Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!


ohh yeah ni mtazamo wako ... na haina maana kuwa wewe unamiliki ukweli kuliko wa huyo mwenzako unayemshangaa hapo juu.
 
Nyie akina Invisible mbona mnachachawa na kubadilsha heading ku sympathise na Chadema. JF mambo shaghala baghala bora mtangaze wameshinda chadema labda tutakuwa na mtirirko mzuri

kuna watu hawawezi kulala bila kumwaga vilio hadharani.
 
C'mon mkuu,hope hujanielewa kabisa,

hell yes, nimekuelewa kabisa ulivyosema kwa CHADEMA haiko vijijini.

CHADEMA kuongoza halmashauri Tarime kusiwafanye wabweteke hata kidogo...

una hakika kuwa CHADEMA wamebweteka?

Cha msingi kama wana nia ya dhati kabisa ya kuwa chama mbadala(kama wanavyojiita)wajiimarishe/wajitangaze Tanzania nzima(mpaka visiwani) kama ilivyo kwa chama tawala-CCM...Wajiimarishe kuanzia ngazi ya shina(Tanzania nzima).....

Unaonaje kama nawe ukiungana nao ili uwasaidie kujitangaza nchi nzima?

kuhusu unafiki kabla hujawahukumu wengine kwa kuwaita wanafiki jiangalie wewe kwanza mkuu

Katika hili, hata sikushangai.
 
ohh yeah ni mtazamo wako ... na haina maana kuwa wewe unamiliki ukweli kuliko wa huyo mwenzako unayemshangaa hapo juu.
Hata wewe nakushangaa na nitazidi kukushangaa kwa mawazo yako haya MACHAFU ya kutishia kumwaga DAMU kisa CHADEMA imeshindwa uchaguzi Biharamuro...Lol...Haki haidaiwi kwa Mapanga,marungu,Bunduki wala Silaha yoyote ndugu.......Unafikiri ukimwaga hiyo damu ndo CHADEMA itashinda?,thubutuuuuuuuu...Ama na nyie mnataka muanze yale mambo ya Ngangari na Ngunguri au Jino kwa Jino??,mkianza hivyo ndo mtakufa kisera kama walivyokufa wale wengine..Halafu muwe makini na kauli kama hizi,2010 hiyoooooo,majirani zenu watazitumia kauli hizi kuwamaliza kama walivyomalizwa wale wengine...pa1 mkuu
 
Hata wewe nakushangaa na nitazidi kukushangaa kwa mawazo yako haya MACHAFU ya kutishia kumwaga DAMU kisa CHADEMA imeshindwa uchaguzi Biharamuro

Ushaanza kuweka maneno kwenye maandishi/mawazo yangu. Au ndiyo kuishiwa hoja nini?

...Lol...Haki haidaiwi kwa Mapanga,marungu,Bunduki wala Silaha yoyote ndugu.......Unafikiri ukimwaga hiyo damu ndo CHADEMA itashinda?,thubutuuuuuuuu...

Haya sijui hata unakoyatoa.... inawezekana unahitaji miwani mkuu.

Ama na nyie mnataka muanze yale mambo ya Ngangari na Ngunguri au Jino kwa Jino??,mkianza hivyo ndo mtakufa kisera kama walivyokufa wale wengine..

Mhh ... asante sana mkuu, inaonekana una PhD ya political science. Yaani umefanya uchambuzi hadi nimekoma mwenyewe.

Halafu muwe makini na kauli kama hizi,2010 hiyoooooo,majirani zenu watazitumia kauli hizi kuwamaliza kama walivyomalizwa wale wengine...pa1 mkuu

Unajaribu sana kutumia third part kwenye maandishi yako wakati unajua kabisa unachokiongelea kinatoka kwenye nafasi ya kwanza (ambayo ni wewe mwenyewe).

Kazi kweli kweli
 
Hongera sana CCM kwa kushinda kiti cha ubunge cha jimbo la Biharamulo. Ushindi huu unadhihirisha wazi kuwa CCM ni chama kinachomika na kimbilio la wanyonge.
Aidha ninawapongeza CHADEMA, TLP kwa kushiriki katika uchaguzi huo mdogo. Kushiriki kwao kunaonesha jinsi demokrasia inavyoendelea kuimarika ndani ya nchi yetu.

