Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Tusiwaendekeze hawa CCM, tuwaonyeshe si rahisi kuiba kura. wakiwa wanaachwa itaendelea kuwa ndio mchezo wao
 
Yaani watanzania haki inaminywa tunanyamaza kikondoo kweli hakuna nchi duniani yenye mazingira mazuri kwa ustawi wa ufisadi kama Tanzania, kwa mwendo huu kushinda mafisadi ni ndoto!
 
Nashindwa kushangaa na napigwa na bumbuwazi. Hasa hasa aliyeshinda Biharamulo ni CHADEMA au CCM. Habari zinakanganya hizi. CCM stuka! Hizo ni salamu za 2010!
 
Kule znz kwanza walianza kupigwa mapanga watu weupe,watu weusi wakaelewa wanaopigwa ni weupe tu,wao ndo wenye nchi,eh! wakaanza kupigwa watu weusi,tanganyika wakaelewa wanaopigwa ni waznz tu kwani ndo wenye vurugu,oh! mara wakaanza kupigwa tunduru,eh! mara mbeya wahaya,mara wasukuma kule busanda,

Duh! kazi kweli kweli,kumbe mwanzo watu walikuwa hawajui kuwa utapigwa ikiwa utaikataa ccm tu,lkn sio kwa rangi,kabila,dini wala cheo chochote,muhimu ikiwa wewe umeikataa ccm basi mapanga yatakukuta tu..

Hiyo ndio ccm na wameapa na hata kuthubutu kuongea hadharani kuwa serikali haitoki kwa kipande cha karatasi,duh! sasa sijui niseme Chadema wamepoteza mwelekeo au vipi,maana Cuf wakisema wameibiwa waliambiwa wamepoteza mwelekeo, kwa nini chadema wasiwaachie TLP kule Biharamulo kwa kuwa TLP ndio inakubalika kule,Y? wakakusanya nguvu pamoja kuiondoa ccm. doooooh! hii ndio Tz, Chadema waliwaambia Cuf upepo umebadilika,kweli upepo umebadilika kwa hali hii?

Ikiwa hatujakaa pamoja waTz wote,tukaunganisha nguvu zetu unafkiri tutaishinda ccm,abadan.. tutabaki kulalamika siku zote tumeibiwa.. lazima tuwe kitu kimoja na tena basi sio turidhike na kura tunazopiga bali tuhakikishe kila kura yake anailinda kwa njia yoyote...
UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI DHAIFU
 
Last edited:
Sio lazima kuwe na tume huru wala nini wafanykazi wote wakiacha kazi na mtanzania yoyote akakataa kazi mpaka ccm itakapong'oka mbona ni tiba tena ya week tu


Ndugu yangu hadi hapo, kwakweli umechangia very low.
Kama unadai kwamba wazee wako vijijini walikutuma ukasome upate elimu kisha uje kuwasaidia kuondokana na hali duni, na hapo juu umeonyesha kuwa umesoma kama ulivyotumwa na wazee wako.
Lakini ghafla unapogeuka na kutoa hoja dhaifu kama hii, nabaki kuwaonea huruma hao wazee wako huko kijijini. Watakuwa wamekula hasara kama hali yenyewe ndio hii.Tangu mwanzo nilikuwa nasoma post zako naona kama una kitu cha maana unataka tukifahamu toka kwako, pamoja na mapenzi yako ya dhati kwa ccm, lakini kwa ushauri huu, umejishusha mno. Pole sana yego mwamba.
 

Mwiba, unataka iwe kama Tarime?
 
Mimi nilichoka vibaya na kulegea vibaya sana kwa ajili ya matokeo hayo hivyo ni bora kutokuwa na uchaguzi huo
 
Baada ya kuona zile takwimu zilizopelekwa JF especially na Invisible zikidhihirisha ushindi wa Chadema (17313) dhidi ya CCM (16682) na TLP (187), tulianza kushangilia.

Ucheleweshaji wa kutanganza rasmi matokeo, ambapo eti wakala wa Chadema walighairi na kuwaachia Msimamizi wa Uchaguzi na CCM kuingiza kura za kughushi ndio vimesababisha ccm kutangazwa mshindi. Demokrasia gani hii?????

Hata hivyo Mchungaji mmoja anayefahamu mimi ni mshabiki wa Chadema amenitumia ujumbe wa simu akisema "Chadema chama chetu, Mungu atakisaidia. Ipo siku tutakesha tukishangilia ushindi. Tuombe Mungu atuimarishe, na ccm awasamehe. Kwa Mungu yote yanawezekana".

Hii ni changamoto kwa Watanzania wapenda haki, amani na maendeleo. Hakuna kulala. Iko siku tutashinda.
 
Mukasa keshatangazwa mshindi. Hakuna sababu ya watu kuumia sana au kuwa na anza na hisia ya kuona kuonewa. Japo kuwa hisia hizo zina msingi uhalisia unatulazimisha kukubali kuwa njia ya kuelekea demokrasia haiwezi kuwa mteremko hivyo.

