Matatizo ya wakulima wa miwa Mtibwa

Matatizo ya wakulima wa miwa Mtibwa

Zambavuni

Senior Member
Joined
May 24, 2012
Posts
118
Reaction score
26
Hello wana JF!
Hivi matatizo ya wakulima wa miwa huko mtibwa mbona huwa ni kitendawili kisichoteguka? Akienda Mkuu wa nchi hana majibu, mkuu wa mkoa, yale yale, mawaziri hamna kitu. Huko kulikoni? Nasikia Muwekezaji halipi kwa wakati, pesa anawapa kidogo mpaka wanashindwa kuendeleza zao hilo. Ebu jamani kuna mdau mwenye uelewa kulikoni huko?
 
Ndugu yangu Zambavuni, serikali na viongozi wake wote wamo mifukoni mwa wafanyabiashara wakubwa unadhani nani atamsikiliza mkulima mdogo au mlalahoi. Matokeo ya serikali za aina hazikusanyi kodi na maendeleo huwa ni ndogo; wizi, ufisadi, rushwa na uonevu kwa walalahoi ndio sifa ya serikali ya aina hii. Kwa hiyo tuungane na tuseme inatosha.
 
Nawaonea huruma sana watu wa Mtibwa. Kusema kweli wamerudi nyuma sana kimaendeleo kuliko hata miaka ile ya shirika la umma. Mwekezaji yule, (Superdol) kama sikosei, sidhani kama ana uelewa wa kuendesha kiwanda hata cha kutengeneza ice cream. Ukifananisha na Kilombero, Mtibwa is a pathetic story. Sio tu hawana uwezo wa kulipa miwa wanayo nunua kwa wakati, lakini mara nyingi tu anachelewa hata kuanza msimu wa kutengeneza sukari.
Lakini hii ndiyo Tanzania maana ubinafsishaji wake nao umejaa mastory kibao
 
Ok! Tunafanye nini sasa? Au Kigoda wa Viwanda na biashara yaweza kuja na suruhisho kwa hili?
 
Hivi hakuna uwezekano wa kuanzisha kiwanda kingine karibu na Mtibwa? Nasikia wakulima wa miwa wa kenya wanaendesha mercedes benz tokana na kilimo hicho hicho cha miwa.
 
That alternative could be the best...however, are the cans enough to run more than one factory in the same place? Pili, iliyokuwa Dakawa Ranch, sasa hivi amechukua nani? NAFCO Dakawa inamilikiwa na nani? In the past, the capitalization in the area was massive. kama kawa, sisi tunaorithi we are not visionaries. We kill everything, kama Gen. Ariel Sharon
 
Kwani Kilombero wanafanyaje? Nimesikia Kiombero Illovo wanajenga Ethanol plant wakati Mtibwa walima miwa hawana pakupeleka. Kilombero wanawezaje na Mtibwa wanashindwa nini? This is an area which could expand out of propotion...again it lies iddle and soon the opportunity will be wasted.
 
That alternative could be the best...however, are the cans enough to run more than one factory in the same place? Pili, iliyokuwa Dakawa Ranch, sasa hivi amechukua nani? NAFCO Dakawa inamilikiwa na nani? In the past, the capitalization in the area was massive. kama kawa, sisi tunaorithi we are not visionaries. We kill everything, kama Gen. Ariel Sharon
Dakawa anaendelea kupanua mashamba yake muwekezaji. Kwa nini aongeze mashamba yake na miwa ya wakulima ipo? Nini hasa ufumbuzi wa matatizo ya wakulima? Nini wafanye? Hakuna kweli ufumbuzi?
 
Hivi hakuna uwezekano wa kuanzisha kiwanda kingine karibu na Mtibwa? Nasikia wakulima wa miwa wa kenya wanaendesha mercedes benz tokana na kilimo hicho hicho cha miwa.

Nasikia hauruhusiwi kuweka kiwanda kingine kama 100KM, mimi nadhani solution ni wakulim awenyewe wangeanzisha viwanda vidogovidogo vyao wenyewe.
 
Back
Top Bottom