Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

mugongo... hiyo ndiyo hatari... kama CCM haiwezi kushirikisha wapinzani.. siku ikianguka (na hiyo siku ipo), wale wote wanaojulikana kuwa ni makada wa ccM itabidi waondolewe katika utumishi na makada wa chama hicho kipya wawekwe madarakani. Nina uhakika CCM watakuwa wa kwanza kulaani kitendo cha kuwaondoa wana CCM katika utumishi wa ngazi za juu kisa tu wao ni wana CCM... Ni lazima serikali ya CCM ioneshe mfano kuwa Tanzania inaweza kuongowa kiumoja!!
 
MKJ
Umoja ambao ccm upo kwa sasahivi ni wa sherehe tu muungano, uhuru,hapo utawaona wapinzani wamejaa lakini baado ya hapo ndio unaporudi uadui kama kazi,
kwanini wengine wanathubutu kusema kwamba mpizani katika tanzania hatatawala maisha ? halafu wewe unatuambia hiyo siku ipo unamakengenza mzee MKJ? wakati leo watu wanapanga nani achukue nafasi ya muungwana na nani pm
Si unaona mwenyewe au unasikia tunduru vipi ushindi umepatikana au zanzibar ni vipi hao watu wanashinda sasaleo mgombea anasema kabisa kwamba kura yake na ya mkewake zinawatosha kuingia ikulu na nikwelizinawafikisha huko jee hauoni kuwa upinzani tz ni wakati wa kampeni tu? fisi aliufuata mkono hivyo hivyo
 
Wanasema kile ambacho watu kila leo wanakipigia kelele lakini hatuoni hatua zozote. Huyu Mwakyembe kwa nini hakuwaambia wenzie wasilijadili kama kamati ya CCM suala la Richmond kama kweli anataka mikataba?

Kama ni kweli wanataka mikataba ipelekwe bungeni ni nini kitawazuia kufanya utaratibu wao wa kawaida wa kukutana kama kamati ya chama kuweka msimamo wa pamoja ?

Ninachoona hapa na wao wanataka mgao katika dili hizi za mikataba. Hiki ndicho bila shaka wanatafuta; Wizara husika ikilipeleka suala bungeni basi wanawatafuta wale wanaoamini ndio vocal Mps kama huyu Mzindakaya na Mwakyembe halafu wanawapenyeshea bahasha na wanakubaliana kuwaunga mkono, halu tunaambiwa suala lilifikishwa bungeni!
 
Hakuna Mkapa wala baba yake Kikwete hawa wametuangamiza na kutufikisha hapa tulipo kila moja kwa njia moja au nyingine Ila huyu mwenye usukani kwa sasa Mwendo wake ni mbovu na wa HATARI YA AINA YA BUFALLO Katika ustawi wa Nchi Yetu Kiuchumi..
 
SHULE.jpg


http://harakati.blogspot.com/2007/04/unaona-nini-katika-picha-hii.html

Ziko wapi pesa za kuwanunulia madawati na viti watoto hawa? Mikopo na misaada yote tunayopata kama nchi inaishia wapi?

Mikataba tuliyosaini ya uchimabaji wa madini inasemekana inaingiza mabilioni ya fedha katika mfuko wa hazina, ziko wapi pesa hizo ziwaondolee adha hii watoto hawa?

TRA inakusanya shilingi bilioni 250 kwa mwezi, ziko wapi pesa hizo ili watoto hawa na wafurahie matunda ya "kukuwa kwa uchumi"?

Baada ya miaka 46 ya uhuru inatia aibu na kusikitisha kuona hali kama hii inaendelea katika shule nyingi za Tanzania.
 
Something good happen To those who deserve less and well prepared to work hard!!

Keep Faith....

I think this should sound like Maisha bora kwa kila mwenye Nia
 
Mimi nasema hawa watu ndiyo maji ya aina hii waliahidiwa? Maji haya yana rangi gani sijui hebu angalia mwenyewe ama kweli maisha bora .

attachment.php
 

Attachments

  • MajiTaaabuKwelikweliDar0428.JPG
    MajiTaaabuKwelikweliDar0428.JPG
    8.5 KB · Views: 87
Kulaumu tu hakuwezi kutusaidia.

siasa ni kama biashara, ambapo tunasema biashara ni kuuziana na kunuliana.