CCM oyee!
 

Mhh, umeamkia wapi mwenzangu, hivi vyama vimekuwa vinashiriki chaguzi kuanzia mwaka 1995.
 
hell yes, nimekuelewa kabisa ulivyosema kwa CHADEMA haiko vijijini.



una hakika kuwa CHADEMA wamebweteka?



Unaonaje kama nawe ukiungana nao ili uwasaidie kujitangaza nchi nzima?



Katika hili, hata sikushangai.
Taratibu mazee...Ok fine CHADEMA hawajabweteka na wanajulikana nchi nzima kuliko hata CCM....Kuhusu kusaidia kuitangaza CHADEMA nchi nzima sitaweza kufanya hivyo maana kwanza sina muda huo na pili sina tabia ya kushiriki siasa za Chama chochote,ila naweza kutoa ushauri kwa chama chochote kupitia hapa JF where we dare to talk openly,sasa ni jukumu la chama hicho kuchagua ama kufuata ushauri wangu ama kuupuuza...So naomba unisamehe kama nimekukwaza mazee maana kila shemu unani attack as if nina lengo la kuichafua CHADEMA..Ina maana ni kosa kusema kuwa CHADEMA imebweteka(kwa walio na busara huichukulia hii kama changamoto na kuifanyia kazi) ama kushauri kuwa CHADEMA itumie muda huu uliobaki kujitangaza nchi nzima?????....Dah!!!,nways pa1 mkuu
 

Kweli mkuu
hizi fikira za wapi sijui eti kumwaga damu ,labda damu ya mbuzi tena fikra za namna hii zipitie mbali sana .Wazee wetu vijijini hawakututuma tuende shule ili tuje tuwahamasishe umwagaji damu.

Hayo yalikuwa kipindi cha maji maji walijifunza baada ya kipigo ndio wakatutuma twende shule tuje na soln rahisi na ya uhakika sio kurudia soln zile zile ambazo zimefeli
 
Tuachane na malumbano haya mkuu,hayana Tija yoyote..Tuendelee kumkoma nyani giladi...Pa1
 
Taratibu mazee...Ok fine CHADEMA hawajabweteka na wanajulikana nchi nzima kuliko hata CCM....

Naona unazidi kupandikiza maneno, hayo ya kuliko ccm unayasema wewe.

Kuhusu kusaidia kuitangaza CHADEMA nchi nzima sitaweza kufanya hivyo maana kwanza sina muda huo na pili sina tabia ya kushiriki siasa za Chama chochote

Mhh, pamoja na uchambuzi wa nguvu ulioutoa hapa bado huna muda wa kushiriki kwenye siasa za chama chochote? Tafadhali weka talent yako pale inapostahili mkuu. Uchambuzi wako (hasa kuhusu CHADEMA) sio mchezo.


Wewe sasa una lako jambo na hizo attacks zako. Umeshasema kuwa watu wana-talk openly ..... si ndiyo?

Ina maana ni kosa kusema kuwa CHADEMA imebweteka(kwa walio na busara huichukulia hii kama changamoto na kuifanyia kazi) ama kushauri kuwa CHADEMA itumie muda huu uliobaki kujitangaza nchi nzima?????....Dah!!!,nways pa1 mkuu

Ukiona sehemu yoyote nimekuambia kuwa unakosea kwenye uchambuzi wako makini naomba uiweke hapa nami nitakuomba msamaha. Kinachofanyika hapa ni uchambuzi wa kile unachoandika kwa kadri wewe unavyochambua vya wengine.

Take it easy mkuu ..... hiyo ndiyo kawaida ya JF ... kwa muda mrefu sasa.
 
................................Pa1
 

Tanzania kweli nchi ya kijamaa ... kuna watu bado wanatumwa na vijiji vyao kwenda shule!
 
Tuachane na malumbano haya mkuu,hayana Tija yoyote..Tuendelee kumkoma nyani giladi...Pa1

Malumbano ? far from it.

