Mateso Makuu ya Kimyakimya Hayajifichi, Lakini Mtesaji ni Kama Hayamhusu

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
22,898
Reaction score
33,309
Sitaandika mengi hapa, kwa sababu ushahidi upo, kila mmoja anauona waziwazi.

Chungulia video yoyote inayomwonyesha katika kila hadhara mtu anayetakiwa sasa awe karidhika kwa kumkomoa mtu aliyemweka gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Zichunguze tu hizo video uone kama kuna alama yoyote ya furaha machoni mwa mhusika.

Kwa upande wa pili, tazama video yoyote ile ya anayeteswa, kila mara afikishwapo mahakamani kuhudhuria kesi
Wakati huu ilitazamiwa awe anageuzwa tu kama chapati inayoungua upande mmoja.

Mwangalie huyo mtu vizuri.
Kama angekuwa ni " mwigizaji" ili aonyeshe hali tofauti na aliyonayo ndani kwa ndani, ingefahamika tu

Gerezani siyo mahali pa mchezo.

Sasa jiulize, ni kitu gani hasa kinachomfanya huyu mtu awe na hali hii, tofauti kabisa na yule aliyetaka kumfanya awe na haliduni zaidi ya aliyonayo mtesaji.

Mimi ninayo nadharia ya kueleza hali hii; lakini hilo tuliache kwa siku nyingine.

Tazama video yoyote utakayopenda kuitazama, kati ya wawili hawa, utaona wazi ninachojaribu kueleza hapa.

Unatafuta njia ya kumtesa na kumkomoa mtu, lakini badala yake unateseka mwenyewe!

Huyu mtu alitegemewa hadi wakati huu angekuwa kanyooka kama rula
 
Umeanza lini kuwa mtunzi wa taarabu nyoka kama lura samia anateseka yeye badala ya kutegemea lissu angenyoka huko gerezan alikomswinda
 
Sitaandika mengi hapa, kwa sababu ushahidi upo, kila mmoja anauona waziwazi.

Chungulia video yoyote inayomwonyesha katika kila hadhara mtu anayetakiwa sasa awe karidhika kwa kumkomoa mtu aliyemweka gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Zichunguze tu hizo video uone kama kuna alama yoyote ya furaha machoni mwa mhusika.

Kwa upande wa pili, tazama video yoyote ile ya anayeteswa, kila mara afikishwapo mahakamani kuhudhuria kesi
Wakati huu ilitazamiwa awe anageuzwa tu kama chapati inayoungua upande mmoja.

Mwangalie huyo mtu vizuri.
Kama angekuwa ni " mwigizaji" ili aonyeshe hali tofauti na aliyonayo ndani kwa ndani, ingefahamika tu

Gerezani siyo mahali pa mchezo.

Sasa jiulize, ni kitu gani hasa kinachomfanya huyu mtu awe na hali hii, tofauti kabisa na yule aliyetaka kumfanya awe na haliduni zaidi ya aliyonayo mtesaji.

Mimi ninayo nadharia ya kueleza hali hii; lakini hilo tuliache kwa siku nyingine.

Tazama video yoyote utakayopenda kuitazama, kati ya wawili hawa, utaona wazi ninachojaribu kueleza hapa.

Unatafuta njia ya kumtesa na kumkomoa mtu, lakini badala yake unateseka mwenyewe!

Huyu mtu alitegemewa hadi wakati huu angekuwa kanyooka kama rula
Guilty conscience
 
Wamwachie tu, wampe fidia, wafanye reforms, watupe katiba na tume Huru. Tofauti ya hapo, wanaomshikilia, wataendelea kuteseka sana na kujutia maamuzi yao hadi watubu kwenye vitabu watavyo viandika wakitoka madarakani Kwa kuomba msamaha uchwara…
 
Nikuulize tu mkuu, 'mr pipa; hayo maneno umeyasoma wapi katika andiko hilo.

Mimi naweza kuwa "mtunzi wa taarab", na wewe je, utakuwa nani?
mimi karungu yeye mdudu mmoja hv anakiviliga kinyes kama mpira afu anasukumia miguu ya nyuma unajua nini dingili, pamoja sana
 
"It's me against the world "
Hakuna mtu timamu anaeweza kua na furaha na amani moyoni.
Ukifikiria kumfanya mateka mtu anaependwa na wengi,
Watu wamekufa,
Wengine hawajazikwa,
Wengine wametupwa TU.
Hapa hata taahira atakua na huzuni TU.
 
Kauli za kipuuzi za kujifariji, Lissu mwenyewe alishasema jela sio kuzuri..
 
Back
Top Bottom