matibabu kwa njia ya kompyuta

matibabu kwa njia ya kompyuta

Smile

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
15,347
Reaction score
11,619
Ni ramli ya kizungu au ni nini?

Sometimes nikiwa katika kipindi cha ovulation kiuno/nyonga huwa inaniuma sio sana lakini.especial kama ni ovary ya upande wa kushoto, sasa juzi ikanitokea nikamueleza best yangu sasa tukiwa njiani tukaona clinic ya wanawake na uzazi nikamwambia tucheki maeneo yetu kama yapo vizuri siku hizi magonjwa mengi basi tukaenda pale kumuona dokta.

Kupima ni 50, wakasema kupima ni kwa computer basi tukalazwa kitandani pale tukavuliwa vichupi vyetu vikatupwa nje huko
tukashikishwa mouce ya kompyuta dkk mbili tatu tukaambiwa tayari tufate majibu kesho yake eti system ina load matatizo yetu
kesho yake hao tukaenda.

Maweeeeeeeee mimi nikaambiwa eti nina cyst ndogooo ndo inaanza kujitokeza matibabu laki mbili,nikawaambia mi nina insurance nitaenda kununua dawa sehemu ingine wakasema kama ni hivo sitapona ila niliogopa kweli. Nikaenda kwa dokta mwingine akaniambia sina chochote akanieleza na sababu za kuumwa kwangu.

Shoga yangu nae kidogo afe pressure maana aliambiwa mlango wa kizazi upo wazi so unatakiwa ufungwe yaani ngoja narudi.
 
Tehe tehe tehe, wanapiga ramli hata kwenye mambo serious namna hii?
 
Hii kitu ipogo hata huku Same kuna hosp. moja hv ya private ukienda kupima wanakuambia ugonjwa tofauti na ulionao na hawataki uende kutibiwa kwengine ili tu wakukombe viela vyako ukafie mbele
 
Hii kitu ipogo hata huku Same kuna hosp. moja hv ya private ukienda kupima wanakuambia ugonjwa tofauti na ulionao na hawataki uende kutibiwa kwengine ili tu wakukombe viela vyako ukafie mbele
yaani acha tu uchungu wa mwana aujuae mzazi tu!
 
Wajinga ndio waliwaoo!

:biggrin::biggrin::biggrin::biggrin:
 
Back
Top Bottom