Inamaana CHADEMA imeshindwa ,kule mwanzo nilisoma na kuona watu wengi wanaisakama CUF, sijui kwa nini ,ila hisia zinaonyesha kuwa CUF ni tishio hata katika vyama vilivyo upande wake wa upinzani.
Baada ya kukaa na kuratibu kinachoendelea wameivamia CUF matokeo yake CCM anaondoka na kapu la kura taratibu na kulikarabati.
Hivi tunaposema matokeo ya Uraisi ,Wabunge na Wawakilishi kule Zanzibar huwaga yanabadilishwa na tume ya uchaguzi mlizani tunatania ?
Mnapoambiwa CUF mara zote inashinda uchaguzi wa Zanzibar kuanzia wa Uraisi mpaka wa Udiwani ,mnaonana mnadanganywa ,CUF ni wagonvi ,walafi wa madaraka au sio ?
Basi kwa taarifa yenu CCM imepima wizi wa kubadilisha matokeo kwa upande wa Tanganyika (Hakuna Tanzania Bara kwenye makubaliano ya Muungano,mnielewe) hivyo kipimo hicho ndicho kitakachotumika ,na kwa wale waliozoea kutokuwa tayari kwa lolote kwa kuogopa kuwa damu itamwagika basi msahau ushindi .
Kuiong'oa CCM kunahitajika nguvu za ziada kushinda zilizotumika Kenya au Zimbabwe maana hao akina Zimbabwe na Kenya ,Tz ni baba yao ,sasa ikiwa watoto wamekurupushwa kwa mbinde ,je CCM Baba ,si mnawasikia wakiimba CCM baba ,baba uyoo ! Akili kichwani mwenu ,ila kwa kuongezea akiba ya maneno ,vyama vya upinzani upande wa Tanganyika zi lazima viwaandae wanachama wake kwa lolote lile na sio lelemama kutegemea ushindi wa kugaiwa.
Zanzibar CUF imefanikiwa kuwaandaa wanachama wake ,zoezi la kuwakusanyanya wananchama wake kudai haki yao kwa mass people(Power of the people) pale Mjini Unguja lilifanikiwa (Ule ulikuwa mwito tu wa kujaribisha kama watu wanaweza kuitikia na nyote mmeona na CCM wameona) ,sasa pale palikuwa hapana mipango yoyote ile zaidi ya CUF kuipima nguvu yao kwa siku zijazo ,sasa kama kukiwa na mipango watu hawatakusanyika tena makao makuu bali itakuwa kujigawa kila kona na pembe ya Zanzibar Pemba na Unguja ,ikiwa Pemba peke yake ,serikali ilibidi iagizie polisi kutoka DSM ,je ikichafuka Zanzibar nzima ?
Ni lazima wananchi waandaliwe kupambana kikweli na sio ya anao anao ! Siku zote atakuwa nao CCM kama upinzani nao haukujiandaa kucheza rafu ,tena rafu za kweli ili kumng'oa Baba 😀