Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!


Mchakamchaka.....chinja...mchakamchaka.....chinja akija mcc....chinja akija kamba....chinja akija mchela......chinja.................

Ohhhh ishakuwa taabu Ruandis is at corner, just timeframe!
 
Sisi watu huru tunaomba kuuliza maswali
mtu uko kwenye computer ni kipi kimekufanya ujiridhishe kuwa ccm wamewaibia chadema kura??
 
Aleluya!

Ninachoona mimi CCM watangaze Utawala wa Chama Kimoja kwani hawataki kushindwa!
Kulikoni kwahadaa mataifa kuwa Tanzania kuna Democrasia ya Vyama vingi! Period!

Mungu wetu na atusaidie!

Pale Kenya ilikuwa vipi mkuu, sikuzote cancer huanza taratibu
 
Kikwete ni dikiteta big time. Ameanza kuonesha makucha yake. Subiri uone kitakachofuata baaada ya kushinda ngwe ya pili. Nchi itageuzwa kuwa na utawala wa kijeshi huku wakitumia sheria za dini (jina mfukoni).
 
Mkuu Invisible,

Mimi naona unisaidie, hivi haya matokeo uliyokuwa unabandika ulikuwa unayatoa wapi? Una uhakika 100% kwamba yalikuwa ni matokeo ambayo yamebandikwa vituoni? isije ikawa ni matokeo ambayo unapewa na wafauasi wa vyama ambao wako tayari ku spin jambo lolote.

Ningependa kujua nini kimetokea, na je ni kweli kwa kura za kila kituo CHADEMA walishinda?

Kwenye mambo ya uchaguzi inatakiwa kuwa makini sana kabla ya radio/TV kutangaza ushindi.

Kama ni kweli CHADEMA walishinda na wameibiwa basi nawaonea huruma. Isije ikawa kama ya Iran ambayo hata watu wa West wenyewe wanaamini huyu rais ameshinda ila vijana walikuwa wanataka mabadiliko wakawa tayari kutumia kila njia ili ku take advantage of the situation.

Binafsi ningependa kweli kujifunza CCM wanatumia mbimu zipi kuiba? Hivi hakuna wana CCM hapa wanaotaka ku spill the beans? Yaani vyama vya upinzani mmeshindwa kabisa kuiba siri za CCM?
 
Tulia............Tafakari.........Mmiliki wa Timu ni Refa, wewe unatarajia nini hapo mbona mnajifanya mnashang'aa na wakati kilichokuwa kinatokea hahitaji ukawa na degree kukiona. Na mkubali sana nyerere aliwajua watu wake nakuambia hii cheni ya ujinga Tanzania itabaki hivyo hivyo
Mpaka Yesu Aje au Mtume!
 
Na sasa wameanza kuleta mambo ya kidini ili kupoteza malengo yao ya kishetwani.
Yaani utawala wa Kishetani kazi yake kubwa ni kudhulumu watu hata kile kichache za maskini kama vile uchaguzi wa biharamulo vile
 

Mkuu ni kigezo gani umekitumia kuamini hivyo ,mfano hukuwepo B'mulo lakini bado unaamini umeibiwa ni stds zipi mnatumia?

Mnipe Desa mnalotumia na mimi nijifunze jinsi stds hizo zinavyotumika.
 
Mkuu ni kigezo gani umekitumia kuamini hivyo ,mfano hukuwepo B'mulo lakini bado unaamini umeibiwa ni stds zipi mnatumia?

Mnipe Desa mnalotumia na mimi nijifunze jinsi stds hizo zinavyotumika.

hivi limekaaje hili la wakurugenzi wa halmashauri/miji waajiliwa wa serikali za mitaa zilizo chini ya ofisi ya waziri mkuu kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo? Je kweli tume ya Uchaguzi itakuwa huru hapo? Kuna makamishina wangapi kwenye Tume ya uchaguzi toka vyama vya upinzani?
 
Yaani utawala wa Kishetani kazi yake kubwa ni kudhulumu watu hata kile kichache za maskini kama vile uchaguzi wa biharamulo vile

Na bado wakitoka hapo wanaenda kusali na kuswali misikikitini na makanisani huku wamevaa misuti na mitai na wengine mikanzu kwa unafiki mkubwa kabisa.

Utawaweza hawa, watangaze tu kuwa Tanzania ni nchi ya chama kimoja cha siasa.
 
Kuna member kadhaa wamesema haya yangetokea. CCM itakua nyuma na ghafla dakika ya mwisho mnaambiwa kuwa wameshinda sijui kata gani na kuchukua uongozi. Kweli politics in Tanzania is predictable.
 
Tanzania si nchi ya amani tena,kwani sasa hivi mioyo ya watanzania haijatulia kwa sababu ya ccm,wameshindwa kusoma alama za nyakati kuwa Watanzania wa sasa si wa miaka ya 80 na 90,taratibu fundo la uchungu wa watanzania linajaa,ipo siku litafumuka na hapatakalika.Hakuna aliyezaliwa akamilikishwa amani,amani inatafutwa na inatunzwa.

Mi inaniuma sana.
 

Mkuu Mtanzania tupo pamoja, hizi ndiyo hoja zinazotakiwa kwasasa.
 

Inawauma wengi tu, sio wewe peke yako. It is time people demand for ammendment in the constitution, coz kwa hii iliyopo wapinzani hawawezi kushinda hata kwa 25% tu.

ISSUE NI MAREKEBISHO YA KATIBA, that's the solution.
 
Inatia huruma sana kuona chama hicho kikongwe kinajigamba kuwa wanashinda kumbe ushindi ni wa kishetani kama hivi tunavyoona kuwa ni ushindi wa nguvu za giza huku Tume ya Taifa ikibariki maovu yao
 

Bona hapo hapo Kabuye alichukuwa kutoka TLP,hata hivyo bado hujajibu swali.
Ni kitu gani unaamini kwamba kuna wizi umetokea.?Wanaoleta habari za wizi kumbuka nawo wako biased na chama chao.Sasa ni kigezo gani kinatumika kuutambuwa wizi ?

Waliko B'mulo kuna vurumai yoyote kati ya wananchi na ffu?? ama vurumai iko kwa viongozi wa chama kutoka dar?
 
Wote wamepanda ndege wamerudi bongo!! Hakuna jipya huko mzee wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…