Match Analysis: Young Africans SC vs. MC Alger

Match Analysis: Young Africans SC vs. MC Alger

Tjedi

Member
Joined
Jan 12, 2025
Posts
15
Reaction score
100
FT: 0-0

Takwimu

Possession:
Hapa Yanga wali-dominated umiliki wa mpira kwa asilimia (69%) wakati MC Alger (31%).

Mashuti:
Yanga walikuwa na mashuti 18 wakati MC Alger's 3, Lakini hakuna lililozaa goli.

Big Chances:
Yanga walitengeneza nafasi 1 kubwa ya kufunga, wakati MC Alger hawakutengeneza nafasi yoyote.

Kona:
Yanga walipata kona 14 corner wakati MC Alger walipata 1.

Pasi:
Yanga walikamilisha pasi 539 mara mbili ya zile za MC Alger pasi 260.

Nidhamu:
Hawa jamaa walitumia nguvu sana. MC Alger walipata kadi za njano 3 wakati Yanga hawakuwa na kadi yoyote..

Pia angalia: News Alert: - FT: Yanga 0-0 MC Alger | CAF Champions League | Estadio Benjamin Mkapa | 18.01.2025


MY TAKE
---

Matatizo niliyoyaona:

1. Yanga wana udhaifu mkubwa kwenye ushambuliaji.
Licha ya kuutawala mchezo na kupata nafasi nyingi, Yanga walishindwa kuzigeuza kubwa magoli. Hii inathibitisha kabisa kwamba kuna tatizo la kushindwa kumalizia nafasi wanazotengeneza kwa kukosa washambuliaji makini kama F. Mayele

2. Ulinzi imara wa Mc Alger
MC Alger, licha ya kushindwa kuutawala mchezo na kuzidiwa mashuti lakini waliweza kulinda lango lao pia kipa alijitahidi sana.

3. Yanga wapiga mikwaju hawana madhara kabisa:
Yani licha ya kupata kona 14 lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo hii inaonyesha udhaifu mkubwa.

4. Kutumia nguvu kubwa
MC Alger walitumia nguvu kubwa sana na walifanya makosa mengi yaliyopelekea kadi 3 za njano. Hizi faulo zilikuwa zinavuruga sana harakati za Yanga.

---

Hitimisho:
Hii game Yanga walipaswa kushinda, walitawala mchezo lakini tatizo walikosa umakini wa kumalizia nafasi zao.

Mapendekezo;
Kocha anatakiwa kufocus na mazoezi ya kumalizia nafasi wanazotengeneza pamoja na kuwajengea ujasiri washambuliaji wakiwa mbele ya lango la adui.

kocha anatakiwa afocus na mazoezi na mbinu za kutumia nafasi za kona maana wanapata kona nyingi lakini wanashindwa kuzitumia.

Pia kocha anatakiwa ajiandae na mazoezi ya kutafuta nafasi zinazoachwa wazi kwenye safu ya ulinzi inapotokea wamekutana na timu zinazotumia nguvu kubwa kujilinda kama hawa Mc Alger.
 
Ahmed ally.jpg
 
Kadi 3 za njano ndo matumizi ya nguvu?

Kuna za kupoteza muda, nazo ni matumizi ya nguvu?

Nadhani hapo ndo ulipoharibu analysis yako!
 
Back
Top Bottom