Brutus, while youa re at it.. jaribu kuninyambulia kama tungetaka kujenga "Ujamaa wa Kiafrika" ungekuwaje?
Nd. Mwanakijiji!
Hili suala sio dogo na wala tusili-underestimate!
kabla hatujatazama "Ujamaa wa Kiafrika hebu kwanza tutupie macho "Ujamaa wa kizungu au ki-asia!
Marx na Angels walieleza kwamba mfumo wa maendeleo ya maisha ya binadamu una hatua kadhaa:
1. Primitive Communalism ( Ujima)
hapa watu waliishi maisha duni yasiyo na teknologia. Waliishi pamoja kupitia jamii zao za kijima (Communal societies)!
mfano mzuri wa hili kaangalie movie.. " The gods must be crazy"
2. Utumwa ( Slavery)
Hapa watu waliuzwa toka kwenye "Communal Societies" kwenda kwenye tabaka jingine la watu walioendelea kidogo baada ya kuhodhi ardhi kubwa "Feudal Lords" ambako walitumika kama vitendea kazi!
Mchanganyiko huu wa watumwa na mabwana zao wenye kuhodhi mashamba makubwa uliunda mfumo mpya..,..
3 Ukabaila..(Feudalism)
Na huu mfumo mpya ulipoendelea na kuanza kuchipuka kwa viwanda... na kukomeshwa kwa biashara ya utumwa kukazaa mfumo mpya...
4. Capitalism ( Ubepari)..
Hapa sasa... wale watumwa walioachiwa huru toka kwenye mfumo wa Ukabaila wakageuka kuwa Wafanyakazi (workers)!
Lakini kukawa na tatizo... hawa wafanyakazi wakawa wananyonywa sana... wakafanyishwa kazi ngumu kwa masaa mengi lakini kwa ujira mdogo. Hali hii ni unyonyaji wa jasho la wafanyakazi... ndipo kukatokea fukuto la mapinduzi .. kwamba kuwe na mgawanyo sawa wa mapato. Fukuto hili likazaa mfumo mwingine wa kinadharia zaidi kuliko vitendo ..
5. Socialism!
Hapa ndipo tunawasikia Bolsheviks na ndugu zao... (Mapinduzi ya Urusi)
Lakini sasa... sio watu wote waliokubaliana na mgawanyo sawa wa mali. Hii ikasababisha mgawanyiko wa itikadi.
Waliofuata Warusi wakaunda kundi lao.. na waliokataa wakaunda makundi yao.. ( Eastern and Western Blocs)!
Ingawa hawa watu wa magharibi hawakukubaliana na Bolsheviks, lakini walikuja na ideas zao.. na mojawapo kuu likawa ni kupunguza makali ya Ubepari ,.. "social injustices) ili mfumo huu uwe na faida kwa wote... wenye mali na wafanyakazi. Vikaundwa vyama vilivyokuwa na lengo la kuimarisha sheria za kazi (labour laws) ili wafanyakazi wapate haki zao za kimsingi.. wasinyonywe na mabepari; vyama hivi pia vikajitahidi kuhakikisha middle class inaneemeka na mfumo mzima wa kibepari kwa kutumia mifumo ya ustawi wa jamii.. (Welfare)!
Hapa ndipo tunapokutana na Democrats wa marekani, Labour wa UK, Social Democrats wa Ujerumani na kadhalika.
Ni vyama vinavyotetea tabia za kijamaa bila kuwa na nembo ya Ujamaa!
Sasa tukirudi Afrika....
Sisi hatukupitia hizi pilika pilika kama walizopitia wenzetu!
Wana wa Afrika akina Lumumba, Nyerere, Mondlane, Nkrumah, Neto na wengineo wakaja na ideologies zao!
Mwl. Nyerere akaonyesha mfano kwa ku-implement Ujamaa na Azimio la Arusha. Na wazo lake kuu ni kama alivyosema;
nanukuu...
The objective of Ujamaa (socialism) in the United Republic of Tanzania is to build a society in which all members have equal rights and equal opportunities; in which all can live in peace with their neighbours without suffering or imposing injustice, being exploited, or exploiting; and in which all have a gradually increasing basic level of material welfare before any individual lives. (Nyerere 1968: 340)
Akaja na idea za Vijiji vya ujamaa,.. hapa watekelezaji wakaanza kuvurunda.. wakawa kama Bolsheviks... mambo ya kuchapana bakora na kuhamishana kinguvu!
Vikaanzishwa viwanda na mabenki... lakini watendaji wakavurunda pia...
Badala ya Kuendesha miundombinu hii kwa kutumia kanuni na sheria za kibepari kwa faida ya umma, wakayaendesha kwa staili ya ( Cha-wote.. who cares!)
Kwa hiyo tulikuwa na mwelekeo sahihi ( vector) lakini tukashindwa kuendesha mambo kisayansi!
Mwalimu alipokata tamaa, waliorithi ndio kama hao.. umesoma mwenyewe hotuba kwenye attachment!
Ikawa ni style ya "fungulia mbwa"!
Awamu ya tatu ikaja.. ikakuta hali imekuwa mbaya... tumeshanasa kwenye nyavu. katika kukuru-kakara za kujinasua.. tumejikuta tunajisonga zaidi kwenye nyavu zao... jamaa wanatubeba kilaiiiniiii wanatimua zao na kapu kwapani!
Tuko kwenye awamu ya nne!
Can we jump out of the basket and be free?
Au ndio tutaangukia mchangani na kukaushwa na jua?
What are we supposed to do?
The middle class is suffering!
The question is...
How can we reform the current situation for our own good?
Grandma aliyeko kijijini atapataje huduma za afya za kisasa kwa gharama nafuu?
Je, Huyu Grandma anaishi vipi wakati anaendelea kulima kwa kutumia jembe la mkono na maksai kama walivyotumia nabii Musa na mitume wenzake karne mia kadhaa zilizopita?
Tunasemaje kwamba Kilimo ndio UTI WA MGONGO wakati babu kizee wa nebraska analima shamba lake kwa kutumia John Deer na kumwagilia na anauza mahindi yake mpaka kwenye makampuni ya kutengeneza Ethanol.. na babu yetu wa Tosamaganga mpaka avute bangi kwanza.. alime weee halafu mvua inampiga bao.. na hakuna alternatives?
Tanzania ilipaswa isambaze chakula mpaka Sudan, Somalia, Eritrea na Ethiopia!
badala yake tunapokea msaada wa vyakula!