Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MATAYARISHO YA KIPINDI MAKTABA NA FLOURANCE MAVIMBI TBC1
TBC1 wanatayarisha kipindi kuhusu majina ya mitaa waliyopewa viongozi wa Afrika katika jiji la Dar-es-Salaam mfano wa Kwame Nkrumah, Nelson Mandela, Sam Nujoma na Samora Machel.
Nikamuuliza mtayarishaji wa kipindi Bi. Flourance Mavimbi iweje TBC1 haitayarishi kwanza kipindi cha wazalendo wa Tanganyika waliopigania uhuru kuanzia enzi za Wajerumani?
Nikamweleza wako wazalendo wapigania uhuru ambao wamepewa mitaa na wako wengine wengi hawajapewa mitaa na wako waliopewa mitaa lakini vibao vya majina yao hayajawekwa.
Nikamweleza pia wako waliopewa mitaa kisha wakanyang'anywa mfano wa Saadan Abdu Kandoro.
Kigoma kulikuwa na kibao cha mtaa kumuenzi Saadan Abdu Kandoro.
Kibao hiki hakipo hivi sasa na mahali pake inasikitisha kimewekwa kibao chenye jina la mtu mwingine.
Mchango wa huyu mtu mpya kwenye kibao cha mtaa hakuna aujuaye.
Saadan Abdu Kandoro kapigania uhuru wa Tanganyika na ni katika watu 17 waasisi wa TANU mwaka wa 1954.
Mshume Kiyate, Max Mbwana na Tatu bint Mzee walipewa mitaa miaka mingi iliyopita hadi leo vibao vya mitaa waliyopewa haijabadilishwa.
Nilimshauri Bi. Flourance afikirie kufanya kipindi katika haya tuliyozungumza kwani itakuwa fursa nzuri ya kuhifadhi historia yetu iliyo kwenye hatari ya kupotea.