Kama mtu kaja na lebo ya bidhaa yake mpya lakini bidhaa hizo unazifahamu zinatengenezwa na kampuni fulani na bidhaa hizo zina ubora fulani na kuna bidhaa nyingine nyingi tu, ukashawihika kwa lebo ukanunua ukikuta bidhaa mbovu usimlaumu tu aliyekuuzia bali hata wewe ujilaumu kwa kununua bidhaa mbovu.

kama tungekuwa ni wenye busara tungehoji tangu mwanzo maisha hayo bora kwa kila mtanzania yatapatikanaje. tukachambuliwa mpango mzima ndio tukubali au tukatae sasa kama tulikubali kichwa kichwa yeye alifaulu maana malengo yake yalitimia.

ila sisi kama tuliyahitaji hatujapata basi sisi ndio tumefeli. Sasa wahenga walisema tunajifunza kutokana na makosa. je kutokana na yaliyopita tumejifunza nini? na turekeshe wapi na kwa jinsi gani ndio changamoto yetu inayotukabili.

lakini vile vile tusisahau kuwa katika kuleta maisha bora kwa kila mtanzania ni serikali kutoa dira na ikishatoa dira jitihada zetu wenyewe ndio zitakamilisha msemo huu.

serikali ikitoa dira wakati wananchi wenyewe hawako tayari kuangaikia maisha yao haiwezi kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. au wananchi kuwa tayari kuangaikia maisha yao wakati serikali haitoi dira ni kazi bure pia.

Hivyo kabla ya kulaumu serikali lazima tuangalie kama sisi wananchi tumeplay part katika eneo letu.
 
Nimekutana na hiki kibomu hapa chini, nimechoka kabisa. Pamoja na maharusi, nyoma choma, totos kwa sana, kumbe sisi ndio Taifa ambalo hatuna furaha kuliko yote duniani! Soma hapa chini. Inawezekana hee! Yaani hata Zimbabwe, Darfur, DRC na Somalia wana furaha kuliko sisi?!

The Happiness Index
See which nations rank high, low and somewhere in-between on a 0-to-10 scale of life enjoyment.
Newsweek
The golden rule of economics is that well-being is a simple function of income. That's why nations strive for a higher and higher GDP; it's also a key reason why people struggle to make more money—income gives us choice and a measure of freedom. But over the past decade or so, there's been growing evidence that wealth isn't as important as once thought. Studies show that beyond a certain income, more money doesn't lead to any permanent increase in happiness. What's more important is not so much what we have, but whether we have more than our neighbors. The following rankings of happiest and least-happy nations was taken from the World Database of Happiness, the product of research by scientists at Erasmus University Rotterdam in the Netherlands. The researchers scored nations based on citizens' responses to survey questions about their life satisfaction from 1995 and 2005. In the 0-to-10 scale, 0 equals "extremely unhappy" and 10 means "extremely happy." The results:

The Happiest Nations
1. Denmark, 8.2
2. Switzerland, 8.1
3. Austria, 8.0
4. Iceland, 7.8
5. Finland, 7.7
6. Australia, 7.7
7. Canada, 7.6
8. Ireland, 7.6
9. Luxembourg, 7.6
10. Mexico, 7.6

The Least-Happy Nations
1. Tanzania, 3.2
2. Zimbabwe, 3.3
3. Moldova, 3.5
4. Ukraine, 3.6
5. Armenia, 3.7
6. Belarus, 4.0
7. Georgia, 4.1
8. Bulgaria, 4.2
9. Pakistan, 4.3
10. Russia, 4.4

Countries With the Biggest Disparity Between Happy and Unhappy Citizens
1. Egypt
2. Tanzania
3. Algeria
4. Venezuela
5. Brazil
6. South Africa
7. Zimbabwe
8. India, Nigeria, Kyrgyzstan, Turkey (four-way tie)

© 2007 Newsweek, Inc.
 
Ukiangalia kwa makini nchi zisizo na demokrasia ndio zinaongoza kwa kutokuwa na furaha. Kuna mtu anafanya utafiti kutafuta link kati ya furaha na demokrasia, nahisi atathibitisha hypothesis yangu hapo juu!
 
Watanzania wangekuwa hawako happy wasingewapigia kura ccm. Hakuna nchi ina watu wameridhika kama Tanzania, pamoja na umasikini wao majority (vijijini) roho zao haziwaumi kuwepo kwao Tanzania. Wao JK hata akipita barabara kuu kuelekea mkoa mwingine wanafurahi kusikia tu amepita.

Huko mijini ndio usiseme hayo uliyosema hapo juu yote yapo, vigezo vya huu utafiti nina mashaka navyo.
 
