Amina Thomas
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 272
- 130
Kuna wakorea ambao wanatibu maradhi mengi sana kwa kutumia mazoezi pamoja na mashine za umeme hapo mwenge karibu na ITV mama yangu anaenda huko kila siku.
Hua namsikiliza kwa makini sana kuhusu matibabu hayo, anaondoka saa 12 asubuhi kila siku, anarudi saa tisa u nusu kwa sababu watu ni wengi sana kiasi kwamba wengine wanaenda saa kumi alfajiri.
Wanaanza kwa mazoezi ya viungo halafu wanaenda kwenye hizo mashine za umeme, wanavaa suruali na t. shirt nyeupe tu. mashine hizo zina toa joto ambalo wanasema linatibu kisukari, busha, ugumba, u bubu, kupooza, vivimbe vya kila aina vikiwemo vya saratani, pamoja na magonjwa mengi sana mengineyo.
Kwa upande wangu naona imekaa ki loliondo maana kila siku watu kibao wanatoa ushuhuda. halafu ni buree!. hivi serikali inafahamu kuhusu hili?

Habari zenu wannajamvi..naomba kuuliza juu ya hawa wakorea wenye kituo cha seragem..je? zile mashine zao zinasaidia?. Yoyote mwenye uthibitisho wa kuona aje hapa anihakikishie..
Nina binti yangu ana 1.8 year.. alipata homa ya uti wa mgongo kwahiyo ikimsababishia celebral palsy. so mpaka sasa hawezi kukaa, shingo haijakaza, hawezi kushika kitu chochote..huwa nampeleka kwenye physiotherapy muhimbili na CCBRT. Improvement ipo kwa mbali namimi sijakata tamaa bado naamini ata improve.
Sasa nimesikia kuwa hawa seragem wana mashine nzuri zinazotibu kupitia uti wa mgongo kwa hivyo mnijuze kwa wale mliowahi kuona kwa macho kwa jirani. ndugu, jamaa, rafiki ama wewe mwenyewe..