rais ana uwezo wa kumchagua na kumfukuza yeyote, taratibu ni lazima ziwe dhahiri siyo kwa sababu mtu fulani hayuko kwenye chama hicho.

Leo hii katika Tanzania, kuna watu ambao wanafikiri kuwa nchi ni ya kwao peke yao!

Kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa inawezekana kabisa kuwa ni jambo ambalo siku moja itabidi tuliweke kwenye sheria. Kwa mfano, Chama kikishinda kura chini ya asilimi 50 basi serikali yake ni lazima iwe ya umoja wa kitaifa ambapo theluthi moja ya mawaziri wake watoke vyama vingine!

Kwa hali ilivyo sasa, siku moja chama kitashinda kwa asilimia 35 na kuendelea kushika hatamu kana kwamba kimepewa mandate!

Ukiondoa mambo hayo ya uongozi wa juu, serikali ya CCM inaweza kuangalia katika upinzani na kuamua kuwashirikisha watu wenye uwezo kutoka katika upinzani au nje ya upinzani katika kutimiza majukumu mbalimbali. Leo hii Rais Bush licha ya mgogoro wake chama cha Democrat amemuomba Gov. Bill Richardson kufuatilia mabaki ya wanajeshi huko Korea ya Kaskazini! Hivi ukisikia Rais amemteua Prof. Shao kuwa mjumbe wa tume fulani au kuongoza idara fulani hali akijua ni mtu wa upinzani utafurahi au utataka nafasi hiyo apewe mwana CCM tu?
 
Kalamu,

Hapa ni suala la mentality. Mwenzio Mzee Mwanakijiji anaamini kwamba, kama kiongozi au mwanachama kutoka upinzani, kutoa mchango kwa nchi ni lazima uwe Serikalini au Rais akuteue kwenye tume fulani (hence mfano wa Prof. Shao). Loyal opposition, and to retain independent voice, ni moja ya mchango kwa Taifa.

Hili ni suala la mentality. Kwamba walioko Serikalini ndio wanaokula. Na kwamba la msingi kwake sio kuwa na majeshi makubwa ya upinzani kulaani ulaji. Yeye kwake la msingi ni kwamba wapinzani nao ni lazima waalikwe kwenye msosi.
 
HALI YAKO KIJANA WANGU.

NNIMI BABU YAKO MASANJA WA MAJEBELE. HUKU MAGU NI WAZIMA NA HATA WALE WADOGO ZAKO WA MISUNGWI.

LEO NILIKUWA NASOMA FORUM YETU NIMEONA MAMBO AMBAYO YAMENISHANGAZA KIASI CHA KUSHINDWA KUAMINI KAMA NI WEWE ULIYEANDIKA. HEBU NIAMBIE MJUKUU WANGU. NI TANZANIA GANI UNAYOITAKA WEWE?
PILI ULIKUWA UNAMAANISHA NINI KUSEMA KUWA

Kalamu, maana yangu ni kuwa kuna wasomi, kuna watu wenye vipaji ambao wangeweza kutumiwa na serikali katika nafasi mbalimbali. Watu hao kwa sababu za "CCM kushika hatamu" wamewekwa nje katika utendaji wa serikali........

KWA MTAZAMO WANGU NAFIKIRI BADO HAUJALELEWA KUWA TANZANIA INA WATU WASIOPUNGUA MILLION 30 NA HAO WASOMI NI WENGI ZAIDI YA 250...................NANI AKAE WAPI NA NANI AKAE WAPI. HIVI NAFASI ZA KUTEULIWA ZIPO NGAPI? NA KWANI NI LAZIMA AWE PROF.SHAYO AU MVUNGI TOKA UPINZANI. KWA NINI ASIWE PROF. ODHIAMBO AU PROF.RWEMA TOKA KWA WATANI WANGU WA JADI?


Kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa inawezekana kabisa kuwa ni jambo ambalo siku moja itabidi tuliweke kwenye sheria. Kwa mfano, Chama kikishinda kura chini ya asilimi 50 basi serikali yake ni lazima iwe ya umoja wa kitaifa ambapo theluthi moja ya mawaziri wake watoke vyama vingine!

UNAMAANISHA NINI KUSEMA KAULI KAMA HII. JE KAMA IKITOKEA KWAMBA BUNGE LIMEJAA WATU WA AMBAO HUWEZO WAO NI MDOGO, TUTAWAKARIBISHA WANANCHI KAMA WEWE NA MIMI?

'.....Ukiondoa mambo hayo ya uongozi wa juu, serikali ya CCM inaweza kuangalia katika upinzani na kuamua kuwashirikisha watu wenye uwezo kutoka katika upinzani au nje ya upinzani katika kutimiza majukumu mbalimbali......'