Kitila Mkumbo, hii sehemu ni nyeti zaidi katika post yako. Walio na furaha na wasio na furaha, gap ni kubwa sana. Je, hii haielezei tunachosema kila siku kuwa tofauti kati ya masikini na matajiri wachache ni kubwa mno Tanzania?
Countries With the Biggest Disparity Between Happy and Unhappy Citizens
1. Egypt
2. Tanzania
3. Algeria
4. Venezuela
5. Brazil
6. South Africa
7. Zimbabwe
8. India, Nigeria, Kyrgyzstan, Turkey (four-way tie)

© 2007 Newsweek, Inc.

Ngoja nikachecki gini-coefficient ili nijue tofauti ya kipato kati ya matajiri na masikini. Inaogofya kwa taifa linalojenga 'jamii ya watu walio sawa na huru'
 
Hapo hata mimi nimechoka kabisa. Kama ni kweli hii ni aibu. Na issue ya income gap our policy makers wanalichukilia ni mzaha lakini ni tatizo kubwa. Gap kati ya masikini na tajiri Tanzania inaonekana kwa macho wala hatuhitaji ma index na ma GIN Coeficient. Gap kati ya vijijini na mijini nayo inatisha lakini hata siku moja sijawahi kufikiria kuwa sisi ndio tusiokuwana naraha kuliko wote duniani!!!!!!!!!!!!!!!! Sasa sipati picha labda nisikie kutoka kwenu wana JF, Watanzania hatujawahi kuwa na vita kama tunazoziona kwa wenzetu, tunarasilimali, tuna kila kitu nachoweza kufikiri mungu alitupa. Hapa sasa inabidi watanzania niwaite Wasoneneka. Umasikini wetu upo kwenye mind zetu na political will ya wanasiasa wetu. Umasikini wetu unasababiswa na ujinga wetu ndio maana wengi wameridhika sasa hii ni hatari wandugu. Yaani hapa navuta pumzi ndefu kupata hii analysisi. Duh poleni sana watanzania wenzangu.
 
Katika mada zilizonifurahisha leo hii kweli kiboko!
Na kutokuwa na furaha nako tumo? Duh!
 
Sasa nakwambia kama wangetupima katika confidence index ndio tungelia kabisa!
 
Kitila,

Yaani wewe mtundu sana, tena sana.

Umeyapata wapi haya? Kwa hiyo watanzania hatuna chochote zaidi ya amani tunayohubiriwa kila uchao. Na hata hiyo inayoitwa amani ni woga tu.

Sometimes mtu unakwenda mbali unaona bora tuchukue mtoto tuanze kufyekana tu. ushakuwa usen.. ooops sorry
 
Labda sisi tunaweza kuwa wakali kwenye mchezo wa ku*ana; na wenyewe na doubt hata hivyo kama tunaweza kufua dafu kwa wanaume wengine (samahanini sana, nawapenda wote!)
 
PICHA KWA NIABA YA BLOG YA MAGGID MJENGWA

Kinondoni2.JPG




shughuli2.JPG



ua2.JPG


xbagashop.jpg



raha itoke wapi katika mazingira haya
 
Je, tutafika! KIpindi cha Makwaiya, cha leo (1 mosi) saa mbili na nusu kilikuwa kinajadili ujio wa uchaguzi mkuu wa ccm kwa kutizama taswira ama visioni ya chama katika kuendesha chama kwa maslahi ya wananchi. Waalikwa kwenye kipindi walikuwa Balozi Daudi Mwakawago 2), Dr. Kamata (Idara ya Siasa UDSM) Yusuphu Khalimoja (Mwandishi)

Mambo mengi yaliibuliwa katika mjadala, lakini yanayokuja akilini haraka haraka, ni mambo makuu matatu: uanachama, itikadi, na visioni ya taifa

A: UANACHAMA
1. Kunamsemo maarufu, mara nyingi unatumika katika nyimbo ama misemo ya chama cha mapindizu nayo husema “CHAMA KINAWENYEWE NA WENYEWE ndio SISI.
*Swali la msingi lililoulizwa “wenyewe ni kinani”?

