Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 270
- 362
Serikali ya Rais Samia Suluhu imedhamira kwa dhati kuboresha viwanja vya ndege nchini kutanua wigo wa kibiashara ili kuinua uchumi nchini. Katika ya viwanja vya ndege vilivyofanyiwa Marekebisho nchini, kiwanja cha Mtwara matengenezo yake yamefikia 92% ambapo barabara ya kutulia ndege ilitanuliwa ili kuruhusu utuwaji wa ndege kubwa zaidi.
Miundombinu mingine iliyojengwa katika kiwanja hicho ni sehemu ya kisasa ya maegesho ya tax, sehemu ya kisasa ya kupaki ndege, sehemu ya kupaki gari za wageni pamoja na hifadhi kubwa ya maji ya akiba ya lita 200,000.
Bado matengenezo yanafanyika ikiwemo kuweka taa za kisasa katika barabara ya kuingia Airport, kuweka uzio wa umeme wa kisasa pamoja na baadhi ya njia za lami za ndani ya kiwanja cha ndege. Uwanja huo wa kisasa pindi utakapokamilika, utakuwa na uwezo wa kufanya kazi saa 24.
Hii itakuwa ni fursa kubwa sana kwa watu wa Mtwara na katia yote ya kusini kwani itachochea biashara. Lengo la Rais Samia Suluhu ni kuona Tanzania inasonga mbele na kuleta maendeleo yenye tija kwa watu.