Matatizo ya wanawake chanzo ni wanaume na matatizo ya wanaume chanzo ni wanawake

Matatizo ya wanawake chanzo ni wanaume na matatizo ya wanaume chanzo ni wanawake

Ali Nassor Px

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,384
Reaction score
3,926
Waungwana habari za muda, naamini tu salama na wazima wa afya, kama una changamoto pole na Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi na itapita.

Nimeandaa post hii kama sehemu ya kusaidia vijana wa kiume na hata wakike pia ili waweze kuishi na wenza wao kwa amani.

Nadhani kila mtu anajua kama bila wanawake wanaume wasingekuwepo na bila wanaume wanawake wasingekuwepo, kwahiyo maisha yetu ni ya muingiliano na mtegemeano mkubwa tu wa lazima.

Mwanaume ni kichwa cha familia, ila kichwa peke kimebeba mengi sana na kinahitaji usaidizi wa viungo vingine ili kifanye kazi kiusahihi kabisa.

Ila pia nataka mjue mwanamke ni mikono, maana yake iko kichwa cha familia kitasafishwa na mikono ili kipate kuona vizuri mbele. Shida inapokuja ni pale tu mikono baada ya kusafisha inachafua, aidha kwa kujua au kwa bahati mbaya.

Na anayeathirika zaidi ni mwanaume (kichwa) na siyo mwanamke (mikono) kwa sababu katika maisha ya dunia ya leo maisha ya mwanaume yapo chini ya mwanamke japo amri za uongozi anazitoa mwanaume.

Nusu na robo ya maisha tokea anazaliwa mpaka anakufa yapo chini ya himaya ya mwanamke. kula yake ya asubuhi ipo chini ya mwanamke, mchana jumlisha na usiku na anayelala naye pia ni mwanamke. hivyo kiumbe wa kike ana uwezo wa kufanya jambo lolote lile la kumdhuru mwanaume bila hata nguvu.

Ana uwezo wa kukuua kwa kukupa kile ukipendacho sana. maana anakujua zaidi kuliko unavyomjua yeye, anatumia hisia zaidi kwenye maamuzi yake ila wa kiume anatumia akili. Shida iliyopo mpaka leo hii mwanaume wengi hawajui wanawake wanataka nini.

Matumizi mabaya au mipango yoyote ya ile pesa ndani ya nyumba hayaendi kumuathiri mwanamke yanaenda kwa mwanaume. Huku mwanamke yakimuathiri kwa asilimia ndogo sana lakini janga linamdondokea mwanaume.

Lakini pia mwanaume anaweza akabeba maradhi au magonjwa kwa kuendekeza tamaa zake za kimwili. Unakuta mwanamke ni mpole na mnyenyekevu ila mwanaume ni mtu wa tamaa na anajiamini sana kwa kusikia dunia siku hizi inasumbuliwa na corona na anajisahaulisha kama ukimwi na magonjwa mengine yamekaa pale pembeni yanamtazama.

Ubaya wa mambo hayamuumizi yeye peke yake, yanaenda kumuumiza hadi yule ambae alitulia zake.

Hivyo kabla haujaoa au kuingia katika mahusiano jitahidi sana kumchagua mwenza ambae unafanana naye, na mna malengo mfanano katika maisha.

NB: Kaka una uwezo wa kujichagukia mkeila watoto hawana uwezo wa kujichagulia mama / dada una uwezo kujichagulia mume ila watoto wako hawana uwezo wa kujichagulia mama.

Jitahidi kuwachagulia na watoto wako mama au baba bora, usijichagulie peke yako tu!
 
Ungeshauri tu wazalishwe na kuachwa ila malezi ya mtoto yaendelee.
 
Ungeshauri tu wazalishwe na kuachwa ila malezi ya mtoto yaendelee.
Tatizo sio kuzalisha na kuacha tatizo utazalisha wangap swala la kutokuwa na sehem mmoja ya kumalizia mahitaj yako ya kimwil unawez ukazalisha watoto weng ambao wapo mbal mbal na maisha hauna ss... watoto wako watakuj kukuchkia na athar yake utaiona pale utakapo kuja kuwa haujiwez
 
Vijana wa hovyo watakupinga na kuanza kubishana.
Wameshaanza kubishana
 
Back
Top Bottom