Yoranda
JF-Expert Member
- Jan 9, 2020
- 341
- 338
kuhusuKwenye simenti ni bora tu ijenge kwa 42.5 kwani tofauti ni 1500 au 2000 na 32.5. Mimi ujenzi wangu wote natumia 42.5 kwa ajili ya uimara. Kwenye gypsum tumia ANDIKA wako vizuri na kwenye rangi jaribu kuwasiliana na wataalam ila kwangu naona PLASCON wako vizuri.
Tiles mspanish yuko vizuri ingawa hata hizi za China ukinunua grade nzuri zinapendeza na kukaa muda mrefu bila kuchoka. Mie nimeweka tiles mchina sakafu za ndani na sijawahi kujutia hata. Ingawa kwenye vyoo nilifunga za spain nilinunua Dar ceramic na walifungia kitaalam sana.
Bati pia zinatofautiana kuna zile zina chenga kama vigae za ALAF au DECRA zinavutia sana na imara. Kwenye finishing za vyoo nashauri uende duka moja liko Mtaa wa Samora la wamisri wana vitu imara sana na bei yao sio mbaya. Umeme funga tu TRONIC ila hakikisha ni original. Fan funga PANASONIC au USHA za wahindi hutojuta. Milango weka MNINGA ili ufe kabla yake maana inadumu vizazi na vizazi. Ila usipende kuweka vitu cheap kwenye ujenzi, Cheap ina-cost sana mwisho wa siku
Tiles Dar ceramic walikufungia wenyewe?