Wick
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 8,313
- 12,170
Unaposhangaa ya United States of America (USA) kuweka mtu anayeitwa 'Designated Survivor' kila panapokuwa na State of Union ili kukitokea shambulio lolote basi huyo jamaa atakuwa raisi basi shangaa na linalotokea kule United Kingdom (UK).
Kila Malkia anapoenda kuhutubia pale Palace of Westminster lazima mbunge wao mmoja awekwe mateka (hostage) kwenye kasri la malkia (buckingham palace). Iwapo lolote likitokea kwa Malkia/Mfalme anapokuwa anahutubia basi askari wa malkia watalipiza na wao kwa yule 'mbunge mateka'.
Chukulia Magufuli anapoenda hutubia Bunge dodoma basi lazima mbunge mmoja awekwe mateka Magogoni, lolote likimtokea kule dodoma huyo mbunge atakayekuwa magogoni imekula kwake!.
Kabla Malkia hajafika bungeni huwa panakaguliwa mabomu bungeni wasije mlipua na wakaguzi wake wanalipwa kwa kupewa wine. Kingine Malkia hatakiwi ingia House of Commons hivyo akitaka hutubia anamtuma mtu anayejulikana kama Black Rod kwenda waita kuja House of Lords kusikiliza hotuba yake!.
Huyu Black Rod sasa akifika mlango wa kuingia House of Commons sio kwamba anaukuta umefungwa ni wanaufunga kwa nguvu mbele yake ili kumuonyesha nguvu yao halafu sasa atatakiwa kuugonga mara tatu (3) ndipo wamfungulie aingie waita!.
Hii ni kwa ufupi tu!..
State Opening of Parliament - Wikipedia
Jumapili njema!