Mathayo 15 (1- 39) Kiingiacho kinywani hakimtii mtu najisi?

Mnapenda sana kutafutiza vifungu vya kujifariji, hulazimishwi na mtu awaye yeyote….. tuseme ndo umesoma leo hilo fungu kabla ya leo ulikuwa unaishije?
 
Sometimes the Bible tends to be contradictive, bt it all depends on the reader's comprehension.
 
Mnapenda sana kutafutiza vifungu vya kujifariji, hulazimishwi na mtu awaye yeyote….. tuseme ndo umesoma leo hilo fungu kabla ya leo ulikuwa unaishije?
Niliaminishwa kuwa, kiingiacho sio najisi ila kitokacho hivyo nikajua mtu anaruhusiwa kula kila kitu. Ila baada ya kusoma mwenye Mathayo 15 (1-39), nimepata ujumbe tofauti kabisa kuwa haina uhusiano wowote na ulaji wa vyakula
 
Niliaminishwa kuwa, kiingiacho sio najisi ila kitokacho hivyo nikajua mtu anaruhusiwa kula kila kitu. Ila baada ya kusoma mwenye Mathayo 15 (1-39), nimepata ujumbe tofauti kabisa kuwa haina uhusiano wowote na ulaji wa vyakula
Sidhani hata kama umeelewa hiki ulichoandika hapa, nikuache kwa amani tu…. uko sahihi.
 
Fundisho hilo pia limenenwa katika Injili nyingine 3 ikiwemo katika Marko 7:13-19 na mstari wa 19 unasisitiza kubwa kwa kusema hivyo alivitakasa vyakula vyote. Hii inamaanisha kuwa, Yesu alikuwa anauchangamanisha/uunganisha tena Uyahudi na mataifa yote ambayo hayakuwa yamewekewa Sheria kuhusu vyakula.

Kimsingi kwenye Biblia kuna nyakati 4 zihusuzo vyakula.
1. Kipindi cha kwanza ni cha Adam. Hii ni baada ya uumbaji na watu wote waliozaliwa na kuishi kabla ya gharika. Hawa Mungu aliwapa chakula kitokanacho na Mimea. Mwanzo 1:26-30.
2. Kipindi cha pili ni kipindi cha Nuhu na wanadamu wote walioishi wakati wake. Wao walipewa Nyama ya kila kiumbe kilichopo duniani na walikatazwa damu. Mwanzo 9:1-5.
3. Kipindi cha tatu ni kipindi cha wana wa Israel. Hiki kiliwahusu wayahudi pekee ambao walipewa sheria na torati ili wajitiishe kwayo. Hawa walichaguliwa/pewa nini cha kula. Lawi 11:1-33
4. Kipindi cha nne ni cha Yesu katika Jinsi ya mwili. Hapa anakuja kuwachangamanisha Wayahudi na Mataifa. Anavitakasa vyakula vyote tena. Marko 7:13_19 inaeleza vizuri na hata Petro alielezwa hilo katika Marko 10 na ndio maana wanafunzi (mitume) waliwasisitizia mataifa walioamini kujitenga na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu na sio nini cha kula na nini cha kutokula.

Infact, we maamuma endelea tu kula nguruwe maana hata kitabu kilichotokana na "Wahiya wa mapepo" kwa muddy (56) mme wa bi. Aisha(9) hakikatazi kula kitimoto.
 
Umeandika vizuri sana, ila mwisho ndio umeharibu.
 
Mwisho umeharibu.Wengi tumesoma andiko lako,tukafikiria huwenda ukawa ni mchungaji,padre,shemasi,mzee wa kanisa,kakini mwisho umeharibu,kuelezea kisichohusiana na mada.
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Ukristo ulioibuka juzi ndio unachanganyikiwa! Ila wenye uzi wa mafundisho na mapokeo toka mitume hili ni kitu kidogo! Hapo Yesu anasema HAKUNA kitu unachoweza kula (kinacholika) kinaweza kukutia unajisi! Kwamsisitizo anasema HAKUNA kitu ambacho kwa asili yake ni najisi bali unajisi ni yale yakutokayo maana ndio yaliyoujaza moyo wako!

Ila siku hizi ndio watu wamekazia vitu kama mfano pombe ni dhambi! Hii ni kusoma bible kwa kuchagua mstari fulani bila kulisoma fundisho lote na kuelewa mpango wa Mungu!

Mfano hapa Biblia inatoa sifa ya shemasi na haimkatazi kunywa pombe.... 8 Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu.
1 Timotheo 3:8

Kula kwa kiasi usiwe mlafi maana ulafi ni mzizi wa dhambi, kunywa kwa kiasi maana ulevi pia ni mzizi wa dhambi! Tukienenda kwa kiasi tutakuwa salama.
 
Umeandika vizuri sana, ila mwisho ndio umeharibu.
Hahaaaa, nimeharibu nini? Unajua tunacheza kulingana na mdundo wa ngoma. Huyo muanzisha thread ni muislamu na hajaandika kwa lengo la kujifunza ila kukosoa ukristo na ndio maana hapo mwisho nimeeleza hilo japo ni kweli quran haikatazi kula nguruwe na kama wewe ni muislamu, naomba andiko linalokataza kula kitimoto toka kwenye quran.
 
Mwisho umeharibu.Wengi tumesoma andiko lako,tukafikiria huwenda ukawa ni mchungaji,padre,shemasi,mzee wa kanisa,kakini mwisho umeharibu,kuelezea kisichohusiana na mada.
Hahaaaa, pole na nisamehe mkuu nilikuwa nataka kumtoa mchezoni mwandika thread japo najua hakuandika kwa nia ya kujifunza ila kukashfu ukristo na hiyo ndiyo changamoto kubwa ya kizazi hiki.
 
Kula bila kunawa uharishe mpaka dhambii, kipindi Cha wafarisayo na wasadukayo masuala ya infections hayakuepo😃😃
 
Ukielewa nini maana ya chakula na ni kipi kiliwe kipi kisiliwe huwezi hangaika na mengine.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ndo maana huwa wanasema kunywa kistaarabu..

Sent from my MHA-L29 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…