Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Ni ngumu kuzungumzia fasihi ya kiswahili bila kumzungumzia Mathias E. Mnyampala. Mnyampala alizaliwa mwaka 1917 huko Dodoma akiwa ni Mgogo. Baba yake alikuwa ni mfua chuma na alimiliki ng'ombe wengi ambao Mathias ndiye alikuwa mchungaji. Mwaka 1931. Akiwa kama na miaka 14-15 aliozwa mke!
Baadaye shule ilianzishwa kijijini kwao. Naye akaomba kuandikishwa. Waalimu wakamwambia wewe tayari una mke, hatuwezi kukupokea. Lakini hakukata tamaa. Kila darasa(la chini ya mwembe) lilipoendeshwa naye alihudhuria. Siku moja mwalimu alijaribu wanafunzi wake kusoma habari fulani, wengi walibabaika. Akamwambia na Mathias naye asome maana amekuwa akihudhuria kila siku. Mathias akasoma vizuri sana, basi mwalimu akaamua kumuingiza rasmi.
Baadaye akaenda shule ya misheni kujifunza elimu na dini. Alienda na mkewe. Ilipotakiwa kuendelea mbele akachaguliwa, lakini alishindwa kwenda sababu mke wake alikataa kubaki akiishi misheni.
Basi hapo akaendelea kujitafutia elimu yeye mwenyewe huku akifanya 'tempo' za kufundisha. Akaanza na kujifunza kiingereza huku akilipa watu wamfundishe.
Elimu hii ilimuwezesha kufanya kazi nyingi sana. Lakini mara nyingi alipata changamoto maana hakuwa na vyeti vyovyote vilivyomuonyesha kuwa kasoma. Lakini kazi yake nzuri ilikuwa inamfanya agombaniwe kila kona na mabosi wa kikoloni wakati huo. Alifariki mwaka 1969.
Mathias E Mnyampala ni shujaa wa Elimu.