BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Daktari Bingwa wa Upasuaji Ubongo kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dkt. Laurent Mchome amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la Wagonjwa wa Kiharusi nchini na wanaokutwa na tatizo hilo sana ni watu wenye miaka 40 na kuendelea.
Akielezea utaratibu wa gharama za Matibabu ya Ugonjwa huo ambao mara nyingi huhusisha upasuaji mkubwa na mdogo, Dkt. Respicious Boniface ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI amesema matibabu ya Ugonjwa huo yanagharimu fedha nyingi ambapo gharama ya chini sana ni Tsh. Milioni 5 na inaweza kufikia hadi Tsh. Milioni 15 kutegemea na aina ya Upasuaji.
Hata hivyo ameeleza kuwa gharama hizo bado ni ndogo kulinganisha na matibabu yanayofanyika nje ya nchi ambako gharama hufikia Tsh. Milioni 30 hadi 60.