Kama unattzo unaweza usfke india na likatbka hap hapa tanzania kwa maelezo zaid piga number 0712757453
Mkuu uko sahihi,suala hili huwa linanisikitisha sana,kasumba hii ya watu kufikiri kwamba India ndio suluhisho la magonjwa yao imeanza kimasikhara sana,sasa hivi viongozi wa serikali na watu maarufu wengine hizi ndio fikra zao hasa pale wanapopata ugonjwa wa cancer.
Watu maarufu hawa wakipata cancer tu basi fikra zao kwanza kabisa ni kwenda India,pamoja na kwamba mimi binafsi sijawahi kusikia mtu aliyepona cancer moja kwa moja baada ya kutibiwa huko India.
Angalizo:
Sina nia ya kudharau mtazamo au fikra za mtu yeyote yule kuhusu maamuzi ya wapi kwa kwenda kutibiwa.Bali nasikitika kwamba watu wamekosa taarifa za kutosha au uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kiafya hasa katika magonjwa sugu kama vile cancer,kisukari na autoimmune.Chanzo cha ukosefu wa uelewa huu ni mifumo mibovu ya afya na uvivu wa watu kujisomea vitabu au kufuatilia masuala ya afya kwa njia nyinginezo ikiwemo mitandao,majarida na semina.
Hali hii ya ukosefu wa uelewa sahihi wa masuala ya afya ndio ilifanya watu wengi sana wamiminike kwa babu wa Loliondo kipindi kile.Watu wamekata tamaa na kupoteza matumaini kabisa kiasi cha kuona kwamba India ndio suluhisho la matatizo yao.
Ushauri:
Nashauri watu watumie muda wao vizuri kudadisi kuhusu masuala ya afya kwa njia mbalimbali zikiwemo zile za mitandao kama JF.Watu wawe na tabia ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu afya kwa kuwa mahali kama JF kuna watu wenye uelewa na uzoefu wa aina mbalimbali katika masuala haya.India sio suluhisho katika magonjwa kama cancer,labda magonjwa mengine,hivyo tuepuke kupoteza gharama kubwa za matibabu bila mafanikio.
Hivyo nakushauri mleta mada/muulizaji uweke wazi tatizo lako(kama inawezekana) ili wenye uwezo wa kukupatia ushauri/tiba sahihi wakupatie.
Natanguliza shukrani kwa kunielewa.