Nimecheka sana kumwona paka aliyeingia uwanjani wakati Liver wanacheza na Spurs....Hata hivyo nimefurahi zaidi kwa jinsi ambavyo ametendewa kwa ukarimu na wadau wote.
Ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni, imebidi mpira usimame kwa dk kama 4 hivi kupisha paka aliyeingia uwanjani wakati mechi ikiendelea. Ingekuwa bongo, leo angeshikwa mtu uchawi.
Natamani huyu paka angekuwa huku bongo na angeingia uwanjani siku ya mechi ya simba na yanga.we wiki nzima habari hii ingetawala kwenye vyombo vya habari. Unakumbuka yule mbwa wa polisi alieingia uwanjani na kumkimbiza Haruna Moshi Bobani. Basi zilikuja taarifa kuwa yule mbwa alimfukuza Boban kwa sababu alikuwa ananukia MARIJUANA. Bongo kiboko!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.