NAFIKIRI HILI SIO WAZO BAYA . LINAWEZA SHUGHULIKIWA BAADAYE. KUNA WATU WENGI WENYE MAWAZO MAZURI TOFAUTI NA YA WAKINA MNYIKA NA MBOWE(MTAZAMO WANGU). NI VYEMA KWELI MHESHIMIWA RAISI AKAWAFIKIRIA. HEBU TUANGALIE UWEPO WA NDUGU YANGU, MWANASHERIA MVUNGI. NI KWELI LAKINI MWANAKIJIJI NAOMBA USIONGELEE HABARI YA MREMA. MAANA HUYU BWANA TOKEA ALIVYOTOKA CCM SIJAWAHI SIKIA AMEONGEA LA MAANA ZAIDI YA SERIKALI MBAYA...HAKUNA SERIKALI ILIYO NZURI. KUBWA ZAIDI NI KWAMBA MAENDELEO YA KWELI YANAKUJA NA TUNARIDHIKA.


Leo hii Rais Bush licha ya mgogoro wake chama cha Democrat amemuomba Gov. Bill Richardson kufuatilia mabaki ya wanajeshi huko Korea ya Kaskazini! Hivi ukisikia Rais amemteua Prof. Shao kuwa mjumbe wa tume fulani au kuongoza idara fulani hali akijua ni mtu wa upinzani utafurahi au utataka nafasi hiyo apewe mwana CCM tu?

SUALA LA KUMSHIRIKISHA MTU KAMA PROF.SHAYO SIO BAYA ILA SIO KAMA BUSH ANAVYOFANYA. KUNA SHUGHULI ZA MAENDELEO LAKINI SIO SUALA LA KWENDA KUFUATA MIILI YA WAFU. NINAZUNGUMZIA KUWA HATA CHAIRMAN WA TUME YA SCIENCE NA TEKNOLOGIA.AU SIO MJUKUU WANGU.

MIMI BABU YENU
CHIEF MASANJA WA MAJEBELE
 
Ideally mwanakijiji you are right kuwa kile aliye mtanzania kwa vigezo vyovyote vile lazima na ni wajibu wake kikatiba kuenjoy national cake, hili lipo wazi halikuhitaji shule yeyote, I am afraid you are lost in the details

1. Mfano wako wa Professa Lipumba uko wrong:

- Sina shaka na elimu bora ya Professa Lipumba aliyoipata ndani ya nchi na nje, lakini hebu niambie mgombea urais wa CUF three times na kiongozi mkuu wa upinzani tanzania achaguliwe nafasi ipi ili amsaidie kikwete?

-Manake nafasi anazoweza kupata ni za kuteuliwa na rais ambaye yeye Prof. kwa kazi yake inatakiwa awe ni monitor wa government activities, sasa unatarajia kwamba lipumba apewe uwaziri wa uchumi ili aanze kuikandya serikali au vipi?!

- Kama ni ualimu wa chuo kikuu mimi nipo tayari hata kumfanyia lobbying awe mkuu wa kitengo chetu cha UCHUMI pale chuo kikuu kipya DODOMA, wasiliana nae nianze kampeni.....

2.Sio kweli kwamba katika Tanzania kuna watu wanadhani ukiwa CCM hufai:

- Unapoomba kazi serikalini huulizwi una kadi ya chama gani, watu wanapewa kazi on merit na uteuzi wa serikali kupitia kwa Rais huangalia uwezo na utendaji wa mtu, kuna renowned wapinzani ambao wapo katika presidential appointment kwa vile wana uwezo:

- Zitto Kabwe ni mjumbe wa Kamati ya Maoni ya Afrika Mashariki, appointed by JK

- Mwanasiasa wetu humu ni renowned CHADEMA tumempa Schorlaship na bado anaendelea kuserve katika faculty nyeti tu pale chuo kikuu.

Mifano ipo mingi kwa hakika.

3. ''Haiwezekani watu milioni 5 watuamulie watu milioni 40'''

I am afraid mwanakijiji unaishi katika cookoo land manake demokrasia inasema wengi wape, kama ni kweli ccm ina watu milioni 5 that's good for a party na kuwa wengine milioni 4 wameichagua CCM it's even better! sasa ulitaka iweje mheshimiwa mwanakijiji? Jeshi litwae madaraka? jeshi lina watu wangapi na litaongoza watu milioni arobaini,


Until you come up with Mwanakijiji alternative to power control I am afraid we have to stick to democracy ambayo imedictate kwamba CCM ina mandate ya kuongoza baada ya kupata USHINDI WA KISHINDO.

Hizi habari za kuwa wapinzani wanachukiwa ni maneno ya baraza ya kahawa na I don't think kama inadeserve kujadiliwa hapa, unless you come up with hoja!