Majibu:

a. Watu wa kawaida ni rahisi kusema ni wenye chama lakini sio viongozi- Yusuphu Khalimoja

b. Maneno hayo yanatumika kama kauli mbiu, kiasili, msingi wa chama ni watu, yaani wakulima na wafanyakazi. Msingi huu ndio uliisaidia TANU na CCM kuleta mapinduzi ya kijamaa, wanachama wakiwa askari wa mbele wa mabadiliko. leo swala ni ushindi wa uchaguzi, hakuna mafunzo ya kiitikadi wala historia ya chimbuko la chama. Hatari – Kamata

c. Wanachama bado ni wakulima na wafanyakazi, ila kuna mkanganyiko. mkanganyiko unaletwa na historia ya mabadiliko ya dunia ya kiuchumi na kisiasa, ikitenganisha kati ya waasisi wa chama na wananchama wapya ama ambao wamebadilishwa na mabadiliko ya kihistoria, au kati ya wanachama waliopita katika tanuru ya itikadi na ambao hawakupitia- lazima migongano na mapambano yatokee katika fikira, mikakati, oganiizisheni - balozi

B: ITIKADI

2. Kunamkanganyiko kati ya itikadi ya chama na sera mbalimbali za nchi. Ukiangalia katiba ya nchi na katiba ya ccm toleo la 2005, lengo ni kujenga ujamaa na kukitegemea wakati nchi imejikita katika uchumi wa kidunia wenye maslahi ya kibeberu na utegemezi.

Maangalizo yaliyotolewa:a) kuna mkanganyiko kati ya itikadi na sera mbalimbali za nchi. Hii ni hatari ni sawa na dereva anayeonyesha ishara ya kukata kulia kumbe anaendelea mbele ama anakata kushoto, na hawa madereva ni wengi, matokeo yake ajali.

b) chama kimeacha taratibu zake za msingi ambazo zilikuwa zinaanda makada wa chama, viongozi na wanachama wa kawaida kikiwajenga kujua maslahi ya chama kwa taifa na kuwapa misingi ya kulinda maslahi ya nchi kwa manufaa ya taifa. Hatari yake ni kwamba vijana wa leo hawajui historia, misingi, itikadi wala visioni ya chama. Hili si tatizo la ccm tu ni vyama vyote vya siasa.
c

3. Ujamaa lengo lake ilikuwa kutengeneza fursa sawa kwa wanachi na kujenga uchumi wa kitaifa, taswira ama visioni iliyosahihi kabisa, haina kosa.

Swali: kama hatutaki usawa na uchumi wa kitaifa tunataka nini?


Misemo iliyokumbukwa.

Pale ambapo chama cha mapinduzi kitakapoacha ilikadi ya ujamaa na kujitegemea haitabaki- Nyerere

Chama changu kimetekwa nyara na Matajiri- Mkapa

Misemo iliyoibuka kwenye mjadala

Chama cha ccm kimebaki kama ganda la yai lakini ndani liko tupu- Kamata

Utabiri uliotolewa

Sitashangaa kuona viongozi wanochaguliwa katika mwaka huu wa uchaguzi kuweka mawazo yao kimaandishi – Balozi

HATARI zilizobainishwa
Tabaka lawaliojuu linajizalisha lenyewe, linaanza kuachana na wabangaizaji, na walioko madarakani wameanza kujizalisha wenyewe.

CCM inabaki kuwa chama cha Uchaguzi, ili kubaki madarakani kinahitaji wakulima na wafanyakazi, si kwa nasaba, kwa kupata kura.

Kwa mtazamo wangu mimi, mjadala huu umeibua maswali ya msingi nayojiuliza kila siku na kichwa kinapata moto kidogo. Ningependa nasi tujiulize maswali hayo kwani ndio msingi wa mabadiliko yoyote yale tunayoyataka kwa taifa hili.

kwanza tujitambue sisi ni watanzania ndivyo tunavyotambulika., na tutaendelea kutambulika hivyo

pili tukubaliane matatizo yetu ya msingi ni yapi

tatu, ni lazima tukubaliane mbinu za kuondoa matatizo yetu

lakini la msingi kuliko yote ni kukubaliana itikadi ambayo ndio itajenga msingi wa mapambano yetu.

Historia yetu, inamafundisho mengi sana ambayo tukirudi nyuma na kutizama tutajifunza na kuendelea. Sioni haya kusema, kama kunawakati ambapo naona taifa hili lilipata kutoa mwelekeo thabiti na kutuonyesha sisi kama taifa sera za ujamaa na kujitegemee kupitia azimio la arusha na mwongozo. Sikujaliwa kuishi enzi hizo, ila niyasomapo maandiko hayo leo ninaona tungefika tu.

pamoja
 
Back
Top Bottom