Matibabu nchini India

Matibabu nchini India

mrbambi

Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
19
Reaction score
0
Habari zenu wakuu, naomba kujua kuhusu chanjo ya homa ya manjano kwa wanaosafiri ni wapi inatolewa na kwa siku gani na gani.

Pia kwa mwenye kujua hospitali ya Apollo iliyoko Chennai nchini INDIA gharama zake na huduma kwa pamoja.

Na jinsi ya kupata VISA pia kwa ajili ya kwenda kutibiwa.
 
Kama unattzo unaweza usfke india na likatbka hap hapa tanzania kwa maelezo zaid piga number 0712757453
 
Kama unattzo unaweza usfke india na likatbka hap hapa tanzania kwa maelezo zaid piga number 0712757453

Mkuu uko sahihi,suala hili huwa linanisikitisha sana,kasumba hii ya watu kufikiri kwamba India ndio suluhisho la magonjwa yao imeanza kimasikhara sana,sasa hivi viongozi wa serikali na watu maarufu wengine hizi ndio fikra zao hasa pale wanapopata ugonjwa wa cancer.

Watu maarufu hawa wakipata cancer tu basi fikra zao kwanza kabisa ni kwenda India,pamoja na kwamba mimi binafsi sijawahi kusikia mtu aliyepona cancer moja kwa moja baada ya kutibiwa huko India.

Angalizo:
Sina nia ya kudharau mtazamo au fikra za mtu yeyote yule kuhusu maamuzi ya wapi kwa kwenda kutibiwa.Bali nasikitika kwamba watu wamekosa taarifa za kutosha au uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kiafya hasa katika magonjwa sugu kama vile cancer,kisukari na autoimmune.Chanzo cha ukosefu wa uelewa huu ni mifumo mibovu ya afya na uvivu wa watu kujisomea vitabu au kufuatilia masuala ya afya kwa njia nyinginezo ikiwemo mitandao,majarida na semina.

Hali hii ya ukosefu wa uelewa sahihi wa masuala ya afya ndio ilifanya watu wengi sana wamiminike kwa babu wa Loliondo kipindi kile.Watu wamekata tamaa na kupoteza matumaini kabisa kiasi cha kuona kwamba India ndio suluhisho la matatizo yao.

Ushauri:
Nashauri watu watumie muda wao vizuri kudadisi kuhusu masuala ya afya kwa njia mbalimbali zikiwemo zile za mitandao kama JF.Watu wawe na tabia ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu afya kwa kuwa mahali kama JF kuna watu wenye uelewa na uzoefu wa aina mbalimbali katika masuala haya.India sio suluhisho katika magonjwa kama cancer,labda magonjwa mengine,hivyo tuepuke kupoteza gharama kubwa za matibabu bila mafanikio.

Hivyo nakushauri mleta mada/muulizaji uweke wazi tatizo lako(kama inawezekana) ili wenye uwezo wa kukupatia ushauri/tiba sahihi wakupatie.

Natanguliza shukrani kwa kunielewa.
 
Mkuu uko sahihi,suala hili huwa linanisikitisha sana,kasumba hii ya watu kufikiri kwamba India ndio suluhisho la magonjwa yao imeanza kimasikhara sana,sasa hivi viongozi wa serikali na watu maarufu wengine hizi ndio fikra zao hasa pale wanapopata ugonjwa wa cancer.

Watu maarufu hawa wakipata cancer tu basi fikra zao kwanza kabisa ni kwenda India,pamoja na kwamba mimi binafsi sijawahi kusikia mtu aliyepona cancer moja kwa moja baada ya kutibiwa huko India.

....Natanguliza shukrani kwa kunielewa.
Una cancer au unamfahamu mtu mwenye cancer?
Unatafuta matibabu?

Unaweza kuni-pm ili nikusaidie au nikupe taarifa zitakazokusaidia.
 
Back
Top Bottom