Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

True, du... kazi ipo, yaani mwili unatetetetemeka sassaaasasa hiiiiviii... siiiieelewi...

Pamoja na yote bado naipongeza CHADEMA!!!
Ni kweli mkuu,CHADEMA wanahitaji pongezi sana kwani kwa kipindi kifupi wameonesha wana mikakati madhubuti sana ya kukifanya chama chao kiwe chenye nguvu na kuwa tishio kwa CCM,cha msingi wasibweteke na mafanikio haya,wajiimarishe zaidi(hasa vijijini maana matokeo ya chaguzi za karibuni yaonesha wanashinda sana mijini kuliko vijijini),wawe na mikakati ya muda mrefu...wasije wakapata anguko kama lile la CUF ambao kimsingi kwa sasa WAMEFULIA
 

mhhh........
 
mhhh........
Habari ndo hiyo..Mtaji wa CCM siku zote uko vijijini.Swali la msingi ujiulize je CHADEMA wana mtandao wa kuanzia kwenye Mashina,Matawi,kata,Wilaya,Mkoa na Taifa kama ilivyo kwa CCM?,vipi kamaw angejiimarisha kuanzia shinani si wangekuwa tishio kwa CCM kuliko sasa??,bado hawajachelewa,muda wanao wa kutosha
 
Tume ya uchaguzi inateuliwa na raisi. Halmashauri za wilaya na mikoa zipo chini ya mtu anaye teuliwa na raisi. What do we expect? Kwa nini waache kumtumikia boss wao? Tunahitaji mabadiliko ya katiba.
 
Wanahitaji pongezi na tena hasa hata watu ndani ya JF kwa masomo yao na Timu yote ya Kampeni ya CHADEMA!! Kama kweli Uchaguzi unakuwa huru na haki CHADEMA wangeshinda uchaguzi huo.Maan kila aina ya Kampeni na Vitisho vilitawala katika Kampeni
 

Inategemea unaongelea vijiji gani ...... Chadema ina mitandao hadi vijijini (mfano - Tarime ambako chadema inaongoza halmashauri). Chadema kwa sasa labda (msisitizo kwenye labda) inahitaji wananchi ngangari kama wa Tarime ambao walisimama kidete kuhakikisha kuwa msimamizi wa uchaguzi habadilishi matokeo ya uchaguzi.

Mengine yote ni ...... well .... haishangazi maana miafrika mingi ni minafiki na ndivyo ilivyo.
 
Sasa wewe ngoja waanzishe haya mambo ya ajabu maana sasa tumeona kuwa Tatizo sio vijijini tatizo ni Watu na Tume ya taifa ya uchaguzi siyo huru hata kidogo inatumiwa na watu. Sina Imani na tume ya kivuitu wa Tanzania jamani
 

hata vijijini wanashinda hiyo ni janja ya ccm

eti biharamulo ni mjini, ccm wanashinda ndani ya vijiji???

walisema majimbo ya vijijini ccm ndio wanashinda, biharamulo ni jimbo la kijijini, chadema walipofika jimbo la kijijini ccm wanasema wao wanashinda ndani ya vijiji na sio wilayani, chadema wakifika vijijini ccm watatuambia wanashinda kwenye kata, wakifika kwenye kata tutaambiwa kwenye vitongoji, wakifika kwenye vitongoji tutaambiwa mitaa, wakifika kwenye mitaa tutaambiwa kwenye kona
 

Watakuambia kuwa Tarime ni mjini. Inatafutwa sababu tu ya kuhalalisha status quo. Hali inasikitisha sana.

NOTE -- kuna mabadiliko makubwa sana yametokea kwenye hii thread..... hata JF? nimechoka kabisa.
 
semilong Pamoja nakusononeka sana leo jinsi CCm wanavyodhoofisha demokrasia,ukweli ni haya uliyosema wakitoka kwenye kona watasema chumbani au kisimani au mtoni ,Tanzania nchi yetu tunayoipenda sana imewekwa rehani na majambazi wezi wa kura CCM,tumwombe sana Munhu kuwe na amani hata kwa miaka miwili tuu ijayo wanaashiria shali,kama bloger mwingine alivyosema hakuna kifaru,wala bunduki wala grenade lakuua watu milioni 38-40
 
Jamani mbona tunachanganyana hivi sasa kwani gazeti la tanzania daima wameandika kuwa chadema wameshinda,mimi naona wameshinda kwani nao wamesema kuwa chadema imepata asilimia 51 kama ilivyowekwa hapa jana usiku.
 
Chanzo CCM wameshinda Biharamulo! haya sasa zimeni chereko chereko zenu mrudi kwenye nyimbo zenu za kawaida mmeibiwa!

The one who laughs last, laughs the best!
Masatu una hakika? soma Tanzania Daima la LEO.
 

sensa za TZ zote zinasema mjini kuna watu wengi lakini ikifika wakati wa uchaguzi vijijini ndio kuna watu wengi
 
Hapa tulipofika tunatakiwa tuende Kenyan style, bila hivyo hawa CCM wataendelea kutufanya sisi wananchi ni mazezeta. So, the next step: let's radicalise our politics. Ustaraabu wanasiasa wanaotawala Africa hawawezi.

Nashangaa hapa ndani kuna mibaba mizima inashangilia ushindi wa ccm, tena bila aibu, sijui ni ushindi gani huo, shame on you akina Masatu!!

Nawapongeza CHADEMA, wanapambana katika mazingira magumu mno, lakini hawakati tamaa.
 
C'mon mkuu,hope hujanielewa kabisa,CHADEMA kuongoza halmashauri Tarime kusiwafanye wabweteke hata kidogo...Cha msingi kama wana nia ya dhati kabisa ya kuwa chama mbadala(kama wanavyojiita)wajiimarishe/wajitangaze Tanzania nzima(mpaka visiwani) kama ilivyo kwa chama tawala-CCM...Wajiimarishe kuanzia ngazi ya shina(Tanzania nzima).....kuhusu unafiki kabla hujawahukumu wengine kwa kuwaita wanafiki jiangalie wewe kwanza mkuu
 
CCM yaibuka kidedea Biharamulo Magharibi; Chadema walalamika

Hii heading ya thread ina pande mbili (a) CCM kuibuka kidedea (b) Chadema walalamika

Hoja: Sijaona mahali popote panapoeleza malalamiko ya chadema. I mean ninapenda kujua hayo malalamiko ya chadema yakoje?
 
Ligi za nini wakuu,mimi nimetoa ushauri tu jamani,kwamba kama CHADEMA wanataka kuwa chama mbadala wanapaswa wajiimarishe kwa kuwa na mtandao unaoanzia katika ngazi ya shina na wajisambaze Tanzania nzima(katika kila kijiji) kama ilivyo kwa CCM ambayo ina mtandao Tanzania nzima unaoanzia ngazi ya Shina,Tawi,Kata,Wilaya,Mkoa hadi Taifa,Hapo ndo watatoa upinzani wa nguvu hasa,pia wawe na mipango ya muda mrefu yenye mwelekeo wa ushindi badala ya kutegema chaguzi ndogo tu(maana hata CCM nao sasa hivi washaona hali ilivyo so wanafanya maandalizi ya nguvu hasa kukabiliana na hao CHADEMA)...Huu ni mtizamo wangu tu mkuu...pa1
 
Oh well.. we have been here before.. and we are going to be here again. The circle of illusion keep on spinning.. What was, is still is and will surely be..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…