Balozi Daraja alimpokea vizuri tu Juma Duni Haji alipokuwa america kwa vile mpinzani ni sehemu nyeti sana ya taifa, Balozi Maajar kafanya likewise alipokuja maalim Seif hapa ubalozini kwetu kwa vile ni kiongozi in his own right i.e. kiongozi wa chama cha upinzani...Sasa uongo kuwa ukiwa mpinzani unachukiwa ubakie hivyo hivyo uongo...

Otherwise nyote mna haki sawa kabisaaaa mbele ya katiba,

For more nyeti rejea hotuba ya Kikwete taifa alipoapishwa, rejea hotuba ya kikwete london *2 [ziara zote mbili]
 
Kulikoni, na wengine... naomba nisieleweke vibaya kuliko nilivyotaka kueleweka. Ninachosema ni kitu chepesi kuwa Tanzania ni yetu sisi sote na kwa hilo tushirikishane kutaka kujenga nchi, na hapa sizungumzii wapinzani tu bali hata wale wasio na vyama (kama mimi). Ninachosema ni kuwa tusikubali hata kidogo watu kuanza kuwa na mawazo kuwa ukitaka kufanikiwa, na ukitaka mambo yako yakunyokee ni lazima uwe CCM! au uwe na uhusiano na "wakubwa" wa CCM

Mfano wako wa Zitto... kama Zitto asingekuwa Mbunge toka Chadema Rais Kikwete angemteua? I doubt it! Na sizungumzii nafasi za uteuzi tu, nazungumzia mentality nzima ya viongozi! Subiri kikao hiki cha Bunge uone mtiririko wa hoja utakavyokuwa, sitashangaa ukiona kuwa mawazo ya baadhi ya Wabunge yanazunguka katika chama na maslahi ya chama zaidi kuliko ya Taifa zima!

Hoja yangu ni nyepesi, Tanzania ni ya Watanzania wote wenye vyama, wasio na vyama, wenye dini na wasio na dini, walioko nyumbani na wasio nyumbani!

Ni rahisi kiasi gani kwa mpinzani kuanzisha radio inayoweza kusikika nchi nzima? Sijui lakini sitashangaa baadhi ya wapinzani wamejaribu kufanya hivyo wakabakia kuzungushwa zungushwa! Ni rahisi kiasi gani kwa watu walio nje ya CCM au wigo wa CCM kupewa tenda au kupewa nafasi ya kuuzia serikali? I'll bet you not that easy! Kwenye ngazi za chini sitashangaa watu wengi tunapewa nafasi karibu sawa.. ila kwa kadiri unavyokwenda juu ndivyo bati la CCM linavyozidi kufunika na kuwakinga wachache!!!

Tafadhali nieleweke, sizungumzii wapinzani peke yao, nazungumzia wale wote ambao kwa namna moja au nyingine hawako connected na Chama cha Mapinduzi! Ukifikiri kidogo, unaweza kuuona kuwa siko mbali sana na ukweli.
 
Kwani hivi ni wapi hapo ambapo wapinzani walitaka kufungua radio wakazungushwa? tutajie mpinzani huyo manake hii msibeat around the bush....


Nawajua wapinzani ambao wanafanya biashara zao freesh tu:

Ndesamburo:

The hotel tycoon pale moshi, dar na kwingineko , hivi umesikia lini watu wakapigwa marufuku au hata yeye mwenyewe akalalamika kuwa ananyanyaswa kibiashara, ukifuata kanuni utatimiziwa yanayotakiwa.

MBOWE:

Ana biashara ya disco lake pale Bilicanas na vile vile Gazeti lake la Tanzania Daima, muulize kama alihangaishwa kusajili tanzania daima au la...

Hivi umeshawahi kusikia wazee wakapiga mikwara watoto wasiende disco la mbowe kwa vile ni mpinzani?

Haiwezekani 'mpinzani' akakataa kutimiza masharti kisha apewe anachotaka kwa vile eti aspopewa itaonekana anasumbuliwa! No way!

Yes najua watu wengi ambao hawana vyama na bado mambo yao safi i mean wapo serikalini na vile vile kwenye sekta binafsi....

Hii habari ya ''ukitaka mambo yako yakunyookee ingia ccm'' msitake kuispin, the logic is simple kuwa ukitaka mambo yako yakunyookee ingia ccm kwa vile ina sera nzuri, kanuni nzuri na utawala bora hivyo you are sure kwamba kwa kujiunga na chama chenye mandate ya kuongoza tanzania basi you are helping to cement these things katika sekta binafsi yaani you are sure kwamba nchi itaendelea kuwa chini ya ccm na hivyo you will continue to enjoy peace and stability kama kawa na kuendelea na shughuli zako!
 
Kulikoni, I like the last part of your comments.... the great spinner.. you spinned it real good this time..!!
 
Tatizo la sisi watanzania ni kutaka kujenga nyumba hewani. Haitasimama. Msingi wa yote haya ni katiba. Madai ya katiba mpya ndio starting point.....Mengine yatafuata
 
Back
Top Bottom