Demokrasia ni mapambano.
 

Mkuu
mimi nafikiri njia nzuri ya kumkoti mtu ni ukoti yote harafu upigilie mstari sehemu panapo kupa duku duku ,hii tabia nafikri sio nzuri sana ya kunukuu nusunusu.

Mimi nimesema kama kweli mnawafuasi wengi watoweza kumwaga damu yetu Basi hiyo nawashauri si njia sahihi nakama mnaweza hilo basi wito kwangu kwenu ni bora mhamasishe wafanyakazi na watanzania wagomee kufanya kazi si mnaungwa mkono na watanzania wanyonge nadhani mtafanikiwa zaidi kuliko kumwaga damu mkuu wangu.

Angalia UKRAINE walifanya nini kama kweli mnaungwa mkono kisawa sawa TUME HURU si hoja kabisa itakuja yenyewe tu ,hebu waambieni wafuasi wenu wote wagome kwenda kazini si wafuasi wenu ni watanzania wanyonge ama vipi? serikali itatulia yenyewe.
Kinyume chake hamna wafuasi mnaotaka watu wawaamini mnao na wala huko kuonewa mnakoku amplify hakuko ktk magnitude mnayotaka tuamini.
 
CHADEMA kubalini matokeo na mujiandae na uchaguzi wa serikali za mitaa. Msitumie nguvu kwani makosa kama yamefanyika kwa kutokukaba penati basi next time hakuna kutoa mwanya. Wafuasi wenu waelimishwe kutoamini mtu hivyo ni kukaba mpaka mwisho. Mpaka hapa mnastahili pongezi kwakweli chadema inaonekana kujulikana kwake kunaongezeka hilo ndilo la muhimu hivyo inabidi mkakati wa kukifanya chama kifahamike usibadilike ila mkakati wa kukifanya chama kishinde chaguzi inabidi uangaliwe upya ili kuwabana CCM. NA PIA HII KAULI YA CCM INAKUBALIKA ZAIDI VIJIJINI INABIDI IFANYIWE KAZI ISIJE WAKAWA WANACHEZA FAULO. CHAMA KIJULIKANE KILA SEHEMU. Vitengenezwe hata vipeperushi watu wapewe ili uwe kama mwimbo.

POLENI SANA KWA FAULO ILIYOCHEZWA LAKINI REFA KAKUBALI GOLI HIVYO NI KUPANGA MASHAMBULIZI KUSAWAZISHA.
 
Naungana na wazalendo wengine kwa ajili ya CHADEMA!! I tolf you guys kuwa chama mbadala cha Tanzania ni CHADEMA, wanaweza na wameweza, ila tunahitaji support zenu wakuu
 

Poti,
Pamoja na kukubali "ushauri" wako wa ku-quote yote lakini siwezi kuzungumzia neno kwa neno kama ulivyojadili. Mimi nimejaribu kuzungumzia hoja mojawapo uliyoitoa na ambayo umeirudia tena hapa. Yaani ni kusema kwamba tuendelee tu kutokuwa na tume huru ya uchaguzi?kama kweli umesoma na unapenda maendeleo ya demokrasia huwezi kamwe kutetea kuendelea/kushikilia tume ya uchaguzi iliyo biased, tume isiyo huru kabisa, tume inayokitumikia ccm na kuhakikisha kuwa hakishindwi.
ushauri wa kususia kazi nao ni low(samahani kwa hilo) kwa kuwa unategemea hao wafanyakazi watajimudu vipi?unadhani wapenda mageuzi wote ni wafanyakazi wa serikali ya ccm kama unavyodhani?je ni wapi hiyo style ya kususia kazi iliwahi kufanyika na ikafanikiwa?
halafu poti wangu usipende ku-generalise mambo, mimi kuwa na mawazo tofauti na yako haimaanishi kuwa mimi ni mchadema kama wewe ulivyo m-ccm.Na kama huu mfumo dhalimu wa kuwa na tume ya uchaguzi isiyo huru unanufaika nao, basi waache wale wasionufaika nao waseme.Mimi nitakuunga mkono na mguu ikiwa kutakuwa na jukwaa lililo sawa kwa vyama vyote kuendesha siasa na mwisho wa yote kuwe na mwamuzi(tume ya uchaguzi iliyo huru) asiye na mahaba na chama chochote.
 
CHADEMA mnapofanya tafakuri ya kushindwa huko B'mulo pia tafakarini sana mwenendo wa mpiganaji wetu mmoja mashuhuri ndani ya chama chenu- nadhani anatumikia mabwana wawili- ushahidi unaendelea kukusanywa ikiwa tayari tutaumwaga hapa na pia wengine wenye kulijua hilo karibuni
 
Fafanua hii sijaelewa
 
Sema ni nani hapa ni ni ukweli na uwaza na sisi kama ni tuhuma ni za kweli tutajua kama ni kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…