Shule yako ni muhimu sana mkuu, tafadhali sana usiache kuendeleza uchambuzi wako. Wanachadema watauhitaji sana wakati huu wanapouguza vidonda vya "kushindwa" B'mulo
 
Malumbano ? far from it.

Shule yako ni muhimu sana mkuu, tafadhali sana usiache kuendeleza uchambuzi wako. Wanachadema watauhitaji sana wakati huu wanapouguza vidonda vya "kushindwa" B'mulo
..............................Pa1
 
Chadema poleni kwa kulikosa Jimbo lkn Hongereni kwa graph yenu kupanda ya kupata kura za wananchi...kwani hili Jimbo lilikuwa la TLP.

Wapinzani watakiwa kujifunza Makosa yapo wapi...otherwise itakuwa ni wasindikizaji tu. Tatizo la kwanza ni Tume ya Uchaguzi.

CCM wamefanikiwa kwa propaganda ambazo imewapakazia Vyama vya Upinzani...the so called "Upinzani" wenyewe wamekuwa wapinzani kwa wapinzani...na Hapa ndipo CCM ilipofanikiwa....kibaya atakae UMIA ni mwananchi wa kawaida.

as long as Tume ni hii hii....wapinzani/Wananchi wasitarajie Mapya!!!!
 
Inamaana CHADEMA imeshindwa ,kule mwanzo nilisoma na kuona watu wengi wanaisakama CUF, sijui kwa nini ,ila hisia zinaonyesha kuwa CUF ni tishio hata katika vyama vilivyo upande wake wa upinzani.
Baada ya kukaa na kuratibu kinachoendelea wameivamia CUF matokeo yake CCM anaondoka na kapu la kura taratibu na kulikarabati.

Hivi tunaposema matokeo ya Uraisi ,Wabunge na Wawakilishi kule Zanzibar huwaga yanabadilishwa na tume ya uchaguzi mlizani tunatania ?

Mnapoambiwa CUF mara zote inashinda uchaguzi wa Zanzibar kuanzia wa Uraisi mpaka wa Udiwani ,mnaonana mnadanganywa ,CUF ni wagonvi ,walafi wa madaraka au sio ?

Basi kwa taarifa yenu CCM imepima wizi wa kubadilisha matokeo kwa upande wa Tanganyika (Hakuna Tanzania Bara kwenye makubaliano ya Muungano,mnielewe) hivyo kipimo hicho ndicho kitakachotumika ,na kwa wale waliozoea kutokuwa tayari kwa lolote kwa kuogopa kuwa damu itamwagika basi msahau ushindi .

Kuiong'oa CCM kunahitajika nguvu za ziada kushinda zilizotumika Kenya au Zimbabwe maana hao akina Zimbabwe na Kenya ,Tz ni baba yao ,sasa ikiwa watoto wamekurupushwa kwa mbinde ,je CCM Baba ,si mnawasikia wakiimba CCM baba ,baba uyoo ! Akili kichwani mwenu ,ila kwa kuongezea akiba ya maneno ,vyama vya upinzani upande wa Tanganyika zi lazima viwaandae wanachama wake kwa lolote lile na sio lelemama kutegemea ushindi wa kugaiwa.

Zanzibar CUF imefanikiwa kuwaandaa wanachama wake ,zoezi la kuwakusanyanya wananchama wake kudai haki yao kwa mass people(Power of the people) pale Mjini Unguja lilifanikiwa (Ule ulikuwa mwito tu wa kujaribisha kama watu wanaweza kuitikia na nyote mmeona na CCM wameona) ,sasa pale palikuwa hapana mipango yoyote ile zaidi ya CUF kuipima nguvu yao kwa siku zijazo ,sasa kama kukiwa na mipango watu hawatakusanyika tena makao makuu bali itakuwa kujigawa kila kona na pembe ya Zanzibar Pemba na Unguja ,ikiwa Pemba peke yake ,serikali ilibidi iagizie polisi kutoka DSM ,je ikichafuka Zanzibar nzima ?

Ni lazima wananchi waandaliwe kupambana kikweli na sio ya anao anao ! Siku zote atakuwa nao CCM kama upinzani nao haukujiandaa kucheza rafu ,tena rafu za kweli ili kumng'oa Baba 😀
 